Tuliowahi kupata pesa na kufilisika/kufulia, tujikumbushe hapa

Tuliowahi kupata pesa na kufilisika/kufulia, tujikumbushe hapa

Mkuu nimepitia comment zote humu ila hii nimecheka kwa sauti hadi majirani nje wamekaa kimya ghafla. Naomba unisamehe sana
hahahaha...kampala acha kabisa mji wenyewe unakushawish kutumia hela...maana starehe jijini pale duuh acha..
Mimi kuna siku nilienda nikiwa kwa akaunt nina kama laki 9,huwezi amini laki 600k ilikatikia mji ule...alafu sio mtu wa totozi kivile
 
mimi ndo ngedere kabisa nilifanya kazi kwenye kampuni ya gas ndan ya miaka mi3 nilipata kama milion 10 nikanunua pikipki yakutembelea nikawa kazi yangu kuwafata mademu na kwenda kula bata beach demu nikimpata mtandaon hata awe anakaa kibaha namfata na pikipiki kiukwel sikuamin kama ile hela ingekuja kuisha nilikuwa naiona nyingisana kumbuka mii nmetokea familia ya kimasikin iv nnavyoandika hapa nmerud naish hom kwa baba na mama sina hata mia mfukon

[emoji23] [emoji23][emoji23][emoji23]
 
Pole sana kaka,huwa tunajifunza tunapoanguka japo kwa maumivu makali sana,hela yako yoyote iweke sehemu ambayo ukiitaka lazima ikupe ugumu wa kuichukua ila ukiiweka sijui bank huku ukitembea na ATM Card mfukoni jua hiyo siyo yako.

Pia usimkopeshe mtu hata kama ndugu pesa yako iweke kwenye assets japo ukiwa na shida maisha utayaona magumu lakini at least utajifariji kwamba unacho kitu umekiweka mahali.maisha yanatisha sana aisee vijana ambao hamjapitia magumu mengi ktk maisha yenu mnaopita ktk uzi huu someni between the lines kinachoandikwa humu maana sio masihara cos kama bro hapa alipoteza 4mill 2yrs nyuma akala msoto huo akitokea mmoja wetu akaipoteza kama hiyo Tanzania ya leo hakuna namna itamfanya asifungwe kamba au asipelekwe Mirembe.

Shida zisikie kwa mwenzako na hazizoeleki tuwe serious na maisha.

Mungu atusaidie
 
Binafsi tokea nikiwa secondary hasa advance kama sehemu ya kutimiza maagizo ya Kristo nilikuwa nikiwatembelea watu wenye uhitaji na walio ktk mazingira magumu hasa wagonjwa wasio na ndugu ama watu wa kuwasaidia nilikuwa nikiwanunulia mahitaji yao muhimu kadiri ya nilivyokuwa nikiguswa na hali ya muhusika na mfuko ulivyoruhusu...

Basi bhana Mungu akajalia nikapata chuo na nikaendeleza huduma nakumbuka trip ya kwanza ilikuwa xmass kama sio mwaka mpya tukaenda gereza la isanga pamoja na AY wengine 7... Baada ya hapo nikawa na ratiba ya kutembelea Hosp kama kawaida basi bwana ikafika hatua nikashawishika nimwombe Mungu anipe hela ili niweze kuwatimizia wale watu haja zao kwa kina zaidi nikampa Mungu ahadi kibao kuwa fedha hizo sitozitumia kwa maslai binafsi kwamba hata wenzangu wa chuo wanaokwama ningewagawia bure...

Mungu alivyomwema haikupita mwaka ghafla 4m na point hizi hapa mkononi hapo ilikuwa ni mwaka juzi basi nilifurahi kweli kweli na kama ilivyoasili yetu ya dhambi nikajikuta natanguliza watu watatu mbele I, Me and Myself yaan tu ghafla nikajawa na ubinafsi nikaanza kuwaza kununua kiwanja mawazo ya matumizi kwa ajili ya maskini yakawa yanaponijia najisemea haina shida hata nikinunua kiwanja nitakapojenga baadae si nitawasitiri ktk hiyo nyumba ama sometime naenda kuwatembelea ila kiasi cha msaada kinabaki kile kile cha zamani hizi nyingine nishazibinafsisha.... Basi kuna ndugu yangu nikampa wazo ili anisaidie ninunue kiwanja mjini ila nae akawa mzito nikampotezea nikaenda front mwenyewe nilipata eneo nzuguni ila wale watu walikuwa wapigaji nikawashtukia nikawaacha...

Roho ya ubinafsi na tamaa vikazidi kuniandama pesa ipo benki mara nafatilia niiweke kwenye fixed account ila jamaa mhudumu wa acb akanikatisha tamaa kuwa i rate ni ndogo sana mara nataka kwenda kilolo nikanunue mashamba ya miti mara hiki na kile... Basi shetani nae alivyomjanja wa kusoma udhaifu wetu tunapokuwa mbali na Mungu akaniletea jamaa yangu wa karibu ambae alikuwa na project iliyokuwa inahitaji kiwango zaidi kdgo cha fedha niliyokuwa nayo kwanza aliniita nitoke mkoani niende DSM ili nikaione project alidai hata nauli angerudisha kama nisingeipenda project....
Basi sababu hizi fedha niliziomba kwa Mungu ikanibidi nipeleke tena ombi la kuipeleka ile fedha ktk uwekezaji huo naoitiwa ili wigo uongezeke nisaidie zaidi ila awamu hii ilikuwa tofauti kwani akili yangu ilishajawa tamaa na nilishafanya maamuzi ya kupeleka hela hivyo nilikuwa nikiomba kama sehemu ya kutimiza wajibu tu yaan lile sio ombi ilikuwa taarifa...

Ee bwana we mwanaume nikaenda DSM project nikaipenda na nikakopa kama kilo naa nikajazia nikajoin kwa 4m+ kwa matarajio ya kupata utajiri wa chap kibaya sikupata hata nafasi ya kuomba ushauri jamaa alinizuia kijanja... Mwaka ule ule likizo nikaenda dsm kukomaa na project ila kiukweli matokeo hayakuwa kama nilivyoelezwa na hadi sana hamna return yoyote... Baadae niligundua kosa langu la ubinafsi na tamaa mbaya nikakiri na kumuomba mwenyewe msamaha na naamini alinisamehe sasa na Amani na kwa wakati wake atanipa nyingine...

Funzo: Ukimwekea Mungu ahadi usikawie kuitimiza, kazi ya Mungu hitaji lake la kwanza sio pesa ila ni "Mungu" maana kuna tofauti kati ya kufanya kazi ya Mungu na kufanya kazi na Mungu, Mungu yupo anasikia na anajibu kingine Amani na furaha ya kweli haitokani na ulichonacho mkononi ila moyoni hivyo ni muhimu sana to shape our attitude positively with total surrender to God tho ni ngumu kibinadamu ila kwa kumtegemea Mungu inawezekana...

[emoji28][emoji28][emoji28][emoji28]hio mipango yako ya kuwasaidia baada ya kupokea pesa imenifurahisha
 
[emoji28][emoji28][emoji28][emoji28]hio mipango yako ya kuwasaidia baada ya kupokea pesa imenifurahisha
Hahahahah binadamu tunakosea tuomba vitu badala ya kumtaka mwenye vitu ikiwa ningeomba uwepo wa Mungu ndani yangu pesa angenipatia kama ziada na ile huduma ingekwenda vzr kbs bila upungufu.

Tujifunze kuomba uwepo wa Mungu ndani yetu tuache kukimbizana kutaka baraka na suluhisho la shida zetu hayo mahitaji yetu anayajua na atatupatia tu ttzo letu hatuna imani tumejawa hofu na mashaka
 
2010s Rafiki ake na bamkubwa alipiga kama m20 hivi..
Jamaa alikula bata laana, kila akija home anakuja na Taxi yupo na mademu.
Alikua akitaka kwenda chooni anakodi gari ihampeleka Tanganyika Hotel..ipo kando ya ziwa Tanganyika.

Siku moja alikodi prado akaenda nalo kasulu akarudi nalo limechafuka akapita sokoni akanunua katon kadhaa za machupa ya maji. Akaenda na gari lake hadi forodhani ujiji akaita vijana waoshe gari lake wakaosha kwa maji ya ziwa, wakati wanataka kulisuza alikataaa kua maji ya ziwani hayana hadhi akatoa yale machupa kwenye buti ndio akasuzia..

December 2012 alikuja home kwenye sherehe..tukawa tunachuna nae mbuzi. Basi akaniambia father kwa jinsi nilivyopigika hata nikiletewa meli inauzwa shilingi 20 sina uwezo wa kuinunua. Jamaa siku hizi anaushi kama yahaya..ukisikia mdananda ndio yeye. Hana future kabisa

Sasa huyu ndio mshamba wa pesa na ilifaa afilisike kabisa
 
Hahahahah binadamu tunakosea tuomba vitu badala ya kumtaka mwenye vitu ikiwa ningeomba uwepo wa Mungu ndani yangu pesa angenipatia kama ziada na ile huduma ingekwenda vzr kbs bila upungufu. Tujifunze kuomba uwepo wa Mungu ndani yetu tuache kukimbizana kutaka baraka na suluhisho la shida zetu hayo mahitaji yetu anayajua na atatupatia tu ttzo letu hatuna imani tumejawa hofu na mashaka

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]hatari sana
 
Nakumbuka miaka hiyo nimemaliza advance najiandaa kwenda chuo kikuu, tukauza nyumba ya urithi ya mzee tukagawana mil50 kila mtu tulikua watatu.
Baada ya kuzipata zile milioni 50
Nilitafuta mjengo kabla sijaenda chuo Mwanza, baada ya kununua hiyo nyumba for approximately 25mil. Remaining balance nikaenda nayo chuo but kiukweli mpaka Leo huwa najiuliza ile pesa iliishaje? Note sikua mtu wa tungi sana wala totoz. But hela zilikuwa zinaisha tu bila kujielewa naweza kuwa na elfu 50 mfukoni nikienda kula hata lunch tu nikija kucheki kwenye wallet nina kama 20k tu.
But hela zilivyokaribia kukata ikabidi nimfuate bi. Mkubwa kuongea nae baada ya kutembea tembea kwa wataalam jibu tulilopewa ni kwamba kuna ndugu alinitupia chuma ulete ili pesa nisiifanyie jambo la maana ikawa inapotea katika mazingira ambayo wew hujitambui.
Nachoshukuru nilinunua nyumba otherwise ningekua sina pakukimbilia.
We nae msomi unaweza uchaqi
 
Back
Top Bottom