Tuliowahi kupata pesa na kufilisika/kufulia, tujikumbushe hapa

Pole sana mkuu, hii thread yako inanikumbusha ndugu na jamaa waliofilisika, nami kupitia wao nimejifunza vitu vingi sana katika maisha, kwanza nnaamini hakuna ajuaye kesho yake, pili kufilisika haina kesho, tatu usijivune ukiwa navyo(usiwadharau wengine), nne kuwa na nidhamu ya pesa(kimatumizi), tano epuka kukopa kiwango kikubwa cha mkopo na pia usiwe mwepesi kukopesha na n.k
 
Kufilisika maumivu yake yasikie tu acha yakupite bila kukugusa, Eeh Mungu naomba sisi vijana tuepushe na kikombe hiki in case ikatokea mazingira hatarishi katika utafutaji wetu wa riziki maana kwanza kibongo bongo jamii itakuchukulia kama wewe ni fala flani hivi failure uliyekosea target ya kile kizuri ulichokuwa umekipanga na hali hii itazidi kukuchanganya kama hujaishia kuokota makopo sijui!!! Noma sana.
 
Pesa za kuhongwa zina mikosi, kama ilivyo za wizi
 
Usinikumbushe mkuu!!yaani mpaka ilipobaki 50,000 ndo nikashtuka kumbe zimeisha!!ATM mbaya sana!!ila Mungu anisamehe tu!
[emoji1] [emoji1] [emoji1] . Nilikuwa nakaanga mayai 10 kila siku.
Nikienda bar. Mbuzi choma ya 10,000.
Kuhonga sasa.kuvaa usiseme.
Mara ya mwisho Naenda ATM. Kuna 4,500..
Nilikuwa mdogo.ila HeLa za kukinga tu hazina Baraka
 
Sure, very true mkuu, bless up.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…