Mimi nilimpeleka Mtu ' Feki ' na nakumbuka tulikubaliana vizuri tu, nikamtoa hadi na ' mtonyo ' kiaina na kujiaminisha kuwa nimemuweza Headmistress Wetu na nikawa natamba kabisa ( ila siyo kama Aslay katika Wimbo wake ) lakini cha kushangaza nilipoingia nae tu Yule Mtu ' Feki ' katika eneo la Shule alinichenjia pale pale na badala sasa ya kuwa ' Mtetezi ' wangu kama tulivyokubaliana akageuka kuwa ' Pilato ' wangu na sijawahi kupigwa Viboko vya Kikatili / Kishalubela kama ambavyo nilipigwa Siku ile na hadi leo hii na Utu uzima wangu huu zile mboko / bakora / fimbo kuna muda huwa nazisikia maumivu yake na ' sometimes ' huwa naziota pia. Tokea Siku hiyo nilishika adabu zangu zote!