Tuliopitia maisha ya "Saidia Fundi" tukutane hapa

Tuliopitia maisha ya "Saidia Fundi" tukutane hapa

Picha linaanza niliambiwa pima ndoo 120 za mchanga jamaa akawasha fegi hapo bado kuchanganya na kuanza kumsogezea,nakumbuka hii siku nilivyopanda kitandani hapo hapo nikasikia jogoo anawika kwamba kumeshakucha siku nyingine inaanza.

Mwamba pole sana hapo nimecheka uliposema ulipolala jogoo akawika manake ukujua umelala lala vp gafla asubuhi hii hapa na kazi bado inaendelea so unatakiwa ujitoe kwa bed uende mishe 🤣🤣🤣[emoji481][emoji481][emoji482][emoji482][emoji482][emoji481][emoji481][emoji481][emoji481][emoji481] waiter tuongezee bapa tupoze machungu na mwamba hapa
 
Nakumbuka kuna jamaa alikuwa anamsaidia fundi ss kuna siku fundi mkuu akawa anaumwa yule saidia akaona hii ndiyo chance sasa ya kupiga hela bila utata utata wala kupunjwa, boss akauliza muliofika vp munaweza kusogeza kazi mbele? Wasaidizi ndiyo! Boss akawapa ukuta wajenge ila kwa sharti ukuta unyooke wakakubali wakapeana kuta za kujenga, saidia mmoja akapiga shoo fresh akamalizw huyu mwingine doooh! Ukuta ulipinda hatari akaishia kuambiwa abomoe daaah! Ila boss alikuwa muungwana akampa kifuta jasho, akaulizwa unafahamu kobilo akasema sijui... pale ndiyo nikajua kuna masaidia wengine wameridhika walipo yaani kujiongeza kwao no big deal... [emoji481][emoji481][emoji481][emoji482][emoji482][emoji481][emoji481][emoji481][emoji481][emoji481][emoji481][emoji481][emoji481]
 
Likizo moj ya advance narudi tu home nakuka jiran kwet wanaset msingi waanz kujenga
Kwakua b mkubwa hana hela ya tution Wala Nini ikabidi aniunganishe na mafundi

Nilipiga kazi mwez mzma
Kimbembe kweny kumimina zege kmmak umaskin mbaya jamani

Licha ya kuaibik kwa madem kitaa maan nyumb ipo barabarani,
Nilikuwa na makovu mwili mzma,
Mikono imechanika n matofari Hadi so poa
 
Ombea usikutane na fundi alievurugwa 😂😂 kuna saidia fundi alikuwa anaitwa "mke wangu" na fundi, yani haya maisha watu wanapitia mengi sana.

mkuu kureport site tu engineer anasema saa 12 asubuhi watu wawe wamefika mazingira ya kazi yaaandaliwe
hapo cement tunatakiwa kuleta eneo la kazi kama mifuko 100 ya kuanzia
mashine ikiwaka haizimi mpaka muda wa chakula cha mchana ikiharibika mnasema alhamdulilah😀😀😀
yani ni lile zege mnamwaga kwa kasi ya ajabu mchaka mchaka ukiwa slow kulikuwa na wana wametoka mjini wanatukana vibaya sana hizi kazi haziendi bila matusi 😀😀
yani kitengo cha afadhali ni kile cha kuweka cement kwenye mashine ukitoka hapo huwezi kupita road watoto wa shule wanakimbia
tulikuwa site moja kubwa mkuu yani mashine inawaka 12;30 inazimwa 6;30 mchana muda wa kula ugali maziwa
baada ya kula watu wanapumzika kidogo kabla ya kurudi tena muda wa kulala ulimi nje kama kibudu cha mbuzi
Mdomo nje kama kibudu Cha mbuzi uongo🤣
 
Saidia fundi Dubai analipwa lakini Tisa Hadi 1.2M bila tatizo.
Maisha Matamu sana
 
Back
Top Bottom