Huyu Mzee ndio Mjanja aliowatoa kwenye Ushamba wa kudhani kuwa na Fridge au TV ni kosa kisheria!
Marehemu Mzee wangu alinyang'anywa Fridge Airport ya Dsm akitokea kwenye Course fupi huko Nertheland kwa kuwa haikuruhusiwa kumiliki TV wala Fridge, gari kumiliki ni mpaka kibali cha RC na Tena uoneshe sababu za Msingi Kwanini unataka kuwa na gari na longolongo kibao, mfano Mikoa Kama Singida ili upate kibali ilikuwa lazima gari lisiwe na mmiliki Mmoja!
Kizazi cha awamu ya kwanza wajukuu wake ndio Watawala wa Sasa kwao Hata kwenda Pritoria na Familia nyakati za Likizo ni uhujumu Uchumi
Nashukru sana sehemu yote ya Utumishi wangu Serikalin ilikuwa Wakati wa Mzee Mwinyi, Mzee Mkapa na Mzee Mashuhuri toka Msoga!