Tuliowahi kudundwa siku ya kufunga shule primary tukutane hapa

Tuliowahi kudundwa siku ya kufunga shule primary tukutane hapa

Duh! Kumbe Kuna watu watata humu eeh, nilikua mpole nilijaribu mapambano mawili, nikawa na near - miss kwenye mapambano, nikahairisha kuwa mgomvi!
Mm niliacha kupigana toka siku hiyo
 
Kama kichwa cha habari kinavyosema. Enzi zile tunasoma kulikuwa na list ya wakali wa masomo darasani (kumi bora)ambayo ilikuwa official na pia kulikuwa na list ya wababe katika kupigana kuanzia wa kwanza mpk wa mwisho.

Sasa mie nilikuwa mkali sana darasani ila kwenye kupigana nilikuwa kama wa tano wa mwisho hivi so kuna jamaa mmoja alikuwa nae wa mwisho mwisho akataka kupigana na mie ili apande kwenye chat ya ngumi na pambano likapangwa siku ya kufunga shule

Jamaa alikuwa mfupi kuliko mimi so nilikuwa nina uhakika wa ushindi. Siku hiyo shule ilipofungwa pambano likapangwa uwanja wa mpira na darasa zima walikuwepo. Mchezo ulianza vizuri na niliutumia urefu wangu vizuri nikawa ninampa nakozi za kutosha sasa kuna kipindi nikawa naona naelekea kushinda nikawa napigana style ya Mohamed Ali ile ya kuruka ruka kwa mguu mmoja (wahenga mtakuwa mnaikumbuka hii) kumbe yule mpinzania wangu alikuwa ananilia timing.

Jamaa alinitisha kama ananipiga kwa kushota nilipokwepa alinipa konde moja la paji la uso na kulia niliona nyota kama 100 hivi usoni na wakati natafakari jamaa alinirukia kichwa kimoja cha usawa wa mdomoni na nikajing'ata ulimi na kutoka na damu balaa, wakati nikiwa nimevurugwa jamaa alinipiga mtama mmoja mkali nikadondoka kama gunia.

Ilikuwa bahatu yangu maana jamaa alinidhibiti kwa juu lakini wataalam wakaamulia na kusema zipigwe za juu juu ili tupate mshindi

Tuliposimama huku damu zikinivuja mdomoni kama teja anavyotokwa mate nilicheki watu waliotuzunguka nikaona upenyo mmoja nikatoka baruti kama Juma Ikangaa unaambiwa darasa zima likaanza kunikimbiza huku wakinizomea mpk demu wangu wa utotoni (Pili) nae alikuwepo ktk watu waliokuwa wananizomea na kunikimbiza. Nilitimkia ofisi ya mwalimu mkuu ndipo nilipookokea hapo
We jamaa mbona kama nakujua!

Unamkumbuka refa wa game alikua nani?
 
Kuna demu mmoja aliwahi kunidunda njiani siku ya kufunga shule, full kunigalagaza chini hadi walipokuja kuniokoa, alikuwa na mwili mimi nilikuwa kimbaumbau. Kuanzia siku hiyo nilikosa raha yaani full kutaniwa[emoji16], nakumbuka alikuwa anaitwa Augusta kifupi anaitwa 'Ugu', nilikuwa nikizingua kidogo utasikia tutakuitia Ugu, basi nakuwa mpole[emoji13][emoji13], hivi karibuni nimejaribu kumtafuta nimuoe sijafanikiwa kujua alipo wala kupata mawasiliano. Mniombee
umekumiss kipigo ha ha ha
 
Kuna mwalim alikua Kijana Mdogo Mdogo siku ya kufunga shule wanafunzi wakawa wanamvizia basi kila akiingia Darasan kikundi cha wanafunzi wanaenda Nje wanajificha chini ya dirisha Na kuanza kumuimbia "Yassin makamasi, yassin makamasi" halaf wanakimbia...alipowadaka walipigana Makonde..

Nikiwa form1 feza nikitokea St kayumba..aisee nilikula kibano cha mbwa koko toka Kwa jamaa anaitwa Steve, alikua boonge halaf mm njiti dahh sitomsahau Yule umaga !
duh feza si imeanzishwa mwaka 2010 kumbe tunachat na watoto wetu humu
 
Hukuwa mjanja ukitaka kuishi mazuri jenga urafiki na wababe husingedundwa hata mara moja
 
Dah!!!Nimepiga sana watoto wa watu makwenzi[emoji1] [emoji1] , nilikuwa nikiomba askirim sinyimwi[emoji4]
 
sikuwai kupigana ila nlikuwa hodari kuchonganisha watu wapigane, nlikuwa middle man,,, nlikuwa straiker uwanjani,, shule nliiona tamu sana,,,
 
'"zipigwe za juu juu'





hahahahahhh
Hapo umenikumbusha mbali sana aisee
 
Yaani[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]nilikuwa nawashangaa walivyo wakubwa nikawa najiuliza hawa walichelewa wapi?...na walikuwa wanavaa uniform kabisaa basi ni balaaa,nadhani walimu walikuwa wakiingia darasa la MEMKWA walikuwa wapole sana.

Halafu ukiwachokoza unaambiwa "wewe huyo MEMKWA shauri yako ee"..
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] kuna hao wamama wawili tulikua tunapishana nao njiani wakati wa kwenda na kurudi, maana walikua shule tofauti na tunayosoma. Sasa mimi na mashoga zangu tulikua na tabia ya kuwazomea kila tukiwapita tunawaita mama wa darasa, siku moja wakaja kunibamba peke angu, aisee almanusra nijikojolee![emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] kuna hao wamama wawili tulikua tunapishana nao njiani wakati wa kwenda na kurudi, maana walikua shule tofauti na tunayosoma. Sasa mimi na mashoga zangu tulikua na tabia ya kuwazomea kila tukiwapita tunawaita mama wa darasa, siku moja wakaja kunibamba peke angu, aisee almanusra nijikojolee![emoji23] [emoji23] [emoji23]
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]nimecheka jamaniii MEMKWA aaaahhh
 
Back
Top Bottom