Tuliowahi kufukuzwa kazi tukutane tupeane experience

Saa nyingine ukiona mambo hayaendi na HAKUNA sababu ya msingi na ni ghafla...
Unagoma, Hii kuna jamaa yangu aliitumia,
Walimkazia miezi 2, watatu wakaanza tena kumlipa, Bosi akabadilishwa, akalipwa malimbikizo, mshahara ukapanda,
Asaivi ndio anataka aache mwenyewe.
 
Kumbe ndivyo inavyokuwa .

Ndio maana watu wanakufa kwa matatizo ya Figo ,ini na mengineyo

Wanamezeshwa dawa Ila hawaumwi kisa hospital ipate hela za dawa

Shenzi sana
Kaka acha tu, kuna jamaa aliwahi pewa dawa ambazo hazijui, amekuja kuuliza kwa specialists akaambiwa ni dawa za magonjwa ya Quouma wakati ni mwanaume.
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
mm sijawahi kufukuzwa,Ila niliwahi kubembelezwa ni resign nikasita kwa muda mrefu baadae nikaamua kukubali ku resign.Ilikuwa hiv ,baada ya kumalizia tu chuo,niliingia kitaa kusaka kazi,nikatumia wk 2 kuzurula mtaani na kibahasha changu Cha vyeti, world vision nilifika lkn wakanpa maneno ya kunifarj lkn nikaona hapa bila mtu sipat kaz nikaachana nao,Kama zali wk ya pili nikapewa mchongo Kuna project mpya shirika fulani hv Iina launch project mpya, iliitwa LEAD project donors wakiwa UK,jamaa Kama masihara wakanichukua kwa mkataba wa miaka 4,ilikuwa 2013yr hiyo,waka nipost mbeya nikagoma,wakanibembeleza weeee nikagoma nakumbuka tuligoma vituo watu 2,mm na jamaa mmoja kutoka tanga aliitwa Jonas,siku hiyo walipangiwa wote pamoja na jamaa angu,kasoro mm,wakaniambia Rudi baadae tutakupigia sm nikawaambia poa,kweli nikarudi zangu home,usiku saa tano manager wa mladi akanipigia sm,kuwa wamenipa iringa nikamwambia poa nitaenda,Nika join iringa,nikiwa kule nilikuwa situlii kila mala naingia internet kuchek mashirika mengine,maana nilijua private sector Kuna michezo michafu na rafu nyingi,muda wowote kinaweza kunuka.

nikiwa iringa 2014,nafasi za ajira zikatoka govt,fasta nikatuma maombi , interview tuliitwa arusha,mwaka huo nikaajiriwa govt mkoa wa mbeya,wilaya ya kyela,nikawakumbuka wazungu waliokuwa wananibembeleza niende mbeya na LEAD PROJECT,nikaona nimebugi Sana kuwagomea kipnd kile.ss nikawa napga govt na LEAD PROJECT,Ila kwa Siri ,boss wangu kule gvt sikumficha maana nilijua nisipompa mchongo kupga huku na kule itakuwa inshu,uzur boss alikuwa sosho Sana,akasema dogo piga kaz usjal,Ila ukiwa unachomoka hapa nipage taarifa,nikamwambia poa .

Sasa baada ya miez 3, LEAD PROJECT HQ,wakasanuliwa na jamaa mmoja tulikuwa nae pale iringa lead project,wakawa Wana nipigia masim kibao ni resign ,nikawakazia ,nilijua hawawez kunifukuza na tayari mkataba nilisha saini.

Niliendelea kupga Kaz huku na huku,Ila kero za masm zilikuwa Mara kwa Mara,wakiniuliza ume saini Kaz govt nawabishia nawaambia hapana ,hakuna kitu Kama hicho,wakiwatuma wakuda waje iringa Kuna jamaa yangu mwngine alikuwa best wa ukweli kwangu,akawa ana nitonya fasta yy alikuwa na ndg yake HQ dar so alikuwa anapata taarifa mapema za project kutoka HQ. Jamaa walichanganyikiwa kweli,kunifukuza hawawezi ,so wakabaki kunipiga saund ni resign.

Siku moja,nikatoka iringa ,kwenda mbeya kazn govt,asbh nikiwa kyela,nikapigiwa sm,kupokea jamaa akajitambulisha yy ni manager kampuni moja inaitwa utravet ,HQ zao ziko Kenya,kwa hapa tz ni Arusha ,akaniambia natakiwa kuripoti Arusha ndani ya siku 3, nisaini mkataba na utravet ,baada ya kusaini natakiwa kwenda Kenya pale Nairobi seminar ya 2wks,akaniambia ulituma email yako tangu mwaka Jana 2013 ,nikamwambia kweli,Basi jamaa akasisitiza hapa huta piga interview yoyote ,wameiona CV yangu hawana haja kunifanyia interview,ni kusaini mkataba na kukwea piga Nairobi kwa seminar,nikirudi Nita manage mkoa wa morogoro na Dodoma,usafr kila ktu poa.

Nikampigia jamaa angu mmoja ,Kama anawajua vizuri hawa utravet ,akaniambia jamaa Kama wamekuita nenda ,wako vzr Sana Tena Sana,Kuna vijipesa vya kipuuzi puuzi kibao .akanipa na contact ya best ake ambae alikuwa bado anapiga nao Kaz mkoa wa mwanza,aise nikabaki sijui Cha kuamua.Niko bado na mkataba na LEAD PROJECT,nimeajiliwa govt ndo kwanza Nina miez Kama 3,huku napewa offer na utravet .
 
Huku ni kuhujumiana afya sasa kwa tamaa ya Pesa du!
 
Kaka acha tu, kuna jamaa aliwahi pesa dawa ambazo hazijui, amekuja kuuliza kwa specialists akaambiwa ni dawa za magonjwa ya Quouma wakati ni mwanaume.
[emoji16][emoji16][emoji3]
 
Inategemea na unataka nn kwenye life kama ni mtaji ili ufanye ishu zako nenda private sector.Kama ni unataka uhakika wa kutokufa njaa baki serikalini
 
Mbona Una povuka bure kila mtu na experience yake bana usitake watu wafanane hyo kitu, hafu kazini superstar wa Nini kwani Kuna kina diamond mule. Hafu majungu sio lazima eti mtu awe juu, mbona hata wafagizi ofisi wanapigwa majungu. Hafu sio kila ofisi watu wanaajiriwa permanent nyingine contract na mda mfupi mfupi ebo.
Acha kupanic na experience za watu bure
 
Ni wapi nimesema nimefukuzwa kazi humu humu mbona mnadandia vitu eti tuko same level plus blah blah nyingi zisizo kichwa Wala miguu, hafu na hayo Mambo ya wivu mbona umekazania wivu tu, hivi watu kuchongeana ili mtu kuonekana mwema mbona huwa ni hulka ya mtu. Usinilishe maneno yako unayofikiri kichwani na mabandiko marefu ambayo sijamaliza kusoma ata
 
Emu eleza ulijuaje kwamba jiwe alikua na chuki na Mwere

so na mimi nikiwa na assumption kama zako, naweza sema Mwere alinunuliwa ili atangaze ugonjwa usiokuwepo?
NB: tusiharibu thread ya watu.
Mtazamo wangu maana daily alikuwa anamsema anatumiwa na mabeberu, that's sadist behavior.
 
Usilo lijua ni sawa na usiku wa Giza naona unapenda ligi kweli.
 
I can spot lies a mile away....

Nikufanyie ligi for the sake of it kuna pahala nalipwa au nafaidika na lolote?

Hakuna mtu anafukuzwa kazi pahali bila sababu!
Dah eti you can spot a lies a mile away bila vivid evidence ni kujifuraisha na kujifariji hasa unapotaka Mambo ya wengine yawe ka akilini mwako unavofikiria.
Usitake tufanane hapa duniani loh
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…