Tuliowahi kuchukua mikopo tukafanya ndivyo sivyo

Tuliowahi kuchukua mikopo tukafanya ndivyo sivyo

nilikopa m3 mwaka 2013 nikaanzisha ufugaji wa nguruwe na kuku wa kienyeji na nyingine nikanunua pikipiki. mwaka wa kwanza mambo yalienda vizuri kiasi hasa kwenye boda boda nilikuwa sikosi hela ya kula, balaa likaanza pikipiki ikapata mzinga wa kugongwa na gari.
kuku wakaanza kufa na nguruwe akazaa lakini watoto wakadumaa. maisha yakaanza kwenda mlama kuna kuna kipindi hata buku nilikuwa naiona kama buku ten.
mbaya zaidi demu wangu akaniacha akaniambia nimeshindwa kumhudumia mahitaji yake. Tangu hapo maisha ya kukopa yamenifunza kitu.
 
Daaah!!mi wakati naanza kazi nilikopa 5mil,nilitoa hela yote kwenye account,nikanunua pikipiki ya kutembelea na iliyobaki niliweka gheto ktk bukta flan zile timberland si unajua zinakuaga na mifuko mingi!!bhas bhana mi nakula ugimbi nikiishiwa narudi gheto nazama ndani nachomoa mzigo nasepa naenda kula vyombo!sitosahau Kuna siku naingiza mkono kwenye mfuko imebaki 30,ikabidi niichomoe ile nguo kwenye msumali nikapekua mifuko yote na kukung'uta hamna kitu!!ikabidi nikatoka njee nikaingiza pikipiki ndani nikalala zangu!!
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji16][emoji16][emoji1787][emoji1787][emoji16][emoji16] no comment [emoji2772]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimekopa mara tatu sijawahi kujuta mara ya kwanza nilichukua mkopo 10 Mil nikamalizia ujenzi wa Nyumba nikahamia hivyo nikatoka nyumba ya kupanga, mara ya Pili Nikachukua 40 Mil nikafungua kiwanda kidogo cha kukamua mafuta ya alizeti na nikanunua mashine ya kusaga na kukoboa AISEEE SIJAWAHI KUJUTA KUKOPA

Sent using Jamii Forums mobile app
😴😴😥 fix
 
aiseee huu uzi nime pitia comment zote #391
nina 2.5 M cash ambazo ni za savings nili plan nichukue mkopo wa 3M ili niwe na 5.5 M ndo nianze biashara ila akili ime stuck kwanza naona bora nianze na hii hii 2.5M mkopo nije chukua baadae biashara ikiwa imesha changanya sasa

Sent using Jamii Forums mobile app
Kabisaaa anza na hiyohiyo! Mdogomdogo ndio mwendo!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom