Tuliowahi kufukuzwa kwa watu/kwa ndugu tukumbushiane ilikuwaje

Tuliowahi kufukuzwa kwa watu/kwa ndugu tukumbushiane ilikuwaje

KUNA TWO SCENARIOS!
Baada ya wazazi kufariki, mimi na mdogo wangu tulichukuliwa na baba yetu mkubwa!
Life wasn't tht okey but Yatima hadeki ujue! maisha yakasonga!
Siku moja ilikuwa mkesha wa pasaka, mdogo wangu na watoto wa baba yangu mkubwa (walikuwa wakubwa zaidi yangu)
Wakaenda kanisani mkesha! mi nilikuwa naumwa sikutaka kusali usiku.
Walikuwa wadada watatu,Mmoja akaona ndio wakati wa kwenda kuchachua ,wanarudi nyumbani bila yeye!
Baba yangu mkubwa anamfokea mdogo wangu(ninayemzidi miaka 5, anaaambiwa arudi alikotoka na asirudi mpk atakapompata yule asiyerudi home). Yule baba alifunga mlango ,nje bariki kali nyumba ipo milimani flan hvi!He was asthmatic, hata kama asingekuwa asthmatic ,how on earth unamwambia mwingine asilale mpk aliyeenda kwenye starehe zake arudi!
Nilikaa ndani kama nusu saa hivi nikiwa nalia!
Nilipotoka nilienda subeleni unapokaa funguo haukuwepo!means ameingia nao kulala!
Nilliingia jikoni nikachukua shoka lile nafikir ,Nililinyanyua juuu kushuka chini kishindo kiliamsha mpk sisimizi!
wakaamka, ananitishia kunipiga!NIKAMWAMBIA NEXT STEP AFTER WHERE YU ARE NAKUPASUA!

nilifunguliwa mlango nikamfuata mdogo wangu alipo nikamwingiza ndani!
kesho yake asbh kabla hajasema ondoka au baki nilikuwa nje na mabegi na mdogo wangu namwambia tunarudi kwenye nyumba ya wazazi!

2. Huko kwenye nyumba ya wazazi alikuwepo mama yetu mdogo na wanae!
NAKO MAISHA YALIKUWA YA KIWEHU TU KWA DOGO!!
huko nilifukuza mimi!
Nikamwambia unajua nini, HII NYUMBA NI YA MAMANGU, isingekuwepo wewe ungekuwa unalipa kodi!
SASA FANYA HIVI!
NAENDA KUMALIZA MTIHANI WA KIDATO CHA SITA! nikirudi uwe umetafuta pa kukaa!
ilikuwa ni likizo ya mwezi wa nne ,pepa ya necta mwezi wa tano!
Niliporudi nilimkumbusha!
MPAKA KESHO I AM THE LAST PERSON KWENYE FAMILIA KUAMBIWA TAARIFA YOYOTE INAYOHITAJI MAAMUZI YA PAMOJA
Dah....una mtu? [emoji7] [emoji7] [emoji7] [emoji8] [emoji7] [emoji14]
 
Nakumbuka ilikuwa Dar mitaa ya Sinza Vatican, nilimtembelea ndugu yangu, asee jamaa alikuwa mkorofi balaa. Akirudi toka kazini lazima aguse li TV lake la uchogo, kama limechemka huo moto wake hata kwa gari la zima moto hauzimiki!!

Siku ikipikwa nyama anahesabia jikoni. Mkishakula lazima ahesabu zilizobaki.

Vitimbi vilikuwa vingi na alikuwa anatusurubu ka vile si ni wafungwa!! Siku moja nilitoka nduki kali, sikuwahi kurudi huu ni mwaka wa 11.

Nilipofika home mkoani nilimsimulia mama, siku hiyo alinipikia kilo nzima ya wali, akapakua kwa sinia kubwa na juu kasimika bakuli kubwa la nyama za kuku! Nilivua shati kuanza kutupia nyali tumboni huku nikijisemea, "ewe ndugu mchoyo wa Dar, njoo uhesabu minyama inayoshuka tumboni"
[emoji23][emoji23][emoji23] navuta picha ulivokua unakula na hilo sinia lako [emoji23][emoji23][emoji23]
 
Ila wakat mwengine hata sie wageni tuna tabu zetu!
Kuna lindugu lake faza la kike
Age kama 25 lilikuja home litafutiwe kazi na mzee
Kufika likawa linamnyenyekea maza kumbe ki unafiki
Lilipopata kazi likawa halimsemeshi maza
Kila muda limenuna tu

Home kwao linasema linanyanyaswa na maza.lilipotoka home likaolewa nasikia saivi linaishi maisha ya shida sana.
 
Kwa watu hakufai...nimezaliwa miaka mingi iliyopita...ila nilisimuliwa nilipozaliwa mama alikuwa akiishi kwa kaka yake...ile kukojoa kwangu kama kichanga kitandani mama akatimuliwa...nilisimuliwa hadi leo huyo mjomba namwona Hitila....yeye amesahau mimi nakumbuka!
same here...mama alinisimulia nlipokua mdogo alipata shida ya macho ikabidi arudi kwao,mama wa kambo na ndugu zake waliyomtenda yaani nimejikuta nawachukia naturally hata nijitahidi vipi kufake nashindwa walah!!!
 
Hello guys,

Hapo zamani kabla sijaijua dunia vizuri, nlikuwa napenda sana kukaa kwa ndugu kipindi cha likizo (shule zikifungwa) au kwenye familia ya marafiki zangu..nlikuwa nkijihis comfortable na happy kabisa kukaa kwa watu

Mtazamo wangu kuhusu kukaa kwa watu ulibadilika baada ya mm kufukuzwa kutoka kwa ndugu kisa kuna kitu kilipotea then mm nlihisiwa kua ndo nimeiba, nlipewa maneno makali sana, roho iliniuma sana na niliapa kua sitakaa nije kukaa kwa MTU hata iweje, bora nilale kwenye gunia barabarani, kuliko kuomba hifadhi ya kukaa kwa MTU, uzuri sahivi najitegemea kipesa na nina sehemu yangu ya kukaa kwa hiyo sijali watu, wakiniambia niwatembelee nawaambia haya ntakuja, ila rohoni nawa-enjoy tu. Nlichogundua ni kuwa kumtegemea mtu ni mateso sana

Wadau mliokutana na hii kadhia njooni m-share experience zenu..
Watu kama nyie mnavunja moyo watu wenye moyo kusaidia ndugu! Kifupi naishi na ninasomesha wadogo zangu 2 na mtoto wa dada 1 maana ktk ukoo mimi ndio niko hapa town, so wakimaliza primary huwa nawachukua baadhi nakuwatafutia shule nzuri ili nao baadae mambo yawe safi...! Nimesoma post yako na baadhi ya coment nimevunjika moyo aisee! Inawezekana nadhani ninasaidia ndugu zangu kumbe baadae nikalaumiwa kama coment nyingi zinavyoonesha hapa! Ee Mungu nisaidie nisipoteze urithi wa wanangu kusaidia watu wasio na shukurani!
 
Nakumbuka ilikuwa Dar mitaa ya Sinza Vatican,

Nilipofika home mkoani nilimsimulia mama, siku hiyo alinipikia kilo nzima ya wali, akapakua kwa sinia kubwa na juu kasimika bakuli kubwa la nyama za kuku! Nilivua shati kuanza kutupia nyali tumboni huku nikijisemea, "ewe ndugu mchoyo wa Dar, njoo uhesabu minyama inayoshuka tumboni"

Mambo ya kuhusu TV chogo nyuma ili kuangalia kam iliwashwa sehemu nyingi sana hata mdingi alikua na michongo hii!!!
 
Watu kama nyie mnavunja moyo watu wenye moyo kusaidia ndugu! Kifupi naishi na ninasomesha wadogo zangu 2 na mtoto wa dada 1 maana ktk ukoo mimi ndio niko hapa town, so wakimaliza primary huwa nawachukua baadhi nakuwatafutia shule nzuri ili nao baadae mambo yawe safi...! Nimesoma post yako na baadhi ya coment nimevunjika moyo aisee! Inawezekana nadhani ninasaidia ndugu zangu kumbe baadae nikalaumiwa kama coment nyingi zinavyoonesha hapa! Ee Mungu nisaidie nisipoteze urithi wa wanangu kusaidia watu wasio na shukurani!
Watu wako tofauti mkuu. Cha msingi fanya unachofanya kwa moyo mmoja na usitegemee kushukuriwa. 1/10 ndo hushukuru kwa matendo.
Pray for the best but expect the worst.
 
Watu wako tofauti mkuu. Cha msingi fanya unachofanya kwa moyo mmoja na usitegemee kushukuriwa. 1/10 ndo hushukuru kwa matendo.
Pray for the best but expect the worst.
Umesema kweli mkuu, na ukifatilia hao wanaofanikiwa baada ya kulelewa/kusaidiwa na ndugu wengi wao hawanaga moyo wa kusaidia hata ndugu zao!
 
Haya maisha noma sana. Uncle alituambia kesho tukamsaidie jirani yake kuvuna mpunga. Hakuna kitu nilikuwa nachukia kama kulima. Nipe kazi zote lakini sio shamba. Mimi nikajitia nunda sikwenda. Nikapiga tu kazi za home fresh. Hakuniambia mimi, akampa salam mkewe. Nashangaa aunt ananambia uncle kasema hanipi pesa ya tution. Nikasema poa. Bahati nzuri hajawahi kunipa hata pesa yake. Tulikuwa tunakomaa na mkewe kupiga mishe pesa nilikuwa napatia humo bahati nzuri alikuwa ananikubali kwa utendaji kazi. Jamaa alikuja kupigwa chini job sasa hivi choka mbaya. Ila maisha mungu fundi
 
Aisee nakumbuka kipindi kile nasoma A level ,basi bwana likizo moja nikaenda kumtembelea bro yangu(mtoto wa baba mkubwa) alikuwa anasoma chuo Dsm, nimekaa wiki ya kwanza ,wiki ya pili nikagundua bro ana mahusiano na demu wangu niliyemuacha nyumbani,kila akifika mida ya saa 6 usiku bro alikuwa anatoka nje then anaanza kuongea na huyo demu ,nilikuja kugundua nilipokuta call history kibao kwenye cm yake ,sikutamani tena kuendelea kukaa pale,nilitoka ghafura likizo nikaenda kuimalizia home,ama kweli kikulacho ki nguoni mwako
 
Nakumbuka ilikuwa Dar mitaa ya Sinza Vatican, nilimtembelea ndugu yangu, asee jamaa alikuwa mkorofi balaa. Akirudi toka kazini lazima aguse li TV lake la uchogo, kama limechemka huo moto wake hata kwa gari la zima moto hauzimiki!!

Siku ikipikwa nyama anahesabia jikoni. Mkishakula lazima ahesabu zilizobaki.

Vitimbi vilikuwa vingi na alikuwa anatusurubu ka vile si ni wafungwa!! Siku moja nilitoka nduki kali, sikuwahi kurudi huu ni mwaka wa 11.

Nilipofika home mkoani nilimsimulia mama, siku hiyo alinipikia kilo nzima ya wali, akapakua kwa sinia kubwa na juu kasimika bakuli kubwa la nyama za kuku! Nilivua shati kuanza kutupia nyali tumboni huku nikijisemea, "ewe ndugu mchoyo wa Dar, njoo uhesabu minyama inayoshuka tumboni"
Tena ukawa unakula huku majasho yanakutoka[emoji1] [emoji1] [emoji1]
 
Alifanya vyema na haki saaana.
Mimi shule walizosoma wadogo zangu kote walinijua, nna kamwili tu ka kinyonge lakini walipowatendea visivyo wadogo zangu vurugu lake kila kitu kinasimama hapo shuleni. Walimu wananichukia mpaka wenyewe wanaanza kunipenda.
Hujawahi kukutana na walimu watata ambao wamewadhibiti wanafunzi wanaojifanya wana harakati.

Na kama huna speaking skills nzuri,unadhibitiwa hadi unajuta.
 
Nakumbuka ilikuwa Dar mitaa ya Sinza Vatican, nilimtembelea ndugu yangu, asee jamaa alikuwa mkorofi balaa. Akirudi toka kazini lazima aguse li TV lake la uchogo, kama limechemka huo moto wake hata kwa gari la zima moto hauzimiki!!

Siku ikipikwa nyama anahesabia jikoni. Mkishakula lazima ahesabu zilizobaki.

Vitimbi vilikuwa vingi na alikuwa anatusurubu ka vile si ni wafungwa!! Siku moja nilitoka nduki kali, sikuwahi kurudi huu ni mwaka wa 11.

Nilipofika home mkoani nilimsimulia mama, siku hiyo alinipikia kilo nzima ya wali, akapakua kwa sinia kubwa na juu kasimika bakuli kubwa la nyama za kuku! Nilivua shati kuanza kutupia nyali tumboni huku nikijisemea, "ewe ndugu mchoyo wa Dar, njoo uhesabu minyama inayoshuka tumboni"
hahaaaaaa nilianza kukuonea huruma ili huku mwisho nimecheka sana aisee, ila huyo ndugu vipi kuhesabu nyama?? tobaa
 
Back
Top Bottom