Binafsi tokea nikiwa secondary hasa advance kama sehemu ya kutimiza maagizo ya Kristo nilikuwa nikiwatembelea watu wenye uhitaji na walio ktk mazingira magumu hasa wagonjwa wasio na ndugu ama watu wa kuwasaidia nilikuwa nikiwanunulia mahitaji yao muhimu kadiri ya nilivyokuwa nikiguswa na hali ya muhusika na mfuko ulivyoruhusu...
Basi bhana Mungu akajalia nikapata chuo na nikaendeleza huduma nakumbuka trip ya kwanza ilikuwa xmass kama sio mwaka mpya tukaenda gereza la isanga pamoja na AY wengine 7... Baada ya hapo nikawa na ratiba ya kutembelea Hosp kama kawaida basi bwana ikafika hatua nikashawishika nimwombe Mungu anipe hela ili niweze kuwatimizia wale watu haja zao kwa kina zaidi nikampa Mungu ahadi kibao kuwa fedha hizo sitozitumia kwa maslai binafsi kwamba hata wenzangu wa chuo wanaokwama ningewagawia bure...
Mungu alivyomwema haikupita mwaka ghafla 4m na point hizi hapa mkononi hapo ilikuwa ni mwaka juzi basi nilifurahi kweli kweli na kama ilivyoasili yetu ya dhambi nikajikuta natanguliza watu watatu mbele I, Me and Myself yaan tu ghafla nikajawa na ubinafsi nikaanza kuwaza kununua kiwanja mawazo ya matumizi kwa ajili ya maskini yakawa yanaponijia najisemea haina shida hata nikinunua kiwanja nitakapojenga baadae si nitawasitiri ktk hiyo nyumba ama sometime naenda kuwatembelea ila kiasi cha msaada kinabaki kile kile cha zamani hizi nyingine nishazibinafsisha.... Basi kuna ndugu yangu nikampa wazo ili anisaidie ninunue kiwanja mjini ila nae akawa mzito nikampotezea nikaenda front mwenyewe nilipata eneo nzuguni ila wale watu walikuwa wapigaji nikawashtukia nikawaacha...
Roho ya ubinafsi na tamaa vikazidi kuniandama pesa ipo benki mara nafatilia niiweke kwenye fixed account ila jamaa mhudumu wa acb akanikatisha tamaa kuwa i rate ni ndogo sana mara nataka kwenda kilolo nikanunue mashamba ya miti mara hiki na kile... Basi shetani nae alivyomjanja wa kusoma udhaifu wetu tunapokuwa mbali na Mungu akaniletea jamaa yangu wa karibu ambae alikuwa na project iliyokuwa inahitaji kiwango zaidi kdgo cha fedha niliyokuwa nayo kwanza aliniita nitoke mkoani niende DSM ili nikaione project alidai hata nauli angerudisha kama nisingeipenda project....
Basi sababu hizi fedha niliziomba kwa Mungu ikanibidi nipeleke tena ombi la kuipeleka ile fedha ktk uwekezaji huo naoitiwa ili wigo uongezeke nisaidie zaidi ila awamu hii ilikuwa tofauti kwani akili yangu ilishajawa tamaa na nilishafanya maamuzi ya kupeleka hela hivyo nilikuwa nikiomba kama sehemu ya kutimiza wajibu tu yaan lile sio ombi ilikuwa taarifa...
Ee bwana we mwanaume nikaenda DSM project nikaipenda na nikakopa kama kilo naa nikajazia nikajoin kwa 4m+ kwa matarajio ya kupata utajiri wa chap kibaya sikupata hata nafasi ya kuomba ushauri jamaa alinizuia kijanja... Mwaka ule ule likizo nikaenda dsm kukomaa na project ila kiukweli matokeo hayakuwa kama nilivyoelezwa na hadi sana hamna return yoyote... Baadae niligundua kosa langu la ubinafsi na tamaa mbaya nikakiri na kumuomba mwenyewe msamaha na naamini alinisamehe sasa na Amani na kwa wakati wake atanipa nyingine...
Funzo: Ukimwekea Mungu ahadi usikawie kuitimiza, kazi ya Mungu hitaji lake la kwanza sio pesa ila ni "Mungu" maana kuna tofauti kati ya kufanya kazi ya Mungu na kufanya kazi na Mungu, Mungu yupo anasikia na anajibu kingine Amani na furaha ya kweli haitokani na ulichonacho mkononi ila moyoni hivyo ni muhimu sana to shape our attitude positively with total surrender to God tho ni ngumu kibinadamu ila kwa kumtegemea Mungu inawezekana...