Tuliopitia maisha ya "Saidia Fundi" tukutane hapa

Tuliopitia maisha ya "Saidia Fundi" tukutane hapa

Leo nilikua nachanganya zege kipande hiki

View attachment 1695487
haya mazingira ni unforgetable kwangu

kuna apartment ilikua inasimamishwa na boss mtasha wa pale town. Kama ilivyo kawaida watoto wa mjini hawakosi connection za madili wakanistua na mimi sikufanya kosa nikaibukia

ilikua ni ishu ya umwagaji zege tu iliyojumlisha wafanya kazi zaidi ya 50 na ndio ilikua mara yangu ya kwanza kufanya kazi na group kubwa la watu ambalo ndani yake hadi wamama na mabinti walikuwepo

Asubuhi mtasha akaja site akatangaza dau kua kila mmoja atamlipa 25k, raia wakaonekana kutoridhika mi nikawa nawashangaa kwasababu ile pesa niliiona kubwa kulingana na idadi ya watu ilivyokua niliamini ni kazi itakayo kamilishwa masaa machache tu.

zikaletwa mashine za kuchanganyia zege na mimi nikachukua chepe nikajiunga kwenye sector ya kupakia kwenye vindoo.

sasa hii zege ilikua inaenda kumiminwa kwenye floor ya pili huko juu, kwa hiyo ukatengenezwa utaratibu wa wabebaji kupanga mstari kutoka chini ambako zege inachanganywa hadi floor ya mwisho ambako zege ilikua inamiminwa

haikua rahisi kwa mmoja mmoja kubeba zege na kupanda nayo hadi juu na ndio maana uliwekwa mstari ambao mtu wa kwanza anampasia zege mtu wa pili mpaka inafika eneo inayo hitajika

Kutokana na kazi kuambatana na wanawake hasa wamama ikabidi iwekwe sheria ya kipimo cha ujazo wa zege kua ni chepe mbili tu ili kutowaumiza

baada ya masaa takribani kama saba hivi baada ya kula lunch watu wakiwa wamejipumzisha kusubiria round ya pili nikasema ngoja nipande juu nicheki tumefikia wapi maana nilikua nahesabu idadi ya mifuko 53 tuliyoitumia nikawa nishafanya estimation kua robo tatu ya kazi kivyovyote itakua imekamilika kutokana na u expert niliopata kwenye kumwaga vizege vya renta

Aisee nilipopanda kule juu nilichoka, kwani nilikuta ile foundation imesukwa kwa namna ya kipekee. Nondo zilisukwa za kutosha halafu space ya kuijaza ile zege kutoka juu mpaka chini ilikua inanifika usawa wa paja na mi nishazoea space ya renta kutoka chini ni inch 5 tu leo hii nimekutana na hii shuguli

halafu ukicheki upana wa lile eneo lilikua ni kubwa sana kiasi cha kufanya kazi tulioifanya ionekane kama ni robo kazi huku eneo kubwa likiwa tupu bila zege

Hapa nikawa nawakumbuka wale wadau waliokua wanadai pesa iongezwe nikajisema daah wale miamba walikua na jicho la tatu walifika hii angle ila kutokana na kujifanya mjuaji nikawapinga
 
Nilishuhidia shughuli ya hawa saidia fundi aisee, kesho yake nikaja na plan nyingine site, sikutaka kabisa mali yangu iwe na jasho linalolalamikiwa...ilikuwa hivi namuuliza fundi kazi yako bei gani?namuambia nakuletea saidia fundi na majukumu yake ni haya na haya, hapo hawajuani ni kazi tuu na unyonyaji hamna, kiuhalisia nilikuwa ninawalipa sawa sizidishi hata senti kwa yeyote
 
Picha linaanza niliambiwa pima ndoo 120 za mchanga jamaa akawasha fegi hapo bado kuchanganya na kuanza kumsogezea,nakumbuka hii siku nilivyopanda kitandani hapo hapo nikasikia jogoo anawika kwamba kumeshakucha siku nyingine inaanza.
Daah umefurahisha ila pole sana mkuu, kuwa ulivyopanda kitandani, ukaja sikia jogoo anawika, umefurahisha sanaa daaaah
 
Hii kazi ilinikosakosa siku moja nimeenda kwa wachina kutafuta kibarua fundi akanichagua baada ya msaidizi wake kuchelewa kufika nikaenda changing room anasema nibadilishe nguo niwe kikazi huku anavuta fegi.

Nikawa nawaza Leo naumbuka hapa ghafla akatokea msaidizi wake daah ndiyo wakanipiga chini akasema njoo Kesho nikuangilizie nafasi, sikurudi tena bila fegi na ndumu hii kazi hutoboi.
 
Nimekumbuka mwaka Fulani nilikuwa na washkaji kwenye site moja jengo la serikali kufika pale asubuhi tukamtafuta injinia mwenyew atupe kazi.

Injinia akatuambia wasaidizi wametosha labda niwapatie kazi nyingine ndogo mtaipiga chap chap mchukue chenu akatuonesha eneo lenyewe lilikuwa la kutoa kifusi kweli kuangalia eneo lenyewe kweli tukakadilia masaa matatu tunachukua chetu tulikubaliana elfu 15 watu watatu tuliiona nyingi.

Tulifanya ile kazi zaidi ya masaa matano lakini kazi haimailiziki kifusi kilikuwa kimejishona chini ilibidi tumfuate yule bro atulipe nusu kazi bro anakataa anasema kama vipi hii kazi mtaendelea nayo hadi kesho sisi tukipiga hesabu tunaona tena ni hasara yani turudi kesho kwa kazi ya elfu tano.

masaa yalikuw yanaenda kazi haisogei kwanza yule bro anatuambia mnatoa kifusi cha juu juu tu nataka mwende chini hapo ndo tulichoka kabisa tukakimbia kazi
 
Nakumbuka mwaka 2007 nilifanya kwa wiki moja siku ya j.mosi tukalipwa dah nikasema sikanyagi tena nakubuka nilipwa 24000 fundi 60,000 wakati Mimi ninaonekana kuwa nilifanya kazi kubwa yeye anasimama tu kwenye jukwaa umpelekee tofali umpelekee tope baada ya kz unahakikisha vyombo vinang'aa
 
Nakumbuka mwaka 2007 nilifanya kwa wiki moja siku ya j.mosi tukalipwa dah nikasema sikanyagi tena nakubuka nilipwa 24000 fundi 60,000 wakati Mimi ninaonekana kuwa nilifanya kazi kubwa yeye anasimama tu kwenye jukwaa umpelekee tofali umpelekee tope baada ya kz unahakikisha vyombo vinang'aa
Aisee.hizo kazi ni zakinyonyaji!
 
Mimi ilikua nimemaliza form 4.

Kazi ilikua ni kumwaga zege la chini (kalavati) kubwa sanaa, nilikua mzoefu kidogo kwenye kazi hizo, malipo yalikua kwa siku.

Kosa langu; wenzangu wanalipwa mimi namwambia boss aniwekee nitazichukua zotee kwa wiki.

Sikupata hata 100 kwenye ile kazi.
 
Back
Top Bottom