OKW BOBAN SUNZU
Platinum Member
- Aug 24, 2011
- 53,868
- 121,001
Just for experience na majuto kama yapo.
Mimi sikudakwa ila niliponea chupchup,jamaa alichelewa kama sekunde 50 hivi. Ogopa sana mwanamke mwenye gari.
Huyu dada alikuwa mchepuko kwa takribani mwaka hivi. Alikuwa huru sana muda wowote yupo available na mimi kuona hivyo nikajiongeza kwamba atakuwa single mother. Dada mzuri na mtoto mmoja. Kumbe alikuwa mke wa mtu mumewe akiishi mbali. Hakuwahi kuniambia.
Basi kumbe siku hiyo mumewe siku hiyo alikuja kushiriki pamoja sherehe ya harusi ya rafiki wa familia.
Yule dada alikuwa amekolea mpaka nikawa naogopa,huyu atakuja kuniharibia ndoa yangu. Basi bwana siku hiyo ya harusi akaniambia ameni miss kinyama anataka hata nimkumbatie tu moyo wake utulie (wanawake ni shida).
Saa tano usiku akanitext nitoke nje yupo na bajaji. Haikuwa kawaida yake kuja na bajaji mara zote hutumia gari ananipakia tunabaki humu hata masaa manne. Kumbe gari alimuachia mumewe kwenye harusi akamdanganya amechoka sana atangulie.
Alipofika nikachezwa machale,nikamwambia just a minute sijisikii vizuri,akaelewa nikaingia kwenye bajaji nikampiga kiss dakika 1 akaondoka. Baada ya dakika 2 gari yake ikapita pale tulipokuwa ikapaki kidogo na kuondoka. Kulikuwa na watu wengi maana ni eneo la lodge na bar.
Nikahisi hali ya hatari,baadae ile gari ikarudi ikakaa kama nusu saa hivi mimi nimebana sehemu naicheki.
Baada ya mtiti kutulia anakuja kunipa mkanda mzima. Kumbe siku hiyo aliyefuata nyuma ni mumewe akimfuatilia. Hata gari iliporudi walikuwa wote,walirudi baada ya kula kichapo akiamriwa ataje alikuwa na nani kwenye bajaji. Akanisimulia mumewe ni mtu wa maudhi sana,walivyokuwa kwenye harusi alimuudhi ikabidi aje kupoza machungu kwangu. Kwenye Mapenzi mazito kuna shetani,shetani wa kuwatia upofu
Kwa kweli wanawake ni majasiri sana. Tukae nao kwa akili.
Mliowahi kudakwa ugoni kazi kwenu kutiririka