Inaweza kuwa biashara yako inaenda poa yani kila ukifunga hesabu kimoyo moyo unasema “mambo si ndio haya ! ”
Mara paaaap! Anatokea mshindani mpya aidha
- anafungua pembeni/karibu yako biashara kama yako, copy paste
- mwenye bei za chini,
- bidhaa zake zina ubora zaidi,
- anafanya free delivery,
- anauza kwa mkopo
- Ana connection
Wataeja haoooo!! Taratibu ama instantly unaona mauzo yamepungua sana, wateja wanakauka, siku nzima ni kubadilisha pozi la miguu tu ofisini na kwenda kupiga story hapo nje mpaka jioni.
Hapa ndipo watu huingia tamaa ya kuanza kwenda kwa waganga kutafuta dawa za mvuto wa biashara, kumuangamiza mshindani, n.k. wengi wanaishia kupigwa tu