Tuliowahi kupata pesa na kufilisika/kufulia, tujikumbushe hapa

Kuna jamaa yetu alipewa hela baada ya mzee wake kufariki million 29.Kipindi hiko kuna nyumba inauzwa million 7 tukamshauri anunue wapi.Yeye alidai mipango yote bandari salama.Bwana kwanza hiyo safari kutoka Kahama to Dar ,Nzega alilala huku anakula bata,Singida hivyo hivyo Dodoma bata kwa kwenda mbele,Moro mwendo uleule.Baada ya mwaka kupita namuona tena Kahama nilimwambia "ntakutandika makofi ".

Baada ya kuanza kuniambia kaka unajua hutu tubiashara twa kuuza mafuta ya vibaba na nyanya chungu tunalipa watu hawajui tu.Kwa sasa hana hata 100 tunambeba ndugu yetu kinachopatikana tunagawana.
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji3]Maisha noma sanaa...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hahahaha hela za urithi zinawatoa wengi akili.



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pole mkuu..naelewa hali unayopitia!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ilikua 2015 nilipata kazi ya miez 6 programu iliokua chini ya wizara ya ardhi na wadernmark fulan nikapiga mill 35 aiseee nikanunua hiace used moja mil 12 hela nyingne nilikula bataa nikaenda southafrica nikakaa mwezi mzima kurud sina hata mia ile hiace kwakua nilinunua used walinipiga ikaanza kusumbua saaana baadae ikapata ajali na sikua na ile insurance kubwa nayo ikawa kama imepotelea hewan ikauzwa screpa kwa bei ya kutupwa.

Aiseee kila nikiikumbuka ile hela roho inaniuma saana laiti kama ningetuliza kichwa vzr ningeweza fanya mradi endelevu mzuri na ningekua mbali kibiashara..ikabidi nirud tena kuajiriwa kwa vihela kiduchu
 

Mungu akubariki saana Mkuu!


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
huyu ndugu yako kavunja record humu😆😆😆😆😆😆😆
 
haahaha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…