Tuliokuwepo enzi za utawala wa Ali H Mwinyi tukutane hapa!

Tuliokuwepo enzi za utawala wa Ali H Mwinyi tukutane hapa!

Binafsi ingawa umri wangu ulikuwa sio mkubwa sana lakini kwa kiasi kikubwa nilishuhudia mabadiliko makubwa ya maisha!

Mwanzo TV tulikuwa tunaenda kuangalia kanisani (mission).

Tuliacha kuvaa mawingu na kaniki tukaanza kuvaa nguo Nzuri za mtumba!

Tuliacha kununua vitu kwny maduka ya ushirika, watu wengi walianzisha maduka mitaani!

Shule za binafsi nyingi zilianzisha!

Enzi zile kutembea ukaokota pesa barabarani Ilikuwa kawaida sana, (enzi hizo sarafu za Tsh 5, 10 na 20.

Hebu wa enzi hizo tukumbushane matukio mbalimbali yaliyotokea chini ya utawala wa mzee wetu Ali Hassan Mwinyi.

Awamu yake ndiyo iliwafanya Wahindi na Waarabu waanze kuwa na ' Jeuri ' kubwa na ' Nyodo ' ndani ya nchi hii huku Dawa za Kulevya ndiyo zikianza kushika kasi nchini ambapo ' Wakubwa ' wake kadhaa waliokuwa katika Serikali yake walikuwa wakijihusisha nazo. Naomba niishie hapa tafadhali.
 
Huyu Mzee ndio Mjanja aliowatoa kwenye Ushamba wa kudhani kuwa na Fridge au TV ni kosa kisheria!

Marehemu Mzee wangu alinyang'anywa Fridge Airport ya Dsm akitokea kwenye Course fupi huko Nertheland kwa kuwa haikuruhusiwa kumiliki TV wala Fridge, gari kumiliki ni mpaka kibali cha RC na Tena uoneshe sababu za Msingi Kwanini unataka kuwa na gari na longolongo kibao, mfano Mikoa Kama Singida ili upate kibali ilikuwa lazima gari lisiwe na mmiliki Mmoja!

Kizazi cha awamu ya kwanza wajukuu wake ndio Watawala wa Sasa kwao Hata kwenda Pritoria na Familia nyakati za Likizo ni uhujumu Uchumi

Nashukru sana sehemu yote ya Utumishi wangu Serikalin ilikuwa Wakati wa Mzee Mwinyi, Mzee Mkapa na Mzee Mashuhuri toka Msoga!
Utawala wa mwanzo ndo ulituletea umasikini kutokana na Sera za kimasikini za kijamaa,maana vitu muhimu vilionekana ni anasa,Sera za kijamaa zilizalisha walevi na wazinzi ikiwemo ndoa nyingi za mitaala maana ukiwa na hela ya ziada ukuruhusiwa kumiliki mali,hivo lzm uzitumie kwenye ulevi au kuhonga malaya. Ndio maana nyingi nyingi za kariakoo zilikuwa za wakinamama wengi walihongwa na makuli wa Bandari au watumishi wengi.
 
Na Kingunge ndio alikuwa Mkandarasi wa Azimio la Arusha
Tunawaaadhimisha sana Waasisi wa Umaskini na Ujinga wetu
 
ni kweli japo nilikua shule niliyaona hayo yalikua mazuri Mitumba wazazi wakaanza kutununulia tulifurahi mno
 
Enzi hizo ndo sukari iliingia sumu.

Watanzania nia wezangu sukari imeingia sumu. Kauli ya Mzee wetu Ally Hassan Mwinyi

Hahahaha misemo tata ya Mzee Mwinyi

Nzi kafia Dondani

Wa Morogoro kazaneni kwenye Mihogo Kama Wahaya wanavyokazana kwenye Migomba!
 
Awamu yake ndiyo iliwafanya Wahindi na Waarabu waanze kuwa na ' Jeuri ' kubwa na ' Nyodo ' ndani ya nchi hii huku Dawa za Kulevya ndiyo zikianza kushika kasi nchini ambapo ' Wakubwa ' wake kadhaa waliokuwa katika Serikali yake walikuwa wakijihusisha nazo. Naomba niishie hapa tafadhali.
Nafikiri awamu hii Ilikuwa Ruksa kufanya kila unachojisikia kufanya.

Mzee aliruhusu watu wawe huru, Ilikuwa furaha kwa wengi maana mzee Mwalimu aliwabana sana watu Toka nchi inapata uhuru.

Ingawa uhuru huu wa manyani ulikuwa na Madhara kadhaa kwa taifa!
 
Utawala wa mwanzo ndo ulituletea umasikini kutokana na Sera za kimasikini za kijamaa,maana vitu muhimu vilionekana ni anasa,Sera za kijamaa zilizalisha walevi na wazinzi ikiwemo ndoa nyingi za mitaala maana ukiwa na hela ya ziada ukuruhusiwa kumiliki mali,hivo lzm uzitumie kwenye ulevi au kuhonga malaya. Ndio maana nyingi nyingi za kariakoo zilikuwa za wakinamama wengi walihongwa na makuli wa Bandari au watumishi wengi.
Umeongea kweli
 
Awamu yake ndiyo iliwafanya Wahindi na Waarabu waanze kuwa na ' Jeuri ' kubwa na ' Nyodo ' ndani ya nchi hii huku Dawa za Kulevya ndiyo zikianza kushika kasi nchini ambapo ' Wakubwa ' wake kadhaa waliokuwa katika Serikali yake walikuwa wakijihusisha nazo. Naomba niishie hapa tafadhali.
In any capitalist country hayo mambo lazima yawepo refer China licha ya sheria kali lkn madawa yanaingia

Sabb kubwa ya madawa kuanza kuingia kipindi chake ni baada ya wananchi kuruhusiwa ku-import bidhaa jamba ambalo awamu ya kwanza individual was prohibited to own any wealth or import things under the umbrella of ujamaa ..

Ili madawa yasiingie nchini basi Magu afunge bandari no more importation tena kwa wafanyabiashara tuwaige marafiki zetu wa zamani North Korea huwezi kukuta heroine ,cocaine kule
 
Rupia walikuwa wanaishi kama malaika walahi!
Kuna liaharusi la mtoto wake alio mtoto wa Kahama nadhani!
Ilikuwa pata shika!
Mwinyi kawekwa katikati ya bwana na bibi harusi!
Duh!
Sasa hivi ndiyo hao wanaishi kama mashetani, ndoa bye bye!
Mhhh!
Dunia hii!
Mwenye Enzi Mungu tuongoze!
 
Mzee Mwinyi alikuwa mwenye busara, hekima na ustahamilivu mkubwa hasa kwa wale waliyompinga na kumtukana, alikuwa akishaurika na wala hakurupuki, alipokea kijiti cha uraisi wakati nchi ilikuwa ikihitaji mabadiliko makubwa ya kisiasa na kiuchumi kutokana na shinikizo la mataifa makubwa yaliyokuwa yakisaidia nchi maskini.
 
Akaamua kutuletea kunguru weusi wa Pakistan ili wale matakataka, pathetic, maana wakala mpaka ndege na mayai yote karibu ya ndege asilia! Hicho kitu nakilaani sana!
Mpaka ikabidi UN iingilie kati kuua hao kunguru wa Pakistan! Heri sasa wamepungua na ndege wa asili wanarudi!
Kumbe walikuja kipindi cha ruksa!? nilikuwa sijui
 
Back
Top Bottom