Tuliowahi kuathirika na washindani wapya katika biashara tukutane hapa, ulipitia wakati gani, ulijiongeza, ulihama au ulifunga biashara?

Tuliowahi kuathirika na washindani wapya katika biashara tukutane hapa, ulipitia wakati gani, ulijiongeza, ulihama au ulifunga biashara?

sky soldier

JF-Expert Member
Joined
Mar 30, 2020
Posts
5,407
Reaction score
19,264
Inaweza kuwa biashara yako inaenda vizuri, yaani kila ukifunga hesabu kimoyo moyo unasema “mambo si ndio haya !” Mara paaaap! Anatokea mshindani mpya aidha
  • anafungua pembeni/karibu yako biashara kama yako, copy paste
  • mwenye bei za chini,
  • bidhaa zake zina ubora zaidi,
  • anafanya free delivery,
  • anauza kwa mkopo
  • Ana connection
Wataeja haoooo!! Taratibu au ghafla unaona mauzo yamepungua sana, wateja wanakauka, siku nzima ni kubadilisha pozi la miguu tu ofisini na kwenda kupiga story kwa jirani mpaka jioni.

Hapa ndipo watu huingia tamaa ya kuanza kwenda kwa waganga kutafuta dawa za mvuto wa biashara, kumuangamiza mshindani, n.k. ambapo wengi wanaishia kupigwa tu
 
Kwani wale wanaofungua pembeni/karibu yako biashara ileile kama yako, bei na huduma mnafanana,n.k hawawezi kukuangusha?
Wazee wa kucopy na ku paste, wakiona umekaa miezi 6 hivi wanapima eneo kama lina wateja kupitia wewe uliechukua risk, wakiona wapo wanakuja kukuiga mgawane faida, ubinadamu kazi
 
Unaweza kuwa ni mtakatifu kabisa, ila kwa hili jambo, ukaanza kuwaza kuroga mtu
Hebu fikiri tu umekomaa mwaka mzima, faida ulianza kupata baada ya miezi mitatu ya hasara, umeanza ku jifuta jasho kwa faida kufidia hasara na kurudisha mtaji, ghafla kuna jamaa anafungua biashara kama yako vile vile pembeni yako, alafu yeye ndio wateja wanaanza kwenda kwake zaidi, aiseee!

Hapa ni kama umempiga roba mtu anapigania uhai wake, anaweza kukufanya kitu hukuwahi kumdhania.
 
Hii kitu isikie tu aise
Mtu anaona wewe unapiga Sana hela anasema aha kumbe ile biashara inalipa naye anaamua kuianzisha lakini mara nyingi watu wa aina hii huangukia pua maana yake yeye amefungua kwa kuiga au kulenga kukuangusha wewe mwisho siku mambo yanamshinda anafunga
 
Hasa walimu, watumishi wa halmashauri, wafanya kazi wa benki, n.k.

Hudani wakikopa na kuiga biashara ndio basi, wengi huangukia pua,

Moja biashara ni maisha yake, mwengine ni jaribio,
 
Hii kitu ni mbaya sana usipokua mvumilivu unafunga biashara. Nina ndgu yangu alifunga biashara yake kwasababu kama hizo.

Yeye alikua anauza duka la vinywaji kwa jumla na rejareja. Mwenye depo kubwa mtaa huo walikua wawili tu.
Wengine walikua bado wanajitafutatafuta. Kapiga kazi kama mwaka hivi akaja jamaa nae kafungua depo tena vitu vyake kapunguza bei mno.
Hii strategy ya kupunguza bei sometimes ni mbaya sana kuingia nayo sokoni, jamaa vitu vilikua bei kitonga, kama wewe unauza 1500 basi yeye ni 1300.

Akasababisha mpaka ndgu yangu akafunga duka, ila na yeye kipindi cha hivi karibuni anapumulia mashine maana mzigo hana. Vitu vingi hana nadhani ile mbinu ilimkata sana mtaji maana unachukua bidhaa nyingi ukitegemea faida kiduchu mno ili uvune wateja, matokeo yake ni kweli unavuna wateja ila unaendesha biashara kwa hasara kwa muda mrefu.
 
Ndugu yako alikosea kufunga, mi nilipambana Hadi mwisho, alinikuta, akashusha Bei akauzaaaa, now kafulia Sababu alikuwa anauza kama kunikomoa yeye hapati faida
 
Ndugu yako alikosea kufunga, mi nilipambana Hadi mwisho, alinikuta, akashusha Bei akauzaaaa, now kafulia Sababu alikuwa anauza kama kunikomoa yeye hapati faida
Yes alikosea hilo biashara ni kupanda na kushuka, hao watu ni kupambana nao tu ye mwenyewe atasanda.
 
Nilitegemea mtoa mada utaonyesha mfano wa biashara yako binafsi kumbe unataka watu watoe experiences zao? Sio mbaya
 
Ndugu yako alikosea kufunga, mi nilipambana Hadi mwisho, alinikuta, akashusha Bei akauzaaaa, now kafulia Sababu alikuwa anauza kama kunikomoa yeye hapati faida
Tatizo Wengine Hawana Mtaji Wa kuweza Kukaza Kipindi kirefu hasa pale Hasala inapotokea !!!!
Inaonekana Wewe ulikuwa na Mtaji ?
 
Tatizo Wengine Hawana Mtaji Wa kuweza Kukaza Kipindi kirefu hasa pale Hasala inapotokea !!!!
Inaonekana Wewe ulikuwa na Mtaji ?
Sikuwa na mtaji wa kutisha mimi nilikuwa na mtaji mkubwa kuliko yule mshusha Bei! [emoji23]
 
Nakumbuka Mimi mtaa huu nilipo tulikuwa wawili tu tunatazamana kwa kutenganishwa na barabara,nilipiga hela Sana Sasa ujana nao nikawa najaza mzigo tu Sina plan nyingine,watu wakashtuka wakaanza kunicopy Mara biashara ikapungua faida ikashuka,kilichonisaidia wakati wao wanalipa Kodi kubwa mim nilikuwa nalipa kidogo,xo walikuwa wanakuja wananiacha ilipokuja Corona mtani uliyumba Sana nikaapa mbele za Mungu Mambo yakikaa sawa nitaanza kujipanga kivingine,so nilipokaa sawa nikaanza kununua mashamba,nikasema acha nijenge kachumba kamoja kwanza maana biashara haitabiriki,nikajenga chumba na sebure ile nimepiga bati nasema ngoja nivute pumzi,akaja mwingine Tena mashindani aixee alikuwa na Kasi yule Ila nikasema ngoja nimuache nimuone,Sasa yeye kamwachia mdogo wake kila siku dogo anampiga buku tano mpaka kumi,nikaona kaanza kupunguza Kasi mpaka sahiz namsoma tu,benefiti niliyonayo Mimi ninauzoefu na biashara yeye analipa laki kwa mwezi Mimi nalipa 50
 
Tatizo Wengine Hawana Mtaji Wa kuweza Kukaza Kipindi kirefu hasa pale Hasala inapotokea !!!!
Inaonekana Wewe ulikuwa na Mtaji ?
Ni kweli hii ili utoboe ni lazima uwe na pesa za ziada za kukuwezesha kustahimili kwa miezi kadhaa wakati mauzo yameshuka,vinginevyo utashindwa kulipia kodi na hata pesa za kujikimu kimaisha utakosa
 
Jamaa alikuja kwa speed alifungua duka la vyakula kama langu karibu yangu
Aisee ilikua ni vurugu mchele maharage alikua anaagiza kutoka mbeya basi alikua anauza bei ya vunja bei kwenye mchele na Maharage, mfano mchele alikua anauza mpaka 1900 kwa sisi wengine ili upate angalau faida kidogo unatakiwa uuze angalau 2200 nikamfuata nikamueleza ndugu biashara haiendi hivyo alichonijibu ni kwamba yeye anapata faida kwa hiyo hajali, basi mimi nikatoa zile bidhaa za maharage na mchele nikatumia nyumbani na familia ila wife aliona uchungu kwa sababu ndio alikua anakaa dukani
Haikupita muda nikapata kazi ifakara Morogoro, nilikuta mchele huo huo anaouza 1900 unauzwa 800 kwa kilo halafu napata usafiri wa bure mpaka mikumi au iringa mjini kwa gari ya ofisi ,yaani mchele ulikua unafika Tanga kwa Tsh 1100 kwa kilo, niliuza mchele 1500 kwa kilo na mzigo ulikua haukauki store, aliona aibu kunifuata mimi akamfuata wife kuomba yaishe, nilikaza kwa sababu nilijua project yangu kule kilosa ni ya miaka minne, hivyo ndani ya mpaka minne ningemnyoosha vya kutosha ila baadae huruma ikanijia
 
Back
Top Bottom