Tuliowahi kudundwa siku ya kufunga shule primary tukutane hapa

[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
We utakuwa ulisoma mkoa wa Kilimanjaro manake kule ndio tulikuwa na mambo hayo kila shule zikifungwa, mikoa mingine sidhani sana.
 
Kuna demu mmoja aliwahi kunidunda njiani siku ya kufunga shule, full kunigalagaza chini hadi walipokuja kuniokoa, alikuwa na mwili mimi nilikuwa kimbaumbau. Kuanzia siku hiyo nilikosa raha yaani full kutaniwa[emoji16], nakumbuka alikuwa anaitwa Augusta kifupi anaitwa 'Ugu', nilikuwa nikizingua kidogo utasikia tutakuitia Ugu, basi nakuwa mpole[emoji13][emoji13], hivi karibuni nimejaribu kumtafuta nimuoe sijafanikiwa kujua alipo wala kupata mawasiliano. Mniombee
 
Kuna mkaka nakumbuka tukiwa standard 5 tumeenda uwanjani kwenye mazoezi akanipigia mpira nilimdunda mpaka akazimia ile wanampandisha kwenye school bus akazinduka ikabidi baba aitwee shuleee nilichezea vitasa sitakaaa nisahau kabisaaaaa
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] aisee
 
Enzi hizo ukitaka uwe vizuri inabidi akili zichaji na mpira uwe unaujua,hutasumbuliwa maanake unafit groups zote. Kuna wale manunda shule zero ila mpira balaa hawa utaelewana nao kwasababu ya mpira. Kuna wale watoto wa mama john visomo hawajui mpira so utaelewana nao kwenye masomo! Enzi zangu nilikuwa naombwa nibaki kucheza mechi za madarasa.
 
Kwa waliosoma muhimbili primary school nadhani mnaukumbuka Barafu Centre

Hicho ndio kilikuwa kiwanja cha hukumu siku za kufunga shule lazima mtu akapigwe au akapige tu

Utoto hahaha siku za kufunga shule zilipokaribia kuwa makini sana mpirani, darasani au mabishano yoyote ilikuwa ndio tiketi ya kwenda kupigana huko muda wa kwenda nyumbani

Na kosa kubwa pale unapojipandisha ktk chati ya wababe wa kupigana wakati wewe ni kibonde...yalinikuta hayo hahaha
 
Hahaa angalia asije akakudunda tena mkuu
 
Nina sura shit balaa mtu alikua akiniangalia anaghairi ugomvi.

Ila roho iliniuma nilizipanga na Mikidadi kisa Salome halafu Salome bado akanichomolea.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…