Tuliowahi kupata pesa na kufilisika/kufulia, tujikumbushe hapa

Tuliowahi kupata pesa na kufilisika/kufulia, tujikumbushe hapa

Ujue pesa ina shida fulani. Kama hujazoea kuimiliki, siku ukiipata ghafla lazima uchizike. Usipokuwa na adabu na pesa yako, itakutesa tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Si kweli mkuu, inategemeana na mtu.

Mimi nilikuwa sijawahi kumiliki hata laki, nikiwa nasoma srkondari, siku nikapata milioni 1.5 na bado nikaitumia vizuri tu bila mapepe. Nilikuwa nikipata mshahara wa laki 2.5 ndani ya miaka 2 nikawa napokea milioni 2.5, ongezeko la 1000% na sijabadilika sijui kwa kuchanganyikiwa.
 
Si kweli mkuu, inategemeana na mtu
Mimi nilikuwa sijawahi kumiliki hata laki, nikiwa nasoma srkondari, siku nikapata milioni 1.5 na bado nikaitumia vizuri tu bila mapepe
Nilikuwa nikipata mshahara wa laki 2.5 ndani ya miaka 2 nikawa napokea milioni 2.5, ongezeko la 1000% na sijabadilika sijui kwa kuchanganyikiwa
Duuuh, Kongole!
 
Hello wananzengo

Jamani jamani jamani, Niko serious, utani matusi na mizaha isiyokua na tija haitapokelewa.

Give me 3 million or 4 million na nakuahidi ntakachopata ambacho ni zaidi ya milioni 250, nitakupa milioni 50. Nina uhakika na nachoenda kufanya.

Guarantee tutaingia makubaliano kisheria kabisa, nina asset kama nyumba na kiwanja. This is serious. Wengi wana hela lakini hawajui wazifanyie nini ila wengine hatuna lakini nafasi kama hizi zinatujia kila uchwao.

When you are Man, you have to find money and more money, and more and more money, pssy, bia, starehe, zipo tu but ... MONEY, POWER. UJI ESTABLISH AS A MAN kwanza ndo mengine yafuate.

Mawasiliano zaidi yatafanyika pm.

Asante na karibu for serious minded.
 
Kati ya mwaka 2011-2015 nilikuwa ktk standard nzuri kiasi kimaisha, biashara nzuri, usafiri binafsi na viwanja 2 mjini, pesa ya kuzungukia mjini na mafuta haikuwa shida..ninapoandika comment hii kesho sifahamu nakula nini! Nimefilisika! Hakuna hata ndugu anaenipigia simu tena maana naonekana kituko. Wakuu tuombeane tu..kufilisika kuna maumivu ambayo si rahisi kuyaandika hapa.

Historia Yako Haina tofauti na yangu, tofauti ni kwamba wewe ulikuwa na viwanja viwili mie nilikuwa nacho kimoja ila hadi miaka ni Ile ile
 
Nina mjomba wangu mmoja hivi alikuwa anaimba imba kwenye hizi bendi za muziki kipindi hicho. Unawataja ma papaa, watu wazito alaf wanakutunza pesa ndefu. Sasa sijui alipigaje hela, ila alikuja kumiliki pesa ndefu. Mjini akawa yeye ndio Don, kila kona ana demu. Muda wote kachomekea, starehe mwanzo mwisho. Baada ya miezi kadhaa akafulia mbaya, hadi soo.

Akapotelea migodini. Huko alikaa kama miaka miwili au mitatu. Akapiga mshindo wa maana. Kurudi town ana hela chafu. Akiingia bar anatoa watu wote, anaikodi bar alaf anabaki na wapambe wake tu. Kuna siku mlevi mmoja wakati anatolewa nje kwavile bar imekodiwa na anko, yule mlevi alitukana. Anko akaomba aitiwe huyo aliyetukana. Kabla hata hajamwangalia usoni, akamuagiza mhudumu ampe yule mlevi kreti za bia sawa na urefu wake. Siku nyingine anaweza akatoa order kuwa wahudumu wote wa bar wabaki na pichu tu na sidiria. Haikupita miaka miwili akafulia mbaya.

Alivyofulia akapotea bila kujua kaenda wapi. Akaja kuibuka baada ya miaka kadhaa. Siku anakuja home kanawiri kichizi, akampa bi mkubwa (mama angu mimi) busness kadi yake ambayo inaonesha yeye ni engeneer na anamiliki kampuni ya ujenzi wa barabara (anko aliishia la saba) [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Sasa hivi ameshaoa na ana life zuri tu. Ukimpigia simu story zake ni either yupo njiani anaenda makao makuu Dodoma au yupo njiani anatoka kule. Ukimpigia simu asipopokea, badae akikuchek utaskia alikuwa kwenye kikao na Mama ndio maana hakupokea (hapo anamaanisha mama Salma Kikwete)

Mara ya mwisho kumpigia simu aliniambia "Ngoja naingia Usalama, ntakuchek badae, siunajua ofisi za watu hizi" [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Mungu akupe maisha marefu anko.
 
Back
Top Bottom