matunduizi
JF-Expert Member
- Aug 20, 2018
- 7,968
- 19,368
- Thread starter
-
- #121
utakuwa ulikwepa kupitia bima ukapita shortcut ya kutokea campLeo nimetembea kutoka Kigogo kituo cha Polisi (First In) mpaka Tabata relini nikanywa Juisi, nikaendelea kutembea hadi Tabata Mawenzi.
Msalimie mremaNakumbuka nilitembea toka Kirua vunjo uparo kwa babu mzaa baba mpaka Kiraracha,Komalagwe nilipofika pale marangu mtoni nikatamani kurudi
Hata sisi babu alikuwa anatutembeza kama 50km au zaidi kwenda kwa ndugu zake huku tumebeba pombe yake. Tulikuwa wadogo ila tulivumimila saana sababu babu alikuwa na stori nyingi njiani. nakumbuka nilikuwa na miaka 9 nilipoanza tembea na babu.Hapo walikuonea hakika.
hongera yake hayati Baba wa Taifa,Nyerere alitembea. Wanzie walifika na malengelenge wengine hawakumaliza. Yakwangu ilikuwa kukimbia jeshi miaka ile ya 80 jeshi likikuwa hatari. Imagine huna pesa, hujui unaenda wapi lakini unatoroka ili mradi kukimbia mateso ya jeshi. Tuliishia mikononi ya maafande. Jela ya jeshi mwezi we acha tu!!!
utakuwa ulikwepa kupitia bima ukapita shortcut ya kutokea camp
mkuu igoma cocacola hadi roundabout pale town ni 10Km nadhani. utakuwa vzr, kwenda na kurudi nikiwa primary route za kirumba airport zilikuwa kawaida sana.Mi kutembea toka msasani Hadi posts,go and return sio ishu,ama toka igoma Hadi mz mjini,go and return,sijui ni km ngapi,
Kiufupi Kama mi natembea sana hata Kama Niko full loaded mfukoni
haha ha,mkuu igoma cocacola hadi roundabout pale town ni 10Km nadhani. utakuwa vzr, kwenda na kurudi nikiwa primary route za kirumba airport zilikuwa kawaida sana.
joto vipi mkuu, maana posta napo ukifika unajasho, ukikutana na Bashite anaweza kukunasa makofi
Mie safari yangu na baba mdogo pamoja na bro ilikuwa mbaya ndio maana naikumbuka tena Kuna wakati nakasirika kuwa walinionea,kwanza nilikuwa mdogo halafu umbali mrefu sehemu nyingine tunapita pori na mara zote walikuwa wananiacha nyuma hata sioni mtu mbele,wakifika sehemu wananisubiri,mie nikifika wanaondoka bila kunipa muda wa kupumzika.Badaye nikakata tamaa ya safari sikutaka tena kuwa nao nikakaa chini nikalala.Mtu unatembea huku machozi yanakulengalengaHata sisi babu alikuwa anatutembeza kama 50km au zaidi kwenda kwa ndugu zake huku tumebeba pombe yake. Tulikuwa wadogo ila tulivumimila saana sababu babu alikuwa na stori nyingi njiani. nakumbuka nilikuwa na miaka 9 nilipoanza tembea na babu.
Akishindwa kukubeba, kesho kutwa Zamu yangu kutembea naweKaribu, ujiandae kunibeba.
Akishindwa kukubeba, kesho kutwa Zamu yangu kutembea nawe
Duuuh, mkuu ulikomaa Sanaa toka Mazimbu, IPO IPO, Modeko,.chamwino, kasanga utoboe Hadi mzumbe,mlali Hadi kufika Mgeta daaah heshima kwakoMkuu unaambiwa nilitoka mazimbu ipo ipo saa kumi na mbili, nikazama tumbaku, then kasanga, nikapita kwenye hayo mashamba kuelekea mzinga, nikaibukia mzumbe hivyo hivyo nikanyoosha mashambani nikaja kuibukia barabara ya mlali, nikanyoosha panda milima shuka mabonde kufika saa tatu usiku Niko mgeta police station. Kurudi hivyo hivyo nilikuja kusikia uchovu wa kufa mtu siku tatu mbele.
Huezi amini nilikuwa napiga mazoezi tu na mpango wangu ulikuwa kuishia mzumbe ila utamu wa mashamba na mifugo niliyokuwa napishana nayo plus vilima na mabonde nikajikuta nishafika huko kote. Nashukuru sikuibukia mikumi ningeliwa na tembo au Simba mazima.
Ubungo kariakoo ni distance fupi hata ukiwa na nauli unatembea tu.Sema ukiwa umekula hela ndo panaonekana parefu balaaaa
Nyerere alitembea toka Butiama mpaka Mwanza. Mimi nilitembea toka Bulombola mpaka Kigoma nikijongo majeshi nikaishia kukamatwa na kuswekwa lupango ya jeshi kwa mwezi. That was during Kagera war hata nyoka karibu atung'ate na mtoro mwenzangu.
Wote yalitukuta. Mimi nilitembezwa na baba mdogo wakati nipo period, nilidondoka tena kwenye daraja la miti wakadhani najifanya. I wished to die. Ndo nikapewa kapombe kidogo kuleta nguvu kumbe ndo wameharibu. I will never forget lakini tulikuwa na maisha ya raha. Hakuna wa kusema huyu ni baba mdogo wala nani ikifika safari twende tena huko ni kwenye makoro yaani kwa ndugu wa babu zetu. Sasa hivi hivyo vitu vimekufa na tumeua undugu.Mie safari yangu na baba mdogo pamoja na bro ilikuwa mbaya ndio maana naikumbuka tena Kuna wakati nakasirika kuwa walinionea,kwanza nilikuwa mdogo halafu umbali mrefu sehemu nyingine tunapita pori na mara zote walikuwa wananiacha nyuma hata sioni mtu mbele,wakifika sehemu wananisubiri,mie nikifika wanaondoka bila kunipa muda wa kupumzika.Badaye nikakata tamaa ya safari sikutaka tena kuwa nao nikakaa chini nikalala.Mtu unatembea huku machozi yanakulengalenga
Ha ha Si kweli...Ka nchi ka zanzibar kidogo nikamalize kote kwa mguu..
Sio kwa siku moja.. nilikua natembea umbali mkubwaa.. nilikua napenda kuona mazingira yake.. ukiwa kwenye vilima..Ha ha Si kweli...
mjingamimi,
mkuu hizi ni kama nyingi sana, Ungekuwa kijijini ungeelewa vizuri.
Wabongo tunapitia mengi mkuu