Kiongozi hii thread yako imenikumbusha machungu Makubwa sana.
Nilivomaliza chuo nikapata sehemu ya kujishikiza bn, nikapiga kazi miezi mitatu tu nikapandishwa hadhi kidogo bana. Kazi ikaendelea, baada ya Mwaka mmoja kuisha, Kiongozi mmojawapo katika ofisi yetu akapa nafasi ya kuajiriwa serikalini, kampuni ikanipa nafasi yake. Kumbe ile hali wenzangu ambao tulikuwa tunafanya nao kazi walichukia sana. Why me?
Sijawa na hili wale like, mdogo wangu akauugua, wadogo zangu wengine walikuwa wanasoma bado secondary, so ikabidi nichukue likizo ya siku 14 kwanza nikamuuguze, bahati mbaya haikuwa riziki akafariki. Baada ya kumaliza matanga, nilirejea kazini, lakn haikuisha hata mwezi mama akaugua.
Akapelekwa hospital, akawa anakaa na dada yangu, kila wikend lazima niwe huko, nikalazimika kumhamishia kwangu (getho) pamoja na sista, afu Mimi nikawa nalala kwa mpangaji mwezangu msela. Uguza weee, hadi hela ikakata. Kazi nikiwa naendelea nayo lakini.
Basi bana nakumbuka ilikuwa Tarehe 1/10 tukaenda kuchukua mshahara, nilivyofika kwa mhasibu akanipa mshahara wangu na barua. Kuifungua, eti nimeachishwa kazi!
Kosa silijui. Basi ile hela yote nikamtibia mama, lakini haikufua dafu. Nikauza kabati la nguo laki 100,000/, nikauza sofa langu elfu 70, latop hp, 150,000,, uza king'amzi na TV, na dish lake 170,00, friji 70,000 nikaendelea kumtibia mama. Nilivyoishiwa kabisa, mama akapona!
Basi tukarejea kijijini, nikaanza kulima nyanya. Nikipeleka maombi ya ualimu hata shule za kata nakataliwa! Naambiwa nitaitwa lakn siitwi. Nyanya hakuna wanunuzi. Ikabidi nianze kuvua samaki, lkn wapi.
Wale watumishi wenzangu hata hawapokei simu yangu, kila surauali sasa hainitoshi, mwonekano umeshazidi umri wangu halisi. Nimezeeka balaa.
Sema ndo hivo siku hazifanani, nilikuja kupata pa kujishikiza na maisha yanaendelea. Lakn ukweli kuamka bila kujua pa kwenda ni shida.