Tuliowahi kuagizwa Mzazi shuleni tukaleta wazazi feki tukutane hapa.

Bismack

JF-Expert Member
Joined
Mar 12, 2018
Posts
387
Reaction score
495
Nakumbuka niliagizwa mzazi na mkuu wa shule baada ya kufanya kosa fulani, nikatafakali nikaona kama nikimpeleka babangu tukifika tu lazima yeye ndo atakua wa kwanza kunipiga mana baba yangu kwa kupenda sifa za kugawa kipigo nikaona bora nimpange jamaa mmoja nashukulu lilisovika vizur.
 
Nakumbuka kumpeleka fundi saa kufika shule akasahau jina langu... Dah... Nilikiona cha moto
 
Haha, kuna mwingine nlimpeleka sasa hata kutamka jina langu ikawa shida.

- Mwanangu cowiimon soma acha ukorofi-

Mama wa watu alikua analilia tu hadi nikasamehewa, haha kweli bongo movie ilikuwepo toka zaman yaan sijui yale machozi alikua anatoa wapi. But alinisaidia kwa malipo ya elf5.
 
Duuh mchezo huo alikuwa nao headmaster wa popatlal Tanga marehemu Chaudry basi kuna siku aliletewa muhudumu wa bombo hospital na jamaa yetu mmoja wakati baba yake alikuwa headteacher mkwakwani primary ilikuwa kashehe kwenye kuelewana lugha haipandi kwa mhudumu.
 
Haha aisee niliongopa kua baba hayupo yupo nje ya nchi nikamtafta msela flani nikampanga awe km ni brother wangu yaani jamaa ni mlevi wala hatufanani hata kidg hatar tupu

Ila teacher akaelewa
 
Kuna jamaa mmoja yeye alimpeleka shule muhudumu wa bar awe kama mama yake mdogo baada ya kutakiwa kumuita mzazi. Huyo mwanamke mwenyewe alikua kajichubua balaa! Walimu wakashtukia issue kisha wakawatenganisha vyumba na kuanza kuwauliza maswali kuhusu watu wa familia yao. Ilipobainika wamedanganya yule Bar Maid akapewa options mbili, ama apelekwe polisi au acharazwe bakora, hahahahaaa mama wa watu ikabidi achague kukinga matako akalambwa mboko sita safi kabisa kisha akaachiwa aende zake huku analia kwa sauti
 
Nakumbuka niliagizwa mzazi na mkuu wa shule baada ya kufanya kosa fulani, nikatafakali nikaona kama nikimpeleka babangu tukifika tu lazima yeye ndo atakua wa kwanza kunipiga mana baba yangu kwa kupenda sifa za kugawa kipigo nikaona bora nimpange jamaa mmoja nashukulu lilisovika vizur.

Mimi nilimpeleka Mtu ' Feki ' na nakumbuka tulikubaliana vizuri tu, nikamtoa hadi na ' mtonyo ' kiaina na kujiaminisha kuwa nimemuweza Headmistress Wetu na nikawa natamba kabisa ( ila siyo kama Aslay katika Wimbo wake ) lakini cha kushangaza nilipoingia nae tu Yule Mtu ' Feki ' katika eneo la Shule alinichenjia pale pale na badala sasa ya kuwa ' Mtetezi ' wangu kama tulivyokubaliana akageuka kuwa ' Pilato ' wangu na sijawahi kupigwa Viboko vya Kikatili / Kishalubela kama ambavyo nilipigwa Siku ile na hadi leo hii na Utu uzima wangu huu zile mboko / bakora / fimbo kuna muda huwa nazisikia maumivu yake na ' sometimes ' huwa naziota pia. Tokea Siku hiyo nilishika adabu zangu zote!
 
Mkuu toka nikufahamu leo ndio nimeona kumbe kuna wakati uliwahi kua mnyonge na mtu akakuonea japo kwa kupanga nyie wenyewe, hahahaa
 
Mimi nilimpeleka Mtu ' Feki ' na nakumbuka tulikubaliana vizuri tu, nikamtoa hadi na ' mtonyo ' kiaina na kujiaminisha kuwa nimemuweza Headmistress Wetu na nikawa natamba kabisa ( ila siyo kama Aslay katika Wimbo wake ) lakini cha kushangaza nilipoingia nae tu Yule Mtu ' Feki ' katika eneo la Shule alinichenjia pale pale na badala sasa ya kuwa ' Mtetezi ' wangu kama tulivyokubaliana akageuka kuwa ' Pilato ' wangu na sijawahi kupigwa Viboko vya Kikatili / Kishalubela kama ambavyo nilipigwa Siku ile na hadi leo hii na Utu uzima wangu huu zile mboko / bakora / fimbo kuna muda huwa nazisikia maumivu yake na ' sometimes ' huwa naziota pia. Tokea Siku hiyo nilishika adabu zangu zote!
hahahaaa hera yako alikuludishia ?
 
hahahaaa hera yako alikuludishia ?

Baada ya kunipa kile ' Kichapo ' akatoka nje ya Geti la Shule akaenda zake kujiburudisha nayo kwa kununua Chips, Coca Cola baridi na chenji iliyobaki alimuhonga Mwanamke pale pale ' Baa ' akaenda ' Kumbandulia ' nayo. Iliniuma sana Mkuu na siku ile ile Mimi na Yeye Urafiki uliisha na hadi hivi leo tumebaki kuwa kama Israeli na Palestina.
 
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] umenifanya niongeze cku zangu za kuishi leo.
 
umenikumbusha mzee kipindi nimeamishiwa shule ya wilaya ya hai kufika tu nikaamasisha mgomo si nikatumwa nikalete mzazi basi nikapeleka mwendesha bodaboda sema ngoma iliisha sema Kwa mbine sana
 
Baada ya kunipa kile ' Kichapo ' akatoka nje ya Geti la Shule akaenda zake kujiburudisha nayo kwa kununua Chips, Coca Cola baridi na chenji iliyobaki alimuhonga Mwanamke pale pale ' Baa ' akaenda ' Kumbandulia ' nayo. Iliniuma sana Mkuu na siku ile ile Mimi na Yeye Urafiki uliisha na hadi hivi leo tumebaki kuwa kama Israeli na Palestina.
Jamani [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Kuna dogo juzi kaagizwa mzazi akaleta mvuta bangi mwenzie.

Tukamstukia, tukamwambia inabidi amuadhibu mdogo wake. Jamaa akamshushia kipigo dogo hadi dogo akajikuta anaropoka kuwa huyo sio ndugu yake ni amemuokota tu. Tulicheka sana.
 
Back
Top Bottom