Tuliowahi kufukuzwa kwa watu/kwa ndugu tukumbushiane ilikuwaje

Tuliowahi kufukuzwa kwa watu/kwa ndugu tukumbushiane ilikuwaje

Dah, nlishakaa kwa ndugu. Sasa wakasafiri, kuna mshkaji akanitembelea. Sasa mi utaratibu wangu ilikuwa nalala na kuondoka asubuhi. Sijawahi kushinda kwene hiyo nyumba, wala kushika chochote kama labda TV redio n.k. Sasa mshkaji aliyenitembelea akakesha sebuleni akiangalia movie kwene TV. Kesho yake tukaondoka. Wenyeji waliporudi napigiwa simu kuambiwa nimeharibu TV. Nliporudi nikaikuta iko poa tu, jamaa aliweka input itoke kwene disc yake na ni kitu ambacho wangeweza kung'amua bila kunipigia simu ila ndo hivyo wakawa na haraka ya kunilaumu.
Cku nyingine tena nyumba hiyo hiyo niliwatembelea mchana, nikakaribishwa vizuri na huosegirl sebuleni. Nikashika kidude flani hivi juu ya meza. Nlipoondoka nikakiacha palepale. Baadae napigiwa simu kimepotea. Ni kitu ambacho hata ningekichukua kisingenisaidia chochote wala nisingekitumia. Dah! nikajiona kama hapo kwene nyumba hiyo si pema kwangu.
Pole
 
Nafkiri hii ipo sana kwa jamii ya huko kwenu tz bara ila huku kwetu tunasema Zanzibar ni njema na atakae aje hata ukitaka kukaa mwaka utakula utalala na hutoulizwa kitu.
 
Mkuu sa
Hizo tabia zinakera sana mkuu
Sijui watu wa hivi huwa wana matatizo gani ya akili
Anatengeneza mazingira kama mnamnyanyasa.
Unakuta familia nzima mpo sebureni mnakula ila yeye yupo huko chumbani peke yake

Mara nyingi ni ndugu za sisi wanaume.
Sahihi kabisa, km mwanaume hana akili iliyotulia mke anageuka mgeni na mkiwa nyumbani kwake!
 
Wengine tu matendo...nimetoka zangu kijijini nikaenda mjini kumtembelea uncle...ukipakuliwa ugali kwenye hotpot wanakukaribisha mezani halafu wao wanabaki wakizugazuga...unaambiwa kapakue chakula...ukiangalia chakula cha kula peke yangu nisishibe naambiwa niwaachie na wao...basi nikawa nakula kidogo halafu naingia kwa mama ntilie nashindilia nguna ya kutosha...kwa watu hakufai
We jamaa atutofautiani aseeeh nimecheka sana[emoji16][emoji16]
 
Wale tuliokaa kwa watu tukanyanyasika kwa namna moja au nyingine, tusilipize kisasi kwa kuwafurahia ndugu zetu kwa kuchoka kiuchumi au kiafya,

Tuzidi kuwapenda na kuwajali. Haswa chakula( kutokana na maisha niliyoishi napenda sana kumpa MTU chakula) bila chakula huwezi kuishi. Chakula kinaufungua moyo alafu nguo ( mashati na vitenge) alafu na vielfu 30/10.) Itategemea na uwezo wetu!

Mungu ni wa wote. Masikini na matajiri, wakosefu na watakatifu...
 
Mie
bora kusaidia wapita njia kuliko.ndugu
Mimi nitamsaidia ndugu yangu... Lazima Kbl ya rafiki au shost.... Yesu kristo alianza kuteua mitume kutoka kwa ndugu zake, ie binamu zake. Na pia kuna mstari kitabu cha methali kimeandika kuwa NDUGU WAMEZALIWA WASAIDIANE KATIKA SHIDA....

SITOMTELEKEZA NDUGU WA TUMBO MOJA, MILELE AMINA. SO HELP GOD.
 
Mm nilipanga chumba nilikuwa naish mwenyewe,sasa kulijuwa kuna shoga angu anadanda danda tu hana makazi maalum ya kulala mara leo kalala kwa shoga huyu mara yule ,mara kwa bwana huyu mara yule,akanihadithia anavyopata tabu pakulala nikaona isiwe shida nikamwambia njoo ukae kwangu huku unajichanga ili baadae na ww upange chumba chako sitokuchaji gharama yyote , poa akaja maisha yakaendelea baada ya kuzoeana mambo yakaaza kuharibika,mara kavaa viatu vyangu bila ruksa yang,mara nguo zangu nikamwambia mm sipend tabia hiyo wala huwa sivalian na mtu nguo yaan hasikii bado anavaa nikiwa sipo lakin baadae akirud naona kavaa vitu vyangu akiniona anajichekesha,mara chupi zangu hasa zile mpya mpya labda nilivaa mara moja au mbil sizion,mara hereni hazionekan ukimuuliza mm sijui wakat tunaish wawili! Yaan alinichosha kwa tabia yake ya wiz na tamaa hata ukisema na ww uvalie vitu vyake ana viatu vya maana wala nguo za maana,nilimfanyia visanga mpaka alihama nikiamua namnunia bila sabab
 
Ukienda kukaa kwa MTU lazima ujiandae kisaikolojia, kama umeenda kusalimia soma alama za nyakati ukiona umechokwa ondoka.Kama unasoma au unatafutiwa kazi jali malengo yako yakitimia shukuru Mungu na washukuru wenyeji wako.Tambua wao ni familia na hawawezi kukupenda wewe zaidi ya wanavyopendana wao ,wakiwa faragha watakujadili ,usisononeke wala usihofu jitahidi kuishi kama wenyeji wako wanavyotaka,jitahidi muagane mkiwa marafiki, binaadamu wanahitajiana ,wakati mwingine kuishi kwa ndugu hakukwepeki
 
Mm nilipanga chumba nilikuwa naish mwenyewe,sasa kulijuwa kuna shoga angu anadanda danda tu hana makazi maalum ya kulala mara leo kalala kwa shoga huyu mara yule ,mara kwa bwana huyu mara yule,akanihadithia anavyopata tabu pakulala nikaona isiwe shida nikamwambia njoo ukae kwangu huku unajichanga ili baadae na ww upange chumba chako sitokuchaji gharama yyote , poa akaja maisha yakaendelea baada ya kuzoeana mambo yakaaza kuharibika,mara kavaa viatu vyangu bila ruksa yang,mara nguo zangu nikamwambia mm sipend tabia hiyo wala huwa sivalian na mtu nguo yaan hasikii bado anavaa nikiwa sipo lakin baadae akirud naona kavaa vitu vyangu akiniona anajichekesha,mara chupi zangu hasa zile mpya mpya labda nilivaa mara moja au mbil sizion,mara hereni hazionekan ukimuuliza mm sijui wakat tunaish wawili! Yaan alinichosha kwa tabia yake ya wiz na tamaa hata ukisema na ww uvalie vitu vyake ana viatu vya maana wala nguo za maana,nilimfanyia visanga mpaka alihama nikiamua namnunia bila sabab
Duh unà roho mbaya
Mtenda hutendewa hata kwa kizazi chake
 
Nilikaaga kwa ndugu kipind nasoma!sio ndugu wa karibu saaaaana! Nilichokuwa nakifanya...nilikuwa nafanyakazi km punda hata kule kwetu ckuwa nafanya! Naamka alfajiri nawasha mashine yakufua naanza kufua nguo, machine inaendelea kufua nafanya kaz za ndani, kuaandaa chai ya asbh n.k na kaz nyingine zote nikilala usiku km punda nmechoka + watoto! Mama mwenye nyumba kiguu na njia!
Cku nikifunga shule nakwenda kwetu,shule zikifunguliwa cku ntayoingia ile nyumba naanza na usafi jikoni store ambapo huwa nakutana kumeoza! Yule mama alikuwa Ana chukichuki na watu lkn alkuwa ananipenda ajabu! Akirud safar zake anakuta mambo yote yapo sawa! Lazma huwa anibebee zawadi pesa alinipa n.k! Alifurahia uwepo wangu hata watoto wake walinipenda Sana,!
Nilipomaliza form six alinizawadia cheni ya dhahabu hereni na Pete! Ckuamini!
Jaman hakuna MTU dunia ya sasa anaetaka kukaa na MTU..hata ndugu hawatakani! Tunapokaa na watu inabd tu tujitutumue tujipendekeze ilimradi tusichokwe!
MTU anaenda kukaa ugenini labda anasoma n.k unaleta uvivu jeuri kiburi yaan hapo lazma uchokwe!
Mschna unaenda ugenini unalala masaa yote..ukiamka kaz zote zmefanywa mpaka chai umeandaliwa! Aibu...hata km hakuna kazi..amka tuu! Jifanyishe kitu chochote kile..omba hata viguo ufue tuu utathaminiwa!
Tusilalamike kufukuzwa kuteswa kumbe sisi wageni ndio wenye shida! Japo kuna case nyingine ziko tofaut kidogo
 
Mm nilipanga chumba nilikuwa naish mwenyewe,sasa kulijuwa kuna shoga angu anadanda danda tu hana makazi maalum ya kulala mara leo kalala kwa shoga huyu mara yule ,mara kwa bwana huyu mara yule,akanihadithia anavyopata tabu pakulala nikaona isiwe shida nikamwambia njoo ukae kwangu huku unajichanga ili baadae na ww upange chumba chako sitokuchaji gharama yyote , poa akaja maisha yakaendelea baada ya kuzoeana mambo yakaaza kuharibika,mara kavaa viatu vyangu bila ruksa yang,mara nguo zangu nikamwambia mm sipend tabia hiyo wala huwa sivalian na mtu nguo yaan hasikii bado anavaa nikiwa sipo lakin baadae akirud naona kavaa vitu vyangu akiniona anajichekesha,mara chupi zangu hasa zile mpya mpya labda nilivaa mara moja au mbil sizion,mara hereni hazionekan ukimuuliza mm sijui wakat tunaish wawili! Yaan alinichosha kwa tabia yake ya wiz na tamaa hata ukisema na ww uvalie vitu vyake ana viatu vya maana wala nguo za maana,nilimfanyia visanga mpaka alihama nikiamua namnunia bila sabab
[emoji3] [emoji3] [emoji3] [emoji3] eti wamnunia bila sababu!
 
Dah! umenikumbusha majonzi niliyo nayo mpaka nahisi kulia. nimekaa kwa ndugu zaid ya miaka mitatu, nimemfanyia biashara zake bila mkataba, mim nilikuwa msimamiz kwa kila kitu. nimefanya kazi kwa uaminifu wa hali ya juu. nimemwingizia faida kubwa mno, ila mwisho wa siku nilifukuzwa kama mbwa.pia kuna kipind mie nilikuwa namiliki duka mkoa fulan hiv sasa nikapata safari ya kwenda kukaa miaka miwili. nikamwachia duka la milion mbili. akanitumia laki nne. pesa nyingine mpaka leo haja nilipa. nimeonda kwake bila kunipa pesa ambazo nilifanyia kazi na ambazo nilikuwa namdai. nilitaka kumshitaki wakanishauri kuwa sina mkataba wowote ambao tuliandikishana. nimeamua kusamehe najipanga upya.
 
Back
Top Bottom