Tuliotembea umbali mrefu kwa miguu kwa sababu yoyote ile tukutane hapa

Hivi unazijua vizuri KM 100? Hafu uzitembee siku 1 hii chai

Kilometa 100 unatembea vzr tu ...nilishafanya field huko mufindi sasa kwakua kulikua chaka sehem ambayo ni center ni kilomita 6 ila kutokana na kuwa board ilikua kila baada ya siku 2 lazima twende hapo center kula gambe enzi hzo..so ilikua kama kil 12 kwenda na kurudi so niki estimate ule mwendo naona kil 100 zinawezekana kutembea kwa siku moja ukiamka kumi usiku hadi jioni unatoboa
 
Nisbawah tembea kwa mguu mara nyingi sana kutoka posta (IFM) mpk gheto Mtoni kwa Aziz Ally kwenda na kurudi kwa kukosa nauli mia8 tu.. Aisee yale maisha siji kusahau..
 
Niliwahi tembea nmemaliza chuo nkatoa bahasha za application zangukibao kama 20 hv nkaanzia tabata relini kuanza kutembea na kusambaza hzo applctn kwny kila kiwanda nilichokuwa nakiona nilitembea mpka airport viwanda vyote hvyo hakuna ambacho sikuingia... cha ajabu sikuwahi kuitwa hata interview tuu mpka leo hii
 
Ama kweli ulitembea yaani 2 miles ndio umetembea?
Nilitembea kwa miguu siku England waliposhinda Rugby World Cup. Barabara zilifungwa nilikuwa ninarudi nyumbani nilitembea mbali sana. Kutoka Holborn mpaka Elephant and Castle.
 
Mlandizi mpka madafu then unaingia ndani mpka zogowale

Mnazi mmoja mpka mombsa

Ilala sokoni mpka mombasa(miaka 9)

Root mnazi mmoja buguruni zikuwa karbia kila siku

Tulikuwa tunaitwa team cha mguu mbali ni mwiko kuwa na nauli unabakiza pesa ya kandoro tu..................
 
Nilipiga route match na cross country si chini ya km 800 enzi za jeshi kunoga jkt
 
Nilipomaliza Form 6 Songea Boys 2010 nilitembea Toka Songea Hadi Iringa kwa Miguu kwakua Mzee hakunitumia Nauli.

Njiani nilipata ila lift za Baiskeli, Pikipiki, Gari binafsi na jamaa mmoja wa Costa anasema alikua kila siku ananiona njiani akaamua kunipa lift hadi Njombe na pia nikadandia roli la viazi kutoka njombe to Mafinga.

Nilijifunza mengi sana njiani. Mengi sana.

Safari nzima ilichukua siku 8 niliondoka Songea Boys saa 11 Asubuhi siku ya Nane nikafika Iringa home saa 5 Asubuhi.
 
umbali uliotembea kwa miguu ukajiwekea rekodi yako. Inaweza kuwa 1KM.
Kuna jamaa walitembeakutoka urusi hadi India kwa Miguu km zaidi ya 2000. Ipo movie yao based on true story

Naipata mzee. Movie inaitwa The Wayback based of True Story ya kitabu cha The Long Walk.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…