Tuliosoma Shule ya Sekondari Tosamaganga tukutane hapa

Tuliosoma Shule ya Sekondari Tosamaganga tukutane hapa

Katika miaka ya 1989-91 kuna mwanatosa mmoja anaitwa Priscus Mtei, huyu bwana tulipeana majukumu lakini sijafanikiwa kusikia habari zake tena. mwenye habari zake ani PM
 
Sasa angalia archtech hii alafu linganisha na shule za serikali. Au angalia shule za msaada za jica japan zilizojengwa karibu kila ya shule ya msingi hapa dar linganisha na za kwetu aibu tupu.
 
Oh! Tosa weee! Nilikuwepo hapo 1981-1983 (EGM). Umenikumbusha mbali sana. Nakumbuka nilivyotumia akili nyingi sana kukwepa fimbo ya DUDU alipoamua kuwashughulikia Kidato cha sita wote kwa kuwachapa viboko vinne @ yeye peke yake. Nilifaulu kupitia dirisha la jikoni nikarukia upande wa magharibi. Kwa kufanya hivyo nilifaulu kutopigwa kiboko hata kimoja na DUDU mpaka nilipomaliza kidato cha sita.
 
nyumba zimejengwa kwa tamaduni za ulaya, napenda sana kuona hivi..safi sana.
 
tupo pamoja sana napakumbuka idete hasa mapela enzi za Mkangwa aliyekuwa adui na wenye upara aka zungu
 
Dah tosa boys,bonge la shule!
Nakumbuka tulipewa adhabu kusafisha half mile na KHAMSINI afu maji yamekatika,unatoka kusafisha na kidumu cha lita 5 afu hapo hapo anaingia jamaa wa form 6 anaachia mzigo pembeni,inabidi uanze upya,kweli udogo kazi! 2002-2003!
Hv bweni la MANDELA halijaanguka kweli?
 
Hii picha ni Tosa kwa upande gani? Najaribu kukumbuka inagoma!!

kutoka picha ilipopigwa nyuma njia ya kwenda uwanja wa mpira, kushoto ni nyumba ya masista, kulia njia ya kwenda ipamba.
mbele- kupanda ndio tosa. Asante kwa aliye tukumbusha enzi hizo za Dudu.
wakati wa mgomo baada ya FFU kutinga sie wakazi wa mandela enoe salama lilikuwa shamba la mahindi pembeni na nyumba ya dudu
 
Tosa boys sio wapiga gitaa kama wa Pugu na Minaki.

Tosa huwezi kuifaidi kama
~hujaenda shambani na bustanini Idete
~hujatembea kwa mguu toka Tosa hill hadi Junction kwa miguu
~hujaenda kwa masista kununua "bans"
~hujaenda Msiwasi ground
~hujaenda half mile, the most luxurious place ever in the hill
~hujaenda power station hadi Ipamba

Kakuruvi, hebu ongezea ktk list.

-hujaugua taifod na amiba
-hujashiriki mgomo
-hujapewa dawa ya kichwa wakati unaumwa tumbo-Ipamba hiyo
 
Nilikuwa hapo 2000-2002 (PCM). Is impossible to forget Tosa Hills. Machache nayoyakumbuka
-Nilikuwa na uniform za wanafunzu wa Taasisi nikiwa natoroka nikikutana na Mkangwa anajua mi natoka evening class( aka taasisi).
-Nilinusurika kufa kwa taifodi na amiba( mwanafunzi mmja mkazi wa kalenga alipoteza maisha-RIP) kwa kutoroka hospitali Ipamba na kuwa home Kihesa na ndipo mama akanipeleka hospitali binafsi nikapata dawa.
-Kulikuwa na ticha anaitwa Sika alitoka Mkwama akija darasani ni story tu hakufundisha topic hata moja za form 6- Thanks to students from Dar mlituletea notes za huko kwa Mkandawile ndo zikatutoa.
-Ticha wa number Khamsin nae toka Mkwawa was so boring
-Hakukuwa na walimu kwa kipindi hicho- Thank God kwa wazee wa tuition mlitutoa
-Umeme full time watu hawakuwa wakilala pale-utalala vipi wakati walimu hawapo inabidi usiku mjifundishe
Tosa i love you tosa
 
Ungeweka na mabweni ya Iringa Girls, kunawengine walikua wanalala kule
 
Duh wewe ukinitajia jina ntakufahamu, maana mm nilijoin 1995-1997 form five na six EGM namkumbuka sana Mwalimu wangu wa economic na Geography Mr Mwavika na Mr Mgaya. Namkumbuka Mwavika kwa a lot of terminologies akija assembly asubuhi kutoa speeach, very interesting. Halafu namkumbuka mtu mmoja alikuwa anacheza sana mpira Masote Kalembo sijui yuko wapi. Huyo mwalimu wako aliyeamishiwa baraza la mitihani anaitwa Mr Magesa kama sikosei alikuwa akifundisha Physics, nilikuwa nikikutana nae siku za miaka ya 2000-2004 ila nina muda sijamuona hapa Dar sijui yuko wapi siku hizi.

Mr. Magesa kwa sasa yuko Eagles Sekondari Bagamoyo kama Mwalimu Mkuu Msaidi na pia anafundisha Physics
 
Shule alisomaga mwalimu wangu wa physics EMANUEL SANGA, .ali2pa sana story za uko enz hzoo
 
Back
Top Bottom