Tuliowahi kupata pesa na kufilisika/kufulia, tujikumbushe hapa

Nilimuamini ndugu yangu miaka hiyo,akawa anakuja mjini nampatia lita za mafuta ya taa akauze kijijini nikiamini baada ya muda mambo yangu yatakaa poa. Matokeo yake baada ya kuuza, fedha akawa anatumia kwa matumizi yake binafsi na starehe, siku namuuliza mapato vipi ....badala ya majibu nikawa nimezua ugomvi.

Basi nikakubali matokeo ikabidi nijipange upya.
 
Ikibaki laki hapo ndio lile wazo la kwenda kununua bia kutafakari nini kilitokea linakuja.
 
Hukua unajua pesa uifanyie nn ndo maana ikaisha kuna watu wanatoboa kwa pesa za madanga
 
Jasiri haachi asili,usikute bado unadanga
 
2010s Rafiki ake na bamkubwa alipiga kama m20 hivi..
Jamaa alikula bata laana, kila akija home anakuja na Taxi yupo na mademu.
Alikua akitaka kwenda chooni anakodi gari ihampeleka Tanganyika Hotel..ipo kando ya ziwa Tanganyika.

Siku moja alikodi prado akaenda nalo kasulu akarudi nalo limechafuka akapita sokoni akanunua katon kadhaa za machupa ya maji. Akaenda na gari lake hadi forodhani ujiji akaita vijana waoshe gari lake wakaosha kwa maji ya ziwa, wakati wanataka kulisuza alikataaa kua maji ya ziwani hayana hadhi akatoa yale machupa kwenye buti ndio akasuzia..

December 2012 alikuja home kwenye sherehe..tukawa tunachuna nae mbuzi. Basi akaniambia father kwa jinsi nilivyopigika hata nikiletewa meli inauzwa shilingi 20 sina uwezo wa kuinunua. Jamaa siku hizi anaushi kama yahaya..ukisikia mdananda ndio yeye. Hana future kabisa
 
Jomoni jomoni [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] nacheka ka mazuri
 
Pole sana mkuu
 
Mkuu nimepitia comment zote humu ila hii nimecheka kwa sauti hadi majirani nje wamekaa kimya ghafla. Naomba unisamehe sana
 
Duh
 
Hahahahahahahaha! Naomba niongezee maneno machache hapo, tatizo sio pesa zina yeyuka tatizo ni kwamba zile pesa tunazo wahonga hamjazitolea jasho so huwezi ukawa na uchungu nazo kwenye matumizi sababu unajua kesho ama kesho kutwa danga lingine litakupa ama danga la zamani litarudi upya!

My advice nidhamu ya pesa ni jambo muhimu sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…