Tuliowahi kupata ajali na kunusurika tukutane hapa

Tuliowahi kupata ajali na kunusurika tukutane hapa

Nishanusurika Kuliwa na Mamba iyo miaka ya 2000 nilikuwa kama age 8 tu. Nishawai kunusurika kufa maji niliogelea kina kirefu nikawa nazama chini narudi juu nazama narudi ila bahati nzuri kuna njemba iliniona ikaniokoa. Nilisha wai kuota Nimekufa kwenye maji yaani ile nakufa tu nikashtuka toka usingizini. Miaka iyo iyo ya 2000. Ya mwaka jana ndo balaa ngoja niliskip tu


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Natokea Dar kuja Arusha bus likapasuka tairi la mbele upande wa dereva halafu tupo spidi,tulichoshukuru Mungu hakuna gari iliyokuwa inatokea upande wa pili hususani lori kwani dereva wa busi ilibidi apambane kupunguza spidi kwanza ili kuweka busi pembeni,tulikuwa tunayumba barabara nzima kwa dakika kama nne hivi. Hapo ndiyo nilipowasifu wanawake,waliporomosha maombi hatari wakati sisi tunatafuta madirisha ya kuruka. Eneo lilikuwa Hedaru kwa wanaofahamu
 
Natokea Dar kuja Arusha bus likapasuka tairi la mbele upande wa dereva halafu tupo spidi,tulichoshukuru Mungu hakuna gari iliyokuwa inatokea upande wa pili hususani lori kwani dereva wa busi ilibidi apambane kupunguza spidi kwanza ili kuweka busi pembeni,tulikuwa tunayumba barabara nzima kwa dakika kama nne hivi. Hapo ndiyo nilipowasifu wanawake,waliporomosha maombi hatari wakati sisi tunatafuta madirisha ya kuruka. Eneo lilikuwa Hedaru kwa wanaofahamu
duh😮😮😮
 
Dah kuna siku nipo guest na mke wa mtu mama flan hivi amaizing kumbe bhana mme wake kapewa taarifa kwamba nipo guest akachukua masela eti lengo wakinikuta mle ndani wanifakamie bahati ilikuwa upande wetu jamaa wamekuja pale yue mhudumu wa guest ni alikuwa mtu wangu maana kuna siku huyo huyo mama mke wa mtu alinichomesha maindi pale ikabidi nimtafune yeye basi walipofika akawaonyesha chumba kingine halafu faster akanitumia sms bahati nzuri tulikuwa bado hatujaanza kuchungulia njemba naziona zinazama kwenye chumba kingine sie tukatokea mlango wa uwani nduki bodaboda yeye kwake mie kwangu hiyo ilikuwa moja ya ajari mbaya sana kwangu ambayo nilipona nyingine ni za kawaida tu kama ile ya treni 2001 igandu nyingine yakawaida pia boti yetu ilibinuliwa na kiboko ila nikapona fresh kabisa mungi ni mwema kwa kweli
 
Kipindi flani nikiwa na miaka 10 nilikoswa koswa kugongwa na pikipiki ikiwa kwenye spidi kali sana, bahati ilikuwa kwangu ila kwa yule dereva inasikitisha.

Tukio lilikuwa hivi.......

Pale mtaani nilipokuwa nikikaa kulikuja gari moja karandinga bovu bovu limechakaa sana, linatembea barabarani ni kelele tu Parapapraprapraprapaparaaa kelele zikisindikizwa na moshi mwingi mweusi,
Bila kusahau mimi na watoto wenzangu wengi tu tulikuwa pamoja nalo kulisindikiza, mara paap likazima pembeni kidogo ya barabara tukawa tunalisubiri liwashwe ili tuendelee kulisindikiza, ukapita muda mrefu bila lile karandinga kuwaka nikaona niondoke niende nyumbani.

Kumbuka hapo nilikuwa upande wa pili wa barabara na lazima nivuke ili niende nyumbani, sasa wakati navuka barabara ghafla naona pikipiki hii hapa iko kasi sana, dah nilipatwa na mshtuko nikaongeza kasi ya kukimbia ili isinigonge, wakati huohuo yule dereva nae alikuwa akinikwepa, akaingia pembeni kwenye majani kuna mti hivi wa muarobaini akaugonga hapo aisee, kulisikika kishindo kikubwa watu waliokuwepo pale wakapiga kelele haah haah kafa yulee kafa yulee.

Aisee nilikimbia mbio nyingi sana nikisindikizwa na kelele za watu kamata huyoo kamata huyoo, niliingia moja kwa moja chumbani mapigo ya moyo yananienda mbio sana nahema ulimi nje, sikutoka tena nje siku hiyo kwa woga nilikaa ndani natafakari ingekuaje kama ningegongwa na ile pikipiki. Nikawa najiuliza atapona kweli yule jamaa daah hili tukio sitalisahau. Mpaka leo najiuliza ilikuwaje mpaka sikusikia mlio wa ile pikipiki ikija.
Nilinusurika kwa staili hiyo aisee.
 
Natumai hamjambo wakuu,

Kusafiri imekua sehem ya maisha yetu ajili yakutimiza majukum yetu japo kuna nyakati hugharimu maisha na kusababisha vilema kwa manusura.

Binafsi nimenusurika mara kadhaa but mara ya kwanza nilikua natoka Moro-Dar kwa gari ndogo, tairi ya mbele ilichomoka gari ikabinuka matairi yakawa juu bt mungu ni mwema hakuna aliedhurika sana isipokua majeraha madogo.

Mara ya pili Kigoma-Mwanza kwa bus, basi liligonga ng'ombe wanaokatiza karibu 20 nakupoteza mwelekeo kila1 wetu alisali sala ya mwisho akijua hakuna kupona bt mungu ni mwema tulinusurika gari haikuanguka.

Mara ya tatu, ilikua kwa dala dala gari lilishika moto mbele kila mtu aliruka kujiokoa, hapa nilipata majera kiasi ajili ya heka heka zakujiokoa.

Karibu nawe utupe visa vyako.
Ilikuwa mwaka 1994 tunatoka dar kuja mwanza enzi hizo mabasi classic ni scania ndo kama ilivyo tutong kwa sasa, leyland ndo kama makopolo. Tulipanda scania inayobeba mizigo juu. Ilikuwa ukitoka dar utalala singida mida ya saa sita ama saba hivi. Basi bwa mzigo ukaimbaaaaaaa ngoma sita tupo singida. Tukalala pale. Asubuhi ikaondoka kuitafuta sekenke. Bwanaweee mida kama saa tano hivi nlikuwa sina seat na tulikuwa 9 watu familia moja tunaenda christmass nakumbuka ilikuwa tr 22 dec kitu kikaitika hadi miguu juu. Ilikuwa basi la super champion, tulipewa bodi na semi dereva akapanda tuta la pembeni bus ikapitiliza hadi nje ya barabara.nakumbuka tulikuwa zaidi ya abiria 120 kwenye bus maana tuliosimama tu tulisimamia mguu mmojammoja. Na nlikuwa nimesinzia. Nlikuwa ndo nimemaliza la saba tunaenda likizo home

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom