Tuliotembea umbali mrefu kwa miguu kwa sababu yoyote ile tukutane hapa

Tuliotembea umbali mrefu kwa miguu kwa sababu yoyote ile tukutane hapa

Ulipofika mzee alichukuliaje?
By the way, nimetembea toka
Muyama to Kasulu
Muyama to Munanila

Nimeendesha baiskel kwa masaa 12, hakuna siku niliyochoka maishani kama hii.

Mzee alilia sana. Nikajisikia vibaya sana. Nikamwambia sijatembea sana nilipewa lift. Atleast akapoa.

Sio kosa lake hakua na hela. Mama mdogo alikua amevuruga nyumba ata kula tu tatizo home.
 
Nilitoka Ifakara mpk Liwale,safar ya siku 11 kwa mguu,kupitia Mahenge,Ruaha,Mwaya,Mbuga,ketaketa,nna tukazama maporin mpk liwale,.. Yote tunatafuta utajiri ambao tulishimdwa masharti.. Ha ha ha Muacheni Mungu akupe unachostahili kwa wakat wako,kuliko kutafuta kwa shortcut...
 
Maisha haya acha yaitwe maisha. Nimetembea mbezi ya kimara to mlandizi siku mbili. aise hiki kisanga kilichonifanya nitembee umbali huo, ipo siku nitakiletea thread kabsa maana ni story ndefu.
At least wewe nakuamini kuwa mbezi to Mlandizi siku mbili.Ila hawa wanaosema km 100 siku moja siwaamini
 
Niliwahi tembea toka kariakoo Hadi ubungo enzi za shule .

Sababu nilikula nauli hasa baada ya njaa kunishika Sana nikiwa shule
Ubungo kariakoo ni distance fupi hata ukiwa na nauli unatembea tu.Sema ukiwa umekula hela ndo panaonekana parefu balaaaa
 
Itakuwa pasi za mjerumani na hela za mkoloni [emoji23]
Nilitoka Ifakara mpk Liwale,safar ya siku 11 kwa mguu,kupitia Mahenge,Ruaha,Mwaya,Mbuga,ketaketa,nna tukazama maporin mpk liwale,.. Yote tunatafuta utajiri ambao tulishimdwa masharti.. Ha ha ha Muacheni Mungu akupe unachostahili kwa wakat wako,kuliko kutafuta kwa shortcut...
 
Wakati wa Elnino 1998 nilitembea 50 kilometre na mkungu wa ndizi kichwani kutoka Ikanga Mdabulo hadi Mtwango Mufindi kwa jinsi kulivyokuwa na njaa wakati ule ilikuwa ni kama nimebeba kilo moja ya numbu na naenda mita chache tu!!! Usiombee njaa
 
Tuliokulia vijijini kutembea umbali mrefu wala siyo story.

Moja kufuata huduma za kijamii kama hospital, maduka etc

Mbili,kwenda kusaga mahindi vijiji jirani vyenye machine ya diesel.

Kwenda minadani kuuza mazao kilometa kadhaa ili kupata kipata cha familia
Jumamosi naenda kufuata miwa,mihogo au ndizi bush huko mashambani,Jumapili naenda kuuza kijiji cha mbali kidogo angalau kwenye ka mji kadogo.Jioni narudi nyumbani,Jumatatu shule.Lakini sio haba akili zilikwepo.Ila siku watoto wetu muda wote wanawekewa mazingira mazuri ya kusoma lkn mwisho wa siku mtoto anashindwa kufaulu dah maisha haya
 
Buguruni Posta Posta Kinondoni... sitamsahau Lowasa afu akatutosa
Lowassa alinitembeza Jangwani to Ubungo Kibo,halafu siku nyingine Mbezi mwisho to Ubungo Kibo,Ila kutoka Uwanja wa Taifa mpaka Ubungo ni mara nyingi tu
 
Mzee alilia sana. Nikajisikia vibaya sana. Nikamwambia sijatembea sana nilipewa lift. Atleast akapoa.

Sio kosa lake hakua na hela. Mama mdogo alikua amevuruga nyumba ata kula tu tatizo home.
Pole sana mkuu, lakini naamini hilo lilikua somo kubwa maishani
 
mkuu kijijini umbali kwa kutoka Gomzi hadi Tegeta kupitia mwenge, unakuwa umefuta vijiji vya kutosha.

nimekuja kugundua dsm unaweza kutembea umbali ambao ukiupeleka kijijini utaonekana shujaa
We jamaaa unajidanganya sana,kijijini pasikie tu,Kuna sehemu Gombs to posta ni Kijiji kimoja
 
Jumamosi naenda kufuata miwa,mihogo au ndizi bush huko mashambani,Jumapili naenda kuuza kijiji cha mbali kidogo angalau kwenye ka mji kadogo.Jioni narudi nyumbani,Jumatatu shule.Lakini sio haba akili zilikwepo.Ila siku watoto wetu muda wote wanawekewa mazingira mazuri ya kusoma lkn mwisho wa siku mtoto anashindwa kufaulu dah maisha haya
Yaani ni zaidi ya kuwa jeshini maisha tuliyoyapitia,watoto wa siku hizi daah unatengeneza kila kitu ila bado anakuangusha
 
Jumamosi naenda kufuata miwa,mihogo au ndizi bush huko mashambani,Jumapili naenda kuuza kijiji cha mbali kidogo angalau kwenye ka mji kadogo.Jioni narudi nyumbani,Jumatatu shule.Lakini sio haba akili zilikwepo.Ila siku watoto wetu muda wote wanawekewa mazingira mazuri ya kusoma lkn mwisho wa siku mtoto anashindwa kufaulu dah maisha haya
Kadili unavymrahisishia mtu kazi ndo anazidi kuwa mvivu.
 
Kilometa 100 unatembea vzr tu ...nilishafanya field huko mufindi sasa kwakua kulikua chaka sehem ambayo ni center ni kilomita 6 ila kutokana na kuwa board ilikua kila baada ya siku 2 lazima twende hapo center kula gambe enzi hzo..so ilikua kama kil 12 kwenda na kurudi so niki estimate ule mwendo naona kil 100 zinawezekana kutembea kwa siku moja ukiamka kumi usiku hadi jioni unatoboa
Watu wanaofanya marathon huwa wanaenda km 10 unaona katumia zaidi ya saa moja je kutembea unafikiri km 10 utatumia muda gani? Kikawaida 5km ni one hour.Hivyo ili umalize km 100 lazima utumie at least 20hrs.Kumbuka muda unavyozidi kwenda uchovu unaongezeka na mwendo unapungua.Hivyo kutembea km 100 kwa siku ni almost uongo
 
  • Thanks
Reactions: rr4
Back
Top Bottom