Canabian Rasta
JF-Expert Member
- Aug 18, 2022
- 775
- 1,745
Mimi kuna jamaa alikuja akanikuta hapa nnapouziaga majeneza naye akachukua chumba jirani tu nikawa namuuliza anafungua biashara gani akasema duka la rejareja lakini cha ajabu alipomaliza kukarabati tu nikaona anashusha mzigo wa majeneza kama 200 hivi nikasema poa!
Nikamuacha kama week hivi nione kama ana madhara yoyote kwangu maana mie nilishakuwa maarufu hapa Dodoma nafahamika sana pia najuana na madaktari wengi kiasi kwamba wananiunganishia wateja kila siku then nawapa 10%
Kumbe hii jamaa ilishafanya uchunguzi njia zote za mimi kupata wateja akaanza kupita mule mule akatengeneza connection na hao watu wa hospital ya karibu halafu akawa anawapa zaidi hata ya hiyo 10% kwa kila kichwa halafu bado angle ambayo office yake ilikuwepo ni mbele kidogo karibu na barabara yaani mteja akifika tu anaanzia pale kwake!
Nikaona isiwe tabu nikasafiri kodogo kutafuta mtaalamu wa ndumba kijijini kwetu niliporudi huyu jamaa hakuchukua hata week akafunga na kuhama kabisa! Sitakagi ujinga kwenye mambo ya biashara yangu.
Tangazo zuri la biashara