Ni siku tofauti.
Ya kwanza nilikwenda kuomba kibarua pale tazara kiwanda cha Panasonic cha betri. Nikakosa kibarua na nauli sina. Ikabidi nirudi kwa mguu kutoka tazara mpaka manzese.
Ya pili nilitoka manzese kwenda kwa ndugu zangu kimara suka.kuwatembelea nilitoka saa 12 asubuh.mpaka saa sita nipo kimara suka. Kurudi wakanipa 5,00.ya nauli.
Sikuwaambia nilienda vipi.
Ya tatu.katika kutafuta vibarua nilikwenda pale ubungo stendi ya shamba. Pale kuna vibarua wengi na mafundi uwa wanakaa wanasubiri magari ya kuwapeleka masaiti.
Kuna tipa likaja watu Waka panda na mimi nikadandia sijui linakwenda wapi . na wale watu.
Nimekaa kwenye gari naona tunapita vituo tu.
Kibo,baruti,Kimara mwisho,stop over ,tumbo temboni. Mara mbezi MWISHO.na bado linaendelea tu.nikasema ohooo.naenda wapi huku?
Nikabidi nimuulize jamaa. Akasema wanaenda kwembe kuna shule inajengwa na kazi za vibarua zimeisha.
Basi nilienda mpaka kwembe.
Shughuli ilikuwa kurudi.acha kabisa.
Ni lite Nilitembea kwa miguu kutoka kwembe mpaka kimara suka kwa wale ndugu zangu. Nikazuga nimekwenda kuwatembelea kumbe nilikuwa sina nauli ya kurudi manzese.
Wakanipa tena 5,00.
Nilivyorudi nililala kama nimekufa
mjingamimi,
mkuu hizi ni kama nyingi sana, Ungekuwa kijijini ungeelewa vizuri.
Wabongo tunapitia mengi mkuu