Tuliowahi kufukuzwa kwa watu/kwa ndugu tukumbushiane ilikuwaje

Tuliowahi kufukuzwa kwa watu/kwa ndugu tukumbushiane ilikuwaje

BORA ulivyofukuzwa mkuu,ungeendelea kutegemea Ndugu ungekuwa masikini hata hela ya kununua bando ungekosa.


Shida yangu sio kufukuzwa mkuu, ila kufukuzwa kwangu kuliambatana na chuki pamoja na kuwaziwa mabaya, yani MTU anaongea na ww, unahisi kabisa kuwa huyu ananichukia, ila mm kwa upande wangu nikiri nilikuwa nina makosa ya kukaa kwa ndugu bila machale, simlaumu sana huyo alienifukuza maana binadamu hatufanani, sitorudia hayo makosa King Kong III
 
Mwaka Fulani nilikuwa Mwanza tuition na mshikaji wangu tulienda kukaa familia ya mwalimu wetu Wa primary, sasa kuna mshikaji alipoteza elfu kumi duh tulihisiwa tumeiba maneno yakawa mengi sana, uzuri hatukufukuzwa.
 
Shida yangu sio kufukuzwa mkuu, ila kufukuzwa kwangu kuliambatana na chuki pamoja na kuwaziwa mabaya, yani MTU anaongea na ww, unahisi kabisa kuwa huyu ananichukia, ila mm kwa upande wangu nikiri nilikuwa nina makosa ya kukaa kwa ndugu bila machale, simlaumu sana huyo alienifukuza maana binadamu hatufanani, sitorudia hayo makosa King Kong III
Pambana ili wanao wasije kukaaa kwa ndugu.
 
Ushapata CV yake? Mwambie tumewekeza kwa binti yetu .. akalkuleti ada ya kuanzia nasare mpk yunivasite... hicho ndicho kishika uchumba kabla hatujazungumzia mahari
Ndo mana nimeleta kwako baba!!
Mambo ya kuingilia maamuzi ya ukoo nayataka Mimi?
 
Ni kuomba MUNGU AKUPE UHAI ULEE WANAO WAFIKE MAHALI PA KUJITEGEMEA mkuu!!
Sisi tulienda kukaa kwa NDUGU ilhali wazaI waliacha nyumba kubwa tu!!
Ila dah!!
Huu Uzi umejua kunivurugia siku!!
Pole sana snowhite kwa mapito.
 
Ukienda kukaa kwa MTU lazima ujiandae kisaikolojia, kama umeenda kusalimia soma alama za nyakati ukiona umechokwa ondoka.Kama unasoma au unatafutiwa kazi jali malengo yako yakitimia shukuru Mungu na washukuru wenyeji wako.Tambua wao ni familia na hawawezi kukupenda wewe zaidi ya wanavyopendana wao ,wakiwa faragha watakujadili ,usisononeke wala usihofu jitahidi kuishi kama wenyeji wako wanavyotaka,jitahidi muagane mkiwa marafiki, binaadamu wanahitajiana ,wakati mwingine kuishi kwa ndugu hakukwepeki


Kwa upande wangu kuishi kwa ndugu kunakwepeka, nkikosa sehemu ya kulala sehemu ya ugenini kisa uhaba wa pesa, ni heri nilale barabarani kwenye maboksi, kuliko nkaombe hifadhi kwa ndugu el bandido
 
Daah wewe 'mseng.e'unaonekana unapenda sana kula km bedui[emoji38][emoji38][emoji38]
Nakumbuka ilikuwa Dar mitaa ya Sinza Vatican, nilimtembelea ndugu yangu, asee jamaa alikuwa mkorofi balaa. Akirudi toka kazini lazima aguse li TV lake la uchogo, kama limechemka huo moto wake hata kwa gari la zima moto hauzimiki!!

Siku ikipikwa nyama anahesabia jikoni. Mkishakula lazima ahesabu zilizobaki.

Vitimbi vilikuwa vingi na alikuwa anatusurubu ka vile si ni wafungwa!! Siku moja nilitoka nduki kali, sikuwahi kurudi huu ni mwaka wa 11.

Nilipofika home mkoani nilimsimulia mama, siku hiyo alinipikia kilo nzima ya wali, akapakua kwa sinia kubwa na juu kasimika bakuli kubwa la nyama za kuku! Nilivua shati kuanza kutupia nyali tumboni huku nikijisemea, "ewe ndugu mchoyo wa Dar, njoo uhesabu minyama inayoshuka tumboni"
 
Dah umenikumbusha mbal sana nilikua kwa uncle wangu kw mda nikaenda kulala chumba ambacho analala mtoto wak asubuh mama mtu alifungua mlango dah ctosahau alinitoa umo chumbani kama mbwa eti nitamfunza mwanae tabia za kihuni kama kuvuta ngada dah nltok nduki ctorud tena
nipo nawaza ulivyotoka nduki nacheka tu...
bila shaka hapo kwenye avatar ni wewe?
 
Hello guys,

Hapo zamani kabla sijaijua dunia vizuri, nlikuwa napenda sana kukaa kwa ndugu kipindi cha likizo (shule zikifungwa) au kwenye familia ya marafiki zangu..nlikuwa nkijihis comfortable na happy kabisa kukaa kwa watu

Mtazamo wangu kuhusu kukaa kwa watu ulibadilika baada ya mm kufukuzwa kutoka kwa ndugu kisa kuna kitu kilipotea then mm nlihisiwa kua ndo nimeiba, nlipewa maneno makali sana, roho iliniuma sana na niliapa kua sitakaa nije kukaa kwa MTU hata iweje, bora nilale kwenye gunia barabarani, kuliko kuomba hifadhi ya kukaa kwa MTU, uzuri sahivi najitegemea kipesa na nina sehemu yangu ya kukaa kwa hiyo sijali watu, wakiniambia niwatembelee nawaambia haya ntakuja, ila rohoni nawa-enjoy tu. Nlichogundua ni kuwa kumtegemea mtu ni mateso sana

Wadau mliokutana na hii kadhia njooni m-share experience zenu..
Kwahilo namshukuru sana late Baba, maana alikuwa hataki uende kokote baki kwenu tu,yaani hata ndugu akija home akikupa zawad unamwangalia kwanza mshua mood yake au aseme chukua lasivyo akiondoka tu unalo,ila nilipo anza kujitambua miaka hiyo ndo nikamwelewa mshua (R.I.P)
 
Dah, nlishakaa kwa ndugu. Sasa wakasafiri, kuna mshkaji akanitembelea. Sasa mi utaratibu wangu ilikuwa nalala na kuondoka asubuhi. Sijawahi kushinda kwene hiyo nyumba, wala kushika chochote kama labda TV redio n.k. Sasa mshkaji aliyenitembelea akakesha sebuleni akiangalia movie kwene TV. Kesho yake tukaondoka. Wenyeji waliporudi napigiwa simu kuambiwa nimeharibu TV. Nliporudi nikaikuta iko poa tu, jamaa aliweka input itoke kwene disc yake na ni kitu ambacho wangeweza kung'amua bila kunipigia simu ila ndo hivyo wakawa na haraka ya kunilaumu.
Cku nyingine tena nyumba hiyo hiyo niliwatembelea mchana, nikakaribishwa vizuri na huosegirl sebuleni. Nikashika kidude flani hivi juu ya meza. Nlipoondoka nikakiacha palepale. Baadae napigiwa simu kimepotea. Ni kitu ambacho hata ningekichukua kisingenisaidia chochote wala nisingekitumia. Dah! nikajiona kama hapo kwene nyumba hiyo si pema kwangu.
tafuta pesa nyingi alafu ukawatembelee tena hakika utayapenda mapokezi...
 
Wengine tu matendo...nimetoka zangu kijijini nikaenda mjini kumtembelea uncle...ukipakuliwa ugali kwenye hotpot wanakukaribisha mezani halafu wao wanabaki wakizugazuga...unaambiwa kapakue chakula...ukiangalia chakula cha kula peke yangu nisishibe naambiwa niwaachie na wao...basi nikawa nakula kidogo halafu naingia kwa mama ntilie nashindilia nguna ya kutosha...kwa watu hakufai
ahaa hiyo wazee wa kubet tunasema ni BOTH TEAMS WILL SCORE
 
Nilikaaga kwa ndugu kipind nasoma!sio ndugu wa karibu saaaaana! Nilichokuwa nakifanya...nilikuwa nafanyakazi km punda hata kule kwetu ckuwa nafanya! Naamka alfajiri nawasha mashine yakufua naanza kufua nguo, machine inaendelea kufua nafanya kaz za ndani, kuaandaa chai ya asbh n.k na kaz nyingine zote nikilala usiku km punda nmechoka + watoto! Mama mwenye nyumba kiguu na njia!
Cku nikifunga shule nakwenda kwetu,shule zikifunguliwa cku ntayoingia ile nyumba naanza na usafi jikoni store ambapo huwa nakutana kumeoza! Yule mama alikuwa Ana chukichuki na watu lkn alkuwa ananipenda ajabu! Akirud safar zake anakuta mambo yote yapo sawa! Lazma huwa anibebee zawadi pesa alinipa n.k! Alifurahia uwepo wangu hata watoto wake walinipenda Sana,!
Nilipomaliza form six alinizawadia cheni ya dhahabu hereni na Pete! Ckuamini!
Jaman hakuna MTU dunia ya sasa anaetaka kukaa na MTU..hata ndugu hawatakani! Tunapokaa na watu inabd tu tujitutumue tujipendekeze ilimradi tusichokwe!
MTU anaenda kukaa ugenini labda anasoma n.k unaleta uvivu jeuri kiburi yaan hapo lazma uchokwe!
Mschna unaenda ugenini unalala masaa yote..ukiamka kaz zote zmefanywa mpaka chai umeandaliwa! Aibu...hata km hakuna kazi..amka tuu! Jifanyishe kitu chochote kile..omba hata viguo ufue tuu utathaminiwa!
Tusilalamike kufukuzwa kuteswa kumbe sisi wageni ndio wenye shida! Japo kuna case nyingine ziko tofaut kidogo


Kuna ndugu wengine naturally wanakuwa hawakupendi/ au hawapendi kukaa na wageni nyumbani kwao, kwahiyo hata upige sarakasi za aina gani utachonga viazi tu korino
 
Back
Top Bottom