Tuliomtetea Kabendera tumwombe radhi mwendazake, Naanza na Pascal Mayalla nisamehe Mkuu

Tuliomtetea Kabendera tumwombe radhi mwendazake, Naanza na Pascal Mayalla nisamehe Mkuu

Wewe unamshangaa Kabendera tu? Vipi kuhusu LHRC ambao wameteswa kwa miaka mi5 na Jiwe akisaidiwa na Polepole, accounts zao zikafungwa, baadhi ya wafanyakazi wao wakatekwa na kubambikiwa kesi! Wapinzani (especially CDM) wakapiga kelele sana kuwatetea!! Leo hii hao hao LHRC wamebadilika, wanawakumbatia walewale waliowatesa, wamesahau kila kitu kwa muda wa miezi 9 tu!! LHRC hawakuwa watu wa kumkaribisha Polepole hadi chumbani na kumpa platform ya kuongea aliyoongea (Ikiwemo kudai uhuru wa kuongea!!!)! Sometimes TZ bora kufanya yanayokuhusu, Brains za watu wengi zimeshikiliwa na tumbo
 
Utashangaa wengine waliokimbia nchi kwa kuogopa jela wanashauri Mbowe aendelee kukaa jela sababu hana kosa.

Maumivi na mateso ya mwenzio huwezi kuyahisi kama yeye. Wamuache Mbowe afanye anachohisi kina faida kwake.
Kinachoshangaza zaidi ni majitu ya ccm
Kumuonea huruma ya kinafiki kamanda Mbowe
 
Sio kwamba kila mhanga wa sera za mwendazake na watawala wa aina yake ni mwanaharakati au mwanasiasa.

Huyu ni mtu alikuwa tu ana practice taaluma yake ya uandishi wa habari kwa dau refu na akafanyiwa fitina zilizoendana na mazingira ya kisiasa ya nyakati hizo.

Wapo wengi tu kama yeye ambao figisu za kuswekwa ndani ziliwanyong’onyeza mapema wakakubali kukiri
makosa wasiyoyajua wala kuyatenda na kulipishwa tozo za kimafia ili tu watoke jela wajumuike na wapendwa wao na kuendelea na mambo mengine ya maisha yao.

Roho jasiri kama za Rugemalira na Mbowe ni vito adimu sana katika jamii yoyote ile hapa duniani.
 
👇👇👇👇🤣🤣🤣

IMG_20211103_093523.jpg
 
Baada ya kuomba radhi Kabendera kapungua nini au ni kipi kimepungua kutoka kwake
Tofauti ya Mbowe na kabendera ni credibility zao...Mbowe ni mwanaSiasa kesi waliyompa akiomba msamaha manake atakuwa amethibisha kosa lake ...Chama kitakuwa wapi? Kabendera katoka Jela anakula ugali wake hakuna anaemuuliza so huo ndio utofauti...kumbuka
hao ccm wamekaa kimya sababu imewakaa vibaya acha Mbowe aombe radhi atoke kwa mkono wa ccm halafu wakutane kwenye Kampeni za Siasa ndio unaweza kuelewa kwanini Chadema wanatoa povu
 
Mkuu ungefatilia hiyo story ya richard nixon na msamaha wa gerard ford....

Kuomba msamaha kwa kosa ambalo hukulifanya ni dalili za unafiki na uchumia tumbo na mbaya zaidi ni kuonekana huna msimamo. Mandela alikaa jela 27 years ,walter sesulu 25 years , hawakuwahi kuomba msamaha , japo kina winnie na wenzake
walikuwa wakiwasihi wakubali makosa ili wawe huru , had the two had compromised ,pengine kusingekuwa na south Africa tuijuayo hii leo

The term "mwanaharakati " comes with it hefty commitment, if one is not up to par with it ,ni bora kufanya kitu kingine .
Acha kupotosha. Winnie Mandela hakutaka kabisa mandela aombe msamaha. Tena hakutaka kabisa kuwe na mapatano kati ya wazungu na weusi. She was very radical on that.....
 
Sijaona alichokosea Kabendera, sema kwakuwa ni ruksa kutoa maoni yako tumeyasikia. Kiukweli nawashangaa ambao mnataka Mwenyekiti anendelee kukaa gerezani wakati watu wameshaomba wakuu waangalie namna ya kulimaliza hili, kipi hasa mnachokitaka?

Familia yake itakuwa inamuhitaji sana waweze kufurahia Christmas na mwaka mpya.
Labda hujalewa au unafanya kusudi kuhusu concept ya Chadema
 
Hawa watu hawaeleweki wanataka nini hasa,hata suala la Mnyika kuzungumza na Mangula ili hili jambo lishughilikiwe,nadhani anatafutiwa timing tu,naye atashambuliwa sana tu
Wanachotaka Chadema Mbowe aachiwe bila mashart yakuomba MSAMAHA maana hakuna kesi pale ni UPUMBAVU tu
 
Kinachoshangaza zaidi ni majitu ya ccm
Kumuonea huruma ya kinafiki kamanda Mbowe
Kumshauri mhanga afanye anchotaka yeye si kumuonea huruma.
Ninyi mashujaa wa mitandaoni ambao mko huru mnakula kunywa na kuwa karibu na familia zenu mnataka mwenzenu aoneshe ushujaa kwa gharama ya mateso makubwa.

Mkiombwa muandamane aachiwe mnaogopa kukamatwa na kwenda jela mnakomshauri aendelee kukaa. Ninyi hamtaki kuwa mashujaa?
 
Mkuu ungefatilia hiyo story ya richard nixon na msamaha wa gerard ford....

Kuomba msamaha kwa kosa ambalo hukulifanya ni dalili za unafiki na uchumia tumbo na mbaya zaidi ni kuonekana huna msimamo. Mandela alikaa jela 27 years ,walter sesulu 25 years , hawakuwahi kuomba msamaha , japo kina winnie na wenzake
walikuwa wakiwasihi wakubali makosa ili wawe huru , had the two had compromised ,pengine kusingekuwa na south Africa tuijuayo hii leo

The term "mwanaharakati " comes with it hefty commitment, if one is not up to par with it ,ni bora kufanya kitu kingine .
Sio kila kitu kiwekwe wazi. Huwezi kuambiwa walikubalianaje nyuma ya pazia
 
Alaaaaaa kumbe ni kweli Kabendera alifanya makosa makubwa sana kwa Taifa mpaka akaombewa msamaha - shame on him!!

Sisi tuliokuwa tunamtete tulifikili alionewa na Mwendazake!!! - shame on us!!
Ukiwa nje unajikuta shujaa, unajikuta huwezi kuomba msamaha kwa kile qmbacho hujatenda ili mradi utoke ndani. Ukiwa ndani unaloyaka ni kutoka nje tu kwa njia yoyote. Inafika muda uko tayari hata kukubali lolote ili uachiwe. Ndiyo maana watu wengi walikubali kuingia makubaliano ma dpp ili mradi waungane na familia zao.
Wanakutesa kisaikolojia. Mama yake alifariki na hakuruhusiwa kuhudhuria hata msiba. Hujui ni maneno gani na vitesho alivyokuwa akipewa.
Shukuru Mungu hujapitia alichokipitia.
Kuna watu uwa wanakiri hata kuua kwa kukaa tu na polisi wakafanyiwa mahojiano kumbe hata hawajaua. Na huko ni Marekani ambako polisi hakupigi katika mahojiano lakini kile kitendo cha kukaa na polisi masaa mengi mtu anajikuta anachoka akili anakubali kila wanachotaka kusikia.
 
Sijaona alichokosea Kabendera, sema kwakuwa ni ruksa kutoa maoni yako tumeyasikia. Kiukweli nawashangaa ambao mnataka Mwenyekiti anendelee kukaa gerezani wakati watu wameshaomba wakuu waangalie namna ya kulimaliza hili, kipi hasa mnachokitaka?

Familia yake itakuwa inamuhitaji sana waweze kufurahia Christmas na mwaka mpya.
Wanaosema hivyo wanasema kwakuwa wako nje, ingekuwa wao wangeshaomba msamaha mapema. Watu nyuma ya keyboard wanajitia ushujaa sana
 
Kuna wakati dola inajua mengi kuliko tuyajuayo, kuna hizi siasa tunazopigia domo kila siku halafu kuna dola ambayo iko kimya inaangalia mambo yanavyokwenda na kuhakikisha watu wanakuwa salama....Dola kuna wakati humshauri Rais juu ya mambo fulani fulani nyeti ambayo sisi raia hatuwezi kuyajua...
 
Back
Top Bottom