Sie tupo wawili mimi ni mdogo wangu wakike mzee baada ya kuzaliwa tu miaka mitatu baadae akamtelekeza bumkubwa,siyo wa sabuni wala chupi,wakati huo bimkubwa akiwa hana nyumba wala kazi yoyote bali akiuza tu tuvitenge na shuka za kigoma,huku akiwa anaumwa ugonjwa wa sicle cell,ambao ilikuwa kila week lazma apigwe chupa za damu,the best moment ambayo sitaisahau katika maisha yangu ni kumbeba mama yangu mgongoni kwangu na kumpeleka hospitali hata usiku wa manane na kumrudisha enzi hizo ilikuwa gari mkoa mzima hazifiki hata 100 kwa idadi.vijibiashara vyake mwwnyewe akawa hivyo hvyo pamoja na kupata sent ndogo ndugu zake wakawa wanawaleta watoto zao akae nao na yeye alikuwa ni mtu wa watu akawa anaishi nao kama watoto zake nakumbuka hata nguo za skukuu walikuwa wanaanza kununuliwa wao the ndo sie tunafata,kimbembe kinaanza baada ya bumkubwa kufariki kwa sicle cell,hivyo kutufanya kulelewa na ndugu zake.nakumbuka wenyewe tuko shule ya msingi tunabebeshwa mgongoni wajukuu wa mtoto wa mama yangu mdogo mgongoni,kila wakija asubuhi na kuwarudisha nyumbani kwao jioni,kwenye chakula wao watakula chipsi kinachobakia(makombo ndo mnapewa nyinyi),na hata upande wa nguo ile nguo ambayo wameshaivaa na kuichoka ndizo ambazo huwa tulikuwa tunapewa.mme mtu alikuwa ni full kutufokea hata kama hakuna kosa tulikula msoto hadi pale nlipofika form 6 nikiwa nasubiria matokeo dogo akiwa form 5.wakati huo mme wa mamdogo akiwa na ugonjwa wa kisukari.basi akawa anaendelea na visa vya kila namna huku kunamda unamskia akimfokea mke wake atufukuze wakiwa chumbani wenyewe,but hakuwahi kutuambia face to face sababu alikuwa hana,inshort nlikuwa mpole mno na nisie na makuu japo wenzangu walisoma shule za bei ghali sie tukasoma kayumba,shule ambayo tulikuwa tunanunuliwa shati 2 kwa mwaka na suruali na sketi moja kwa mwenzangu.basi kuna siku nimechelewa kurudi mida kama ya saa 3,dah basi alinifokea na kunitukania mno mpka mama yangu,kiukweli moyo uliniuma kama unachomwa na moto wa koroboi maana nlikuwa naambiwa mpka kamtafute mama yako na baba yko,dah basi ilivyofika asubuhi nikaondoka,mungu alikuwa upande wangu kufika mida ya mchana bodi ya mkopo waktoa majina nami nkiwemo basi kuna dalali nlikuwa nafahimana nae nkamwelezea yote ikatafutwa nyumba nkàpta chumba na baraza kwa elf 30 wakati huo,yule mzee alinipa mwezi niwe nmeshalipa,basi sku hyo hyo nkahamia maana dalali alinkopa hela kidogo,then nkamfata ndugu yangu maisha yakaanzia hapo tukiwa tunalala kwenye vijigodoro mungu alitusaidia tukafungua vijiabishara vyetu mwisho wa siku tuko hapa now kila mtu na familia yake na kazi pia,japo mzee yule alikatwa mguu huwaga naendaga kumuona mara moja kwa miez mitatu hadi mi 4 na kila tukienda huwa analia mno kwa kujutia alotufanyia maana ni mengi mno japo mengne sikuyaelezea ,na ukiangalia wale watoto wenzetu walokuwa wanasoma international now wanashinda kwa kubeti tu mjini.
My advise kwa vijana unapokaa kwa mtu kaa kwa malengo ya mda mfupi uondoke usiseme unapokaa kwa mtu et kwenu hapana tafuta kwako mapema kwani ipo sik watakuchoka tu
Jerybanks