Tuliokuwepo enzi za utawala wa Ali H Mwinyi tukutane hapa!

Tuliokuwepo enzi za utawala wa Ali H Mwinyi tukutane hapa!

BIGURUBE

JF-Expert Member
Joined
Mar 11, 2014
Posts
6,748
Reaction score
4,252
Binafsi ingawa umri wangu ulikuwa sio mkubwa sana lakini kwa kiasi kikubwa nilishuhudia mabadiliko makubwa ya maisha!

Mwanzo TV tulikuwa tunaenda kuangalia kanisani (mission).

Tuliacha kuvaa mawingu na kaniki tukaanza kuvaa nguo Nzuri za mtumba!

Tuliacha kununua vitu kwny maduka ya ushirika, watu wengi walianzisha maduka mitaani!

Shule za binafsi nyingi zilianzisha!

Enzi zile kutembea ukaokota pesa barabarani Ilikuwa kawaida sana, (enzi hizo sarafu za Tsh 5, 10 na 20.

Hebu wa enzi hizo tukumbushane matukio mbalimbali yaliyotokea chini ya utawala wa mzee wetu Ali Hassan Mwinyi.
 
ab5c584adb5f9160e729018768c4c27b.jpg

nimetumia sana enzi ya ruksa
 
Naona mnaitana wahenga..wengine tumezaliwa ngwe ya mwisho kabisa ya utawala wake...hapatuhusu hapa! naskia gari zilikua zonapita juu ya mlima Wa takataka..*****
Akaamua kutuletea kunguru weusi wa Pakistan ili wale matakataka, pathetic, maana wakala mpaka ndege na mayai yote karibu ya ndege asilia! Hicho kitu nakilaani sana!
Mpaka ikabidi UN iingilie kati kuua hao kunguru wa Pakistan! Heri sasa wamepungua na ndege wa asili wanarudi!
 
Ulikuwa utawala mzuri kwa wakati muafaka,nchi iliingia kwenye utandawazi na bidhaa za nje ziliingia tanzania kwa wingi na kuleta manufaa makubwa.Kitu kibaya ni kuwa serikali haikuwa na hela ila wananchi walijaa mapesa.
 
Akaamua kutuletea kunguru weusi wa Pakistan ili wale matakataka, pathetic, maana wakala mpaka ndege na mayai yote karibu ya ndege asilia! Hicho kitu nakilaani sana!
Mpaka ikabidi UN iingilie kati kuua hao kunguru wa Pakistan! Heri sasa wamepungua na ndege wa asili wanarudi!
Lakini historian inaonyesha kunguru alipewa kama zawadi ha ha kumbe kapewa kimba!
 
Ahhha ngojea maOT waje ,mimi Mwinyi anamaliza term yake ya pili 2 nlkuwa mdogo

Huyu Mzee ndio Mjanja aliowatoa kwenye Ushamba wa kudhani kuwa na Fridge au TV ni kosa kisheria!

Marehemu Mzee wangu alinyang'anywa Fridge Airport ya Dsm akitokea kwenye Course fupi huko Nertheland kwa kuwa haikuruhusiwa kumiliki TV wala Fridge, gari kumiliki ni mpaka kibali cha RC na Tena uoneshe sababu za Msingi Kwanini unataka kuwa na gari na longolongo kibao, mfano Mikoa Kama Singida ili upate kibali ilikuwa lazima gari lisiwe na mmiliki Mmoja!

Kizazi cha awamu ya kwanza wajukuu wake ndio Watawala wa Sasa kwao Hata kwenda Pritoria na Familia nyakati za Likizo ni uhujumu Uchumi

Nashukru sana sehemu yote ya Utumishi wangu Serikalin ilikuwa Wakati wa Mzee Mwinyi, Mzee Mkapa na Mzee Mashuhuri toka Msoga!
 
Ouch aisee!
 
'JF is where we dare to talk openly'

Unajua tafsiri ya kimantiki ( sio kilugha) ya Maneno haya?

Kwahiyo kimtindo ndogo wa expansion joints angetupiamo yale mapicha humu ingekuwa mzuka tu kumbe?

Ahsante kwa kunijuza mkuu
 
Back
Top Bottom