johnthebaptist
JF-Expert Member
- May 27, 2014
- 97,869
- 171,716
Binafsi nilimaliza kidato cha 4 pale The Highlands mwaka 1984 na tukio ninalolikumbuka ni mwalimu wa Chemistry Mr Kibasa kuja kuwa mbunge wa kwanza wa upinzani Iringa mjini mwaka 1995 akitokea Mwembetogwa sec alikohamia baadae akiwa Head Master. Kadhalika namkumbuka Salim Asas ambaye alikuwa kijana mdogo na sasa ni nguzo ya CCM hapo mkoani. Je wewe uliyewahi kusoma Iringa tupe kwa uchache mambo uliyaweka katika kumbukumbu. Wakati wetu alikuwepo mzee Mbigili aka Damu ya chama aliipenda CCM kupita maelezo. Karibu!