Tuliowahi kuathirika na washindani wapya katika biashara tukutane hapa, ulipitia wakati gani, ulijiongeza, ulihama au ulifunga biashara?

Ukiona hivo hama location Afu hukohuko unakoenda copy na paste mbinu za aliekuhamisha
 
Noma Sana jamaa alikosa utu
 
Mimi kuna mmiliki wa kinboss spare parts hivi alinifungisha duka la spare za pikpiki mtwara mjini,sisi tulikuwa tunachukua mzigo kwao kule dar tunakuja kuuza huku ila chakushangaza wakafungua branch mtwara mjini mfano kama bulb tunachukua dar kwa 1000 ili tuje kuuza huku 1500 wao wakawa wanauza 1000 kwa rejareja,mfano cam shaft bei ya jumla 10000 wao wanauza kwa rejareja 11000 hii hali iliua sana biashara zetu kwasababu wao wanachukuwa china moja kwa moja
 
Hii alifanya baada ya kuona mzigo mnaochukua ni mkubwa alafu mnaenda Mara kwa mara,navyoona
 
Hii alifanya baada ya kuona mzigo mnaochukua ni mkubwa alafu mnaenda Mara kwa mara,navyoona
Nikweli mkuu uko sahihi ndicho kilichotokea kinboss aliona 70% ya wateja walikuwa ni kutoka mtwara akajua huko mtwara kuna hela ndio maana akaja kufungua hilo tawi na akaja kutuua njaa
 
Nikweli mkuu uko sahihi ndicho kilichotokea kinboss aliona 70% ya wateja walikuwa ni kutoka mtwara akajua huko mtwara kuna hela ndio maana akaja kufungua hilo tawi na akaja kutuua njaa
Kwa hiyo uliishia Wapi ?
 
Kwa hiyo uliishia Wapi ?
biashara ikafa huku nina madeni kibao pango nililimbikiza mpaka ikatimia 1800000 na pia kuna kampuni inaitwa Hairoad nao nikawakopa mali ya milion 12 na kampuni ya SLL nao wananidai milion 4 mpaka leo sijawalipa na laini nimebadilisha sitaki usumbufu mimi na mtwara nimehama
 
Kwanini usingebeba mzigo uhamie masasi?

Naona pamekaa vizuri ki biashara ungepiga hela kama mwanzo tu
 
Kwanini usingebeba mzigo uhamie masasi?

Naona pamekaa vizuri ki biashara ungepiga hela kama mwanzo tu
Unajua tatizo ni mazoea mkuu na ile hali ya kujipa moyo kuwa labda kesho itakuwa hivi kumbe ndio nadidimia ila nashukuru nimekomaa shambani kwenye ufuta nimepata kiasi fulani na nikichanganya na kiasi fulani nakuwa na kama milion 8 ndio nawaza nifungue goli la viatu vya kike au nifungue goli la urembo na vipodozi masasi
 
🤣🤣🤣🤣
 
Hakika mkuu ingia masasi pamechanganya sana kibiashara
 
kwa ujumla wake hii biashara ya kuuza spare kwa watu wa rejareja unaionaje kiongozi.

kuna kitu kinaitwa Return On Investment vipi kwa biashara hii ya spare za pikipiki inaweza chukua mda gani kurudisha mtaji wako?
 
kwa ujumla wake hii biashara ya kuuza spare kwa watu wa rejareja unaionaje kiongozi.

kuna kitu kinaitwa Return On Investment vipi kwa biashara hii ya spare za pikipiki inaweza chukua mda gani kurudisha mtaji wako?
Kiukweli hii biashara ni kama biashara nyingine huwa inategemea ni mji gani upo mfano hebu nijielezee mwenyewe nilianza na mtaji wa milion 28 mwaka 2010 mwezi na wakati huo maduka pale mtwara yalikuwa yakuhesabika kwa pale sokoni maduka yalikuwa 4 tu mpaķa inafika 2013 niliweza kuushika mtaji wangu mkononi huku biashara bado ipo yakutosha
 
oky shukrani mkuu.
 
Mimi kuna jamaa alikuja akanikuta hapa nnapouziaga majeneza naye akachukua chumba jirani tu nikawa namuuliza anafungua biashara gani akasema duka la rejareja lakini cha ajabu alipomaliza kukarabati tu nikaona anashusha mzigo wa majeneza kama 200 hivi nikasema poa!
Nikamuacha kama week hivi nione kama ana madhara yoyote kwangu maana mie nilishakuwa maarufu hapa Dodoma nafahamika sana pia najuana na madaktari wengi kiasi kwamba wananiunganishia wateja kila siku then nawapa 10%
Kumbe hii jamaa ilishafanya uchunguzi njia zote za mimi kupata wateja akaanza kupita mule mule akatengeneza connection na hao watu wa hospital ya karibu halafu akawa anawapa zaidi hata ya hiyo 10% kwa kila kichwa halafu bado angle ambayo office yake ilikuwepo ni mbele kidogo karibu na barabara yaani mteja akifika tu anaanzia pale kwake!
Nikaona isiwe tabu nikasafiri kodogo kutafuta mtaalamu wa ndumba kijijini kwetu niliporudi huyu jamaa hakuchukua hata week akafunga na kuhama kabisa! Sitakagi ujinga kwenye mambo ya biashara yangu.
 
😂😂😂 sio upo pale chako ni chako kweñye kona ukiwa unashuka kwenda katikati ya jiji
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…