Tuliosoma St. Kayumba unakumbuka haya?

Think Hard

JF-Expert Member
Joined
Feb 12, 2015
Posts
318
Reaction score
303
Kama umesoma st Kayumba utakuwa una aidia na haya...


1. Unaenda shule umechelewa unakuta mwalim anakamata wachelewaj unaamua urudi nyumbani
2. Unachukua kimbegu cha ubuyu unasugua sakafuni af unamuunguza mwenzio
3. Mkiruhusiwa tu unakimbia unataka uwe wa kwanza kwenye njia yenu y kurudia nyumban
4. MTU akikukera unamfungia shule (mnapigana baada ya kufunga shule)
5. MTU akikunyima kitu chake unamwambia "Ahaa eeh utaona sa nne"
6. Wadada wembamba ndo wanaongoza kwa kusuta wenzao
7. Ukiibiwa daftar jipya unalia kuliko hata uliloandika
8. Unajaza mapeni kwenye mkebe(compass) na mengine hayaandiki
9. Vifaa vingine kwenye mkebe hujawahi hata kuvitumia mfano bikari labda utolee mwiba
10. Hakuna habari nzur kama kuambiwa Leo hamna shule au mwalim hayupo
11. Habari mbaya zaidi n kurud nyumban kutoka shule una njaa af unaambiwa chakula mgeni kaja tumempa
12. Mtoto wa mwalim utamgundua tu kwanzia sweta begi na viatu vyake
13. Usiombee umpige mtoto wa mwalim utataman uache shule
14. Unatengeneza kifutio cha ndala af unatishia eti kinafuta hadi peni
15. Ukaguzi na huna ufagio.. unaomba chelewa kwa watu af unaongeza kijiti katikati
16. Siku ukienda na ufagio wanakagua maji, ukienda na maji wanakagua kuni au mbolea

Dah shule zetu hizi!!

Ipi umeipitia wewe
 
Tehetehe what hell!! Umenirudisha kwenyewe kabsaaa [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Au kutolea funza na kuwatoboa wanaojifanya wababe,mi ilikuwa ukinizingua tu nakimbilia bikari au mawe
 
Dah.... Sisi tuliosoma Wakati wa mjerumani hayakuwepo hayo [emoji41]
 
Ukienda mchafu wanakagua usafi, ukienda msafi hawakagui.

Dah! mleta mada leo umenikumbusha mbali sana.
 
kuwahi shule ulikua mtihani mgumu kuliko necta
Wengi waliokuwa wanawahi ni darasa la kwanza wanapewa namba na wanatoka saa tano sasa mwalim akiita namba mara mbili hakuna aliyetoka mnajua ni darasa la kwanza akiita mara ya tatu mnatoka kama watano hivi halafu mnaambiwa kila mmoja amtaje kiranja aliyempa hiyo Namba mnaishia viboko maana hujui umtaje Nani.
 
Nakumbuka sisi wakati wa mkoloni, shuleni tulikuwa tunafundishwa namna ya kutembea na jinsi ya kuketi, namna ya kusalimia mtu kubwa jinsi ya kumpa mkono na namna ya k uweka miguu kabla hujainama kuonyesha heshima.
Tulifundishwa ukakamavu sana.

Sare zetu zilikuwa ni kaptula za rangi ya kaki na shati la kaki America, viatu na soksi ndefu nyeupe hadi magotini. Tulijifunza matamshi y akiingereza na tuliimba nyimbo sana. Tulifundishwa kusali kwa njia ya nyimbo kila kabla ya kutawanyika.

Barua ya kwenda kwa mzazi kama wewe ni mtoro, au huna sare nzuri, au mzazi anaitwa, ama lolote inapitia kupitia kwenye mabaraza ya mahakama.

Mzazi asiyejua kusoma akipata barua hiyo anaibeba kuitembeza majumbani kutafuta mtu wa kumsomea.

Lakini tulikula chakula, tulikunywa uji, tulikuwa na afya na wasafi sana tena tulikuwa na uelewa wa hali ya juu sana. Mwanafunzi enzi zile anapokwenda middle school, ni sawa na hawa waleo wanaokwenda vyuo vikuu vya kata.

Kweli ni afadhali sana mkoloni mzungu kuliko mkoloni huyu mbabaishaji aliyejitwalia nchi na kuifanya watumwa wake, kwa hadaa ya uhuru.


Dah.... Sisi tuliosoma Wakati wa mjerumani hayakuwepo hayo [emoji41]
 
Hawa walimu wa ajabu shule ya mjini mnatumwa mbolea ati debe moja unakuja na debe tunaingia kwenye jalala la shule tunajaza makaratasi juu tunatandika gazeti halafu unajaziwa mikono miwili mbolea unatandaza ikikaguliwa unaenda mwaga makaratasi kwenye sehemu ya mbolea mwalim akiangalia anakuta jalala tupu karatasi zote zimejaa kwenye mbolea aliacha mwenyewe kuagiza
 
Hahahahaaaaa ....hii ilikua kali..
 
Hahahahaaaaaa....ni kweli kabisa...utafikiri mkimbizi kabisa anaekimbia nchi yake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…