Tuliowahi kufukuzwa kazi tukutane tupeane experience

Pole sana mkuu
 
Hakuna sehemu yenye fitina kama sehemu yenye ugali.

Nilishawahi kuondolewa kazini kisa nimeingia pale mimi mgeni halafu navuta pesa ndefu kuliko wakongwe. Zikaanza fitina,ilikuwa kwenye mradi fulani hapa nchini,zikaanza kutumwa habari za uongo makao makuu ya ofisi. Yakatokea yakutokea nikaja kuondolewa kazini. Nikasema sawa nikampa taarifa wife,akaniambia rudi tu mjini. Utapata kingine kilicho bora na wewe,huwezi jua Mola amekuepushia nini.

Baada ya miaka miwili,nikakutana na boss wa ile Kampuni,yuko na boss wangu mpya,alikuja kuomba mkopo kwa ajili ya kupewa mradi serikalini. Ila huyu boss siwezi kumlaumu shida alio wapa majukumu,aliwaamini na walikuwa wana fitina sana.

Ukitimuliwa sehemu usianze kulia lia,ondoka huwezi jua umeepushiwa nini hasa kama sehemu kuna fitina na wivu wa kijinga.
 
Kuna mfanyakazi mmoja ameachishwa kazi baada ya kupata msiba watu wameenda kumpa pole kufika wakakuta mjengo wa maana
Alivyorudi kazini anaulizwa hela ya kujenga nyumba kama hii kaipata wapi

Daah [emoji23]
 
Hahahahahah usiwe una mjini Huyo Jamaa ana mental issues
 
Nipe namba za huyo hod nimtukane tu potelea pote
 
Mpuuz Sana Joyce
 
Nilishafukuzwa kazi mara mbili. Ya kwanza ndio ilikuwa mbaya sana nililipwa mshahara na kuambiwa kazi imekwisha nikasota sana nikaitwa interview pamolive na cocacola nikakutana na mzungu roho jiwe interview ya kiingereza cha Liverpool ikawa yes no majibu nikapewa no job. Nikabahatika kupata kazi nikawapiga tukio Wakenya nikaamua kujiajiri tu. Nikangalia hawa waajiriwa nawasikitikia sana.
 

sio mtego kweli
 
Kuna mama mmoja kapata madaraka chupi ye kufukuza Kazi mtu bila utaratibu ni SAwa na kunywa pepsi kwa roho yake mbaya hana familia hadi leo angekuwa na familia kama mzazi angekuwa anatafakari mara mbili, madaraka ni koti la kuazima.
 
"Walimu mnapiga kelele kama watoto wa primary"..[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…