Nakumbuka ilikuwa Dar mitaa ya Sinza Vatican, nilimtembelea ndugu yangu, asee jamaa alikuwa mkorofi balaa. Akirudi toka kazini lazima aguse li TV lake la uchogo, kama limechemka huo moto wake hata kwa gari la zima moto hauzimiki!!
Siku ikipikwa nyama anahesabia jikoni. Mkishakula lazima ahesabu zilizobaki.
Vitimbi vilikuwa vingi na alikuwa anatusurubu ka vile si ni wafungwa!! Siku moja nilitoka nduki kali, sikuwahi kurudi huu ni mwaka wa 11.
Nilipofika home mkoani nilimsimulia mama, siku hiyo alinipikia kilo nzima ya wali, akapakua kwa sinia kubwa na juu kasimika bakuli kubwa la nyama za kuku! Nilivua shati kuanza kutupia nyali tumboni huku nikijisemea, "ewe ndugu mchoyo wa Dar, njoo uhesabu minyama inayoshuka tumboni"