Tuliothubutu kulima mahindi vuli hii tukutane hapa

Tuliothubutu kulima mahindi vuli hii tukutane hapa

MLUGURU

JF-Expert Member
Joined
Mar 30, 2012
Posts
2,929
Reaction score
3,710
Kwa wale wabishi wenzangu wa kilimo cha kutegemea mvua,waliothubutu kuweka mbegu za mahindi tukutane hapa ili tupeane updates mbali mbali.

Mimi nilipanda tarehe za mwishoni mwa mwezi october na sasa nalima palizi ya kwanza na mahindi yanaendelea vyema kabisa sijajua huko mbeleni.

Shamba ni hekali 2 na nilipanda zigzag
 
Mkuu wewe ni jasiri, mimi nilivyoona kwenye maeneo ya Kilindi mpaka mwishoni mwa mwezi October vuli haijanyesha niliahirisha aise. Ila huenda Mungu akaweka mkono wake ukavuka salama
 
Mimi mwezi ujao namwaga mbegu sijalima kwaajila ya biashara, nimekod ekar kidogo ata nikifeli sintakosa Cha kulisha familia pia nafanya majaribio maana sijawahi Lima kwenye huu mkoa
 
Mimi mwezi ujao namwaga mbegu sijalima kwaajila ya biashara, nimekod ekar kidogo ata nikifeli sintakosa Cha kulisha familia pia nafanya majaribio maana sijawahi Lima kwenye huu mkoa
Mkuu Mkoa gani na huwa masika yanaanza lini...maana usitegemee sana vuli..
 
Nilipanda tarehe 2 October ilinyesha Mvua moja tu nikaitumia kupanda nilinunua mbegu ya mahindi ya DK Nilipanda mifuko mitatu hayakuota vizuri kutokana na jua ila Mvua iliporudi nikanunua mfuko mmoja kurudishia kwa Sasa napalilia palizi ya pili na mahindi yako vizuri sana, niko muheza Tanga.
 
Mkuu wewe ni jasiri, mimi nilivyoona kwenye maeneo ya Kilindi mpaka mwishoni mwa mwezi October vuli haijanyesha niliahirisha aise. Ila huenda Mungu akaweka mkono wake ukavuka salama
Amiin mkuu,ilitokea tu shamba nililiandaa mapema kabla ya october,sasa mvua nyingi zikachelewa kunyesha,hivyo zilivyoanza tu nikaona bora nipande kuliko kula hasara ya kutopanda kitu kabisa.

Vipi mpaka sasa huko mvua bado mkuu.
 
Mimi mwezi ujao namwaga mbegu sijalima kwaajila ya biashara, nimekod ekar kidogo ata nikifeli sintakosa Cha kulisha familia pia nafanya majaribio maana sijawahi Lima kwenye huu mkoa
Mwezi ujao kwa mvua hizi za vuli mkuu au??
 
Nilipanda tarehe 2 October ilinyesha Mvua moja tu nikaitumia kupanda nilinunua mbegu ya mahindi ya DK Nilipanda mifuko mitatu hayakuota vizuri kutokana na jua ila Mvua iliporudi nikanunua mfuko mmoja kurudishia kwa Sasa napalilia palizi ya pili na mahindi yako vizuri sana, niko muheza Tanga
Mkuu hongera sana,mliopanda awamu ile ya kwanza hakika mna uhakika kiasi fulani cha kuvuna mahindi ya vuli,ila wengi tumepanda zile mvua za mwanzoni mwa october.

Na mimi nimelimia muheza pia.
 
Mvua saivi zimekuwa za makisio sana unaweza ukalima mvua ikanyesha kupitiliza kma mwakajana mhindi yanaoza au isinyeshe nyingi yan shida tupu yan tungekuwa na watabili wa hali ya hewa yakinifu tungekuwa na uthubutu mkubwa wa kulima.

Cha kusha uri kma unalima kwa ajili ya biashara bora uwe na eneo ambalo Lina kinzana na MTO au kisima in case of anything.
 
Jamani mimi nimepanda yameota vinzur Sana ivi naweza nikaweka mbolea ya kuchomekea bira kupalilia
 
Haya hapa.
IMG_20201207_095116_3.jpg
 
Jamani mimi nimepanda yameota vinzur Sana ivi naweza nikaweka mbolea ya kuchomekea bira kupalilia
Hapana. Lazima upalilie kwanza ndo uweke mbolea. Mahindi yako tangu yatoke yana siku ngapi? Kama ni zaidi ya wiki 2, weka mbolea ya kukuzia baada tu ya kupalilia. Usipopalilia jua utanenepesha na magugu ambayo yatadumaza hayo mahindi

Sent from my SM-A217F using JamiiForums mobile app
 
Mpaka sasa hali ni hiko hivi,hapa nasubili kudra za mwenyezi Mungu walau lipatikane wingu moja mahindi yabebe nipate hata ya kuchoma.

Ubora wa shamba,mvua za kutosha kipindi cha kupanda,palizi mbili za haraka haraka nashukuru mahindi yamefikia hapo.

Back
Top Bottom