Tuliowahi kufukuzwa kwa watu/kwa ndugu tukumbushiane ilikuwaje

Tuliowahi kufukuzwa kwa watu/kwa ndugu tukumbushiane ilikuwaje

okoyoko

JF-Expert Member
Joined
Jun 15, 2014
Posts
2,664
Reaction score
3,641
Hello guys,

Hapo zamani kabla sijaijua dunia vizuri, nlikuwa napenda sana kukaa kwa ndugu kipindi cha likizo (shule zikifungwa) au kwenye familia ya marafiki zangu..nlikuwa nkijihis comfortable na happy kabisa kukaa kwa watu

Mtazamo wangu kuhusu kukaa kwa watu ulibadilika baada ya mm kufukuzwa kutoka kwa ndugu kisa kuna kitu kilipotea then mm nlihisiwa kua ndo nimeiba, nlipewa maneno makali sana, roho iliniuma sana na niliapa kua sitakaa nije kukaa kwa MTU hata iweje, bora nilale kwenye gunia barabarani, kuliko kuomba hifadhi ya kukaa kwa MTU, uzuri sahivi najitegemea kipesa na nina sehemu yangu ya kukaa kwa hiyo sijali watu, wakiniambia niwatembelee nawaambia haya ntakuja, ila rohoni nawa-enjoy tu. Nlichogundua ni kuwa kumtegemea mtu ni mateso sana

Wadau mliokutana na hii kadhia njooni m-share experience zenu..
 
Jinsia yako tafadhali?
 
Dah, nlishakaa kwa ndugu. Sasa wakasafiri, kuna mshkaji akanitembelea. Sasa mi utaratibu wangu ilikuwa nalala na kuondoka asubuhi. Sijawahi kushinda kwene hiyo nyumba, wala kushika chochote kama labda TV redio n.k. Sasa mshkaji aliyenitembelea akakesha sebuleni akiangalia movie kwene TV.

Kesho yake tukaondoka. Wenyeji waliporudi napigiwa simu kuambiwa nimeharibu TV. Nliporudi nikaikuta iko poa tu, jamaa aliweka input itoke kwene disc yake na ni kitu ambacho wangeweza kung'amua bila kunipigia simu ila ndo hivyo wakawa na haraka ya kunilaumu.

Cku nyingine tena nyumba hiyo hiyo niliwatembelea mchana, nikakaribishwa vizuri na huosegirl sebuleni. Nikashika kidude flani hivi juu ya meza. Nlipoondoka nikakiacha palepale. Baadae napigiwa simu kimepotea. Ni kitu ambacho hata ningekichukua kisingenisaidia chochote wala nisingekitumia. Dah! nikajiona kama hapo kwene nyumba hiyo si pema kwangu.
 
Mimi nilikuwa nikifika kwa ndugu kama walikuwa wanataka kuandaa chakula wanahairisha mpaka niondoke na mm nilikuwa najifanya naondoka halafu naludi nakuta wanakula aisee walikuwa wanachukia balaa kweli sasa nmekuwa sihitaji kudoea kwa mtu maana unakuta anakushupalia usogee kula kumbe kwenye ulmwengu wa roho yake hataki usogee "wanakunjua sura wanakunja roho".....
 
Dah umenikumbusha mbal sana nilikua kwa uncle wangu kw mda nikaenda kulala chumba ambacho analala mtoto wak asubuh mama mtu alifungua mlango dah ctosahau alinitoa umo chumbani kama mbwa eti nitamfunza mwanae tabia za kihuni kama kuvuta ngada dah nltok nduki ctorud tena
 
Aisee kweli maisha mabonde na milima.
 
KUNA TWO SCENARIOS!
Baada ya wazazi kufariki, mimi na mdogo wangu tulichukuliwa na baba yetu mkubwa!
Life wasn't tht okey but Yatima hadeki ujue! maisha yakasonga!
Siku moja ilikuwa mkesha wa pasaka, mdogo wangu na watoto wa baba yangu mkubwa (walikuwa wakubwa zaidi yangu)

Wakaenda kanisani mkesha! mi nilikuwa naumwa sikutaka kusali usiku.
Walikuwa wadada watatu,Mmoja akaona ndio wakati wa kwenda kuchachua ,wanarudi nyumbani bila yeye!

Baba yangu mkubwa anamfokea mdogo wangu(ninayemzidi miaka 5, anaaambiwa arudi alikotoka na asirudi mpk atakapompata yule asiyerudi home). Yule baba alifunga mlango ,nje bariki kali nyumba ipo milimani flan hvi!He was asthmatic, hata kama asingekuwa asthmatic ,how on earth unamwambia mwingine asilale mpk aliyeenda kwenye starehe zake arudi!

Nilikaa ndani kama nusu saa hivi nikiwa nalia!
Nilipotoka nilienda subeleni unapokaa funguo haukuwepo!means ameingia nao kulala!
Nilliingia jikoni nikachukua shoka lile nafikir ,Nililinyanyua juuu kushuka chini kishindo kiliamsha mpk sisimizi!

wakaamka, ananitishia kunipiga!NIKAMWAMBIA NEXT STEP AFTER WHERE YU ARE NAKUPASUA!

nilifunguliwa mlango nikamfuata mdogo wangu alipo nikamwingiza ndani!
kesho yake asbh kabla hajasema ondoka au baki nilikuwa nje na mabegi na mdogo wangu namwambia tunarudi kwenye nyumba ya wazazi!

2. Huko kwenye nyumba ya wazazi alikuwepo mama yetu mdogo na wanae!
NAKO MAISHA YALIKUWA YA KIWEHU TU KWA DOGO!!
huko nilifukuza mimi!

Nikamwambia unajua nini, HII NYUMBA NI YA MAMANGU, isingekuwepo wewe ungekuwa unalipa kodi!

SASA FANYA HIVI!
NAENDA KUMALIZA MTIHANI WA KIDATO CHA SITA! nikirudi uwe umetafuta pa kukaa!
ilikuwa ni likizo ya mwezi wa nne ,pepa ya necta mwezi wa tano!
Niliporudi nilimkumbusha!

MPAKA KESHO I AM THE LAST PERSON KWENYE FAMILIA KUAMBIWA TAARIFA YOYOTE INAYOHITAJI MAAMUZI YA PAMOJA
 
Back
Top Bottom