Tuliopitia maisha ya "Saidia Fundi" tukutane hapa

Tuliopitia maisha ya "Saidia Fundi" tukutane hapa

Mwanga Lutila

JF-Expert Member
Joined
Nov 10, 2016
Posts
4,208
Reaction score
14,143
Hii mikazi sidhani kama kuna mtu anapenda kuifanya ila kuna stage ilitubidi wengine tufanye ili tusukume siku.

Wapo ambao zimewatoa, na tupo ambao hazikututoa.

Niliacha hii mikazi kipindi hicho napambana life baada ya braza mmoja aliyekuwa ameshika kazi, akishachukua mpunga kwa bosi basi anasema tumfuate mpaka kilabuni huko ndiko anaenda kutupea hela. Ili wamama wa kilabuni wajue yeye ndio bosi.

Kiufupi ni kazi ambayo inachangamoto zake hasa zikikukuta sio mtu wa kujichanganya sana kwa watu.

Ukiona mtu miaka nenda rudi anafanya saidia fundi ameshindwa hata kujiongeza na yeye kuwa fundi basi jua ana matatizo ya kiakili.

Nawaoneaga huruma vijana wanaotoka chuo na kuanza kupiga hii kazi.
 
Niliifanya kwa mda wa miez 5 nikiwa nasubr matokea ya kwenda kidato cha tano katika maandalizi ya daw.a

Aisee tulikuwa tunamimina zege, mara kuchimba chamber ,Mara kuchota zege Mara kubeba tofar siku inaisha umechoka balaaa ,afu hapo ukiwaza safar ya kwenda home unafika sa saba usiku.

Nashukuru ilinisaidia kupata ada ya kulipa kidato cha tano na sita na hela ya matumizi pia nilipata ujuzi sahv angalau unaweza jenga hata choo.
 
Leo nilikua nachanganya zege kipande hiki

20210205_164114.jpg
 
Hahahaha umenikumbusha

Wakati nimetoka kupiga paper tu la form 2 nikiwa naendelea kusubiria matokeo nikaamua nijichanganye kitaa kusaka michuzi

Siku moja tulikua kilingeni na wana tunapeana stori mbili tatu za kupata michongo ya town. Jamaa mmoja akasema juzi kuna mzee flani mtaa wa kati hapo alikua anatafuta msaidizi yeye ni fundi kujenga kama vipi mfukuzie huenda bado hajapata mtu

kweli kama zari yule faza hakuwa na mtu na tukaanza makubaliano ya bei, akaniambia kwa siku malipo ni 5000 mi kimoyoni nikasema fresh tu kibishi hata kama halipi kuliko kukaa bila kazi

kosa kubwa nililolifanya ni kufanya mapatano ya bei sehemu tofauti na eneo la kazi maana ile siku ndo napelekwa site nikaanza kufanya tathmini ya mazingira ya kazi ukilinganisha na kiwango nacho lipwa

kwanza ilikua ni ujenzi unaoanzia mwanzo kabisa kwenye foundation ya msingi, ramani ilionesha nyumba inatoa vyumba vitatu hivi...

changamoto ikaanza, nikaambiwa nikabebe mifuko ya cement ambayo mifuko hiyo iko umbali kama viwanja vitatu vya mpira kutoka eneo la site.

Nikapiga hesabu mifuko inayo hitajika ni mitatu na kila mfuko una Kg 50 kwa umbali huo nikifanikisha kubeba ntakua hoi sana, halafu pia hapo bado hatujaanza kazi rasmi mmmh nikajikuta nimeguna nikasema basi fundi akanisikia akauliza unasemaje? nikasema mi nashauri twende tukabebe wote tufanye team work

yule fundi akachomoa akasema hiyo kazi ni ya msaidizi ye haimuhusu kama umeshindwa kazi sema nimtafute kijana mwingine. Kweli alikua amemaanisha ikanibipi nitoke mdogo mdogo kubeba japo kinyonge

ujenzi wa mkoani ni mgumu kipengele hiki wakazi wa dar hawatanielewa

ilifika wakati sasa wa kuset msingi, hapa nazungumzia msingi ule wa mawe na majabari. Hapa nikawa niko high nimemaind kichizi namskilizia fundi kama ataleta midosho ya mwanzo kua hii ni kazi ya msaidizi aniambie ntasomba peke yangu mijiwe yote.

hapa aliponicheki usoni akajua tu ni habari gani ambazo kwa muda huo hapaswi kuniambia akajiongeza akasema twende tukabilingishe mawe.

changamoto ikawa kwenye utegevu, yeye ni mzee so mzigo wote nikama nilikua naubeba mimi peke yangu. Nikasimama nikamwambia faza tulia kwanza nikuchane haiwezekani mi nasukuma jiwe we unategea halafu kwenye mgao unifanyie undava unishkishe buku 5. Faza akasema hapana shida we fanya kazi utaongezwa 5 ya ziada
 
Nilifanya sana hiyo kazi niliambulia kujua spirit level, biriji nk hapa juzi nilisema ngoja nijikumbushe enzi kikatengeza sehemu ya kuchotea bomba kazege weweee niliumwa kila kiungo na gout zikanzia hapo
 
Back
Top Bottom