Tuliowahi kupata pesa na kufilisika/kufulia, tujikumbushe hapa

Tuliowahi kupata pesa na kufilisika/kufulia, tujikumbushe hapa

Du acheni kunikumbisha, nilikuwa nafanya kazi sehemu flani wafanyakazi wenzangu wakashawish kampuni iwe inatoa mkopo Mara pa ikakubaliwa na wenzangu walichukua mkopo mkubwa na Mimi nikachukua 8ml, do kwanza sijazigusa mwezi mzima najaza mipango kwenye makaratasi, usiku naamka napanga mipango, nikapata wazo nidroo pesa zote nikae nazo Ndani.

Nikadraw, siku moja kama demu wangu kaniambia mbona siku hizi unapiga mahesabu sana na makaratasi mengi mezani, nikamwambia hamna mipango tu, Mara akajua Nina pesa, akaja home sijui alinitime VIP akaiba zote, kuna machinga nilimuambia aniletee pas original asijal gharama, siku kaja nachek bahasha sioni pesa nampigia simu Selina hapatikani, nauliza nkaambiwa ameenda Morogoro, jamaa anasema pasi elfu 40, kaiacha hapo,
 
Vyote mkuu!

Ok chukua hiyooo
IMG_1296.jpg
 
hahahaaaa!! unaenda kutoa hela ATM hutaki hata risiti unaona utajipa presha tu
Ukiwa nazo za kukinga.

Rafiki yako mkubwa ATM. Ukiingia pale una bofya tu. Mpunga unatoka. Zingine mpyaaaa. Alafu zina ubaridi ubaridi wa air condition. Ngoja siku ziishe. ATM utaipitia kwa mbaaali. Uingie ukafanye nini?

Nimeyamiss haya maisha kwa kweli.
 
Niliwahi kuzichanga huko nyuma, nikafungua grocery! Kwa kuwa nami nilikuwa mwanachama, mwanzoni nilikuwa na wateja wazuri na waaminifu. Baada ya muda mikopo ikaanza. Mteja akikopa na deni likiwa kubwa, anahama kijiwe. Nakumbuka mara ya mwisho nilifungia crate tupu kwani hata chupa walishakopa zikiwa na pombe ndani. My Take: Biashara ya pombe kama na wewe mmiliki ni mnywaji, usinywee pale, ni hatari kwa usalama wa grocery yako.
Grocery ni kwaajili ya mbogamboga na matunda mkuu!!!!! Sasa hizo beer zimetoka wap au bar?
 
Acha kumkufuru Mungu hapo dukani kwako huingizi zaidi ya elfu 50 kwa week?

Hiyo Tecno umenunua zaidi ya 250k.... Haya bwana mangi
Hapana ninachaji simu. Naingiza wastan Wa buk 5 kwa siku. Nina familia inakula wastan Wa 3000 kwa siku piga hesabu ya 10 kwa wiki.

Tecno naziona kwa wateja
 
Ukiwa nazo za kukinga.
Rafiki yako mkubwa ATM. Ukiingia pale una bofya tu. Mpunga unatoka. Zingine mpyaaaa. Alafu zina ubaridi ubaridi wa air condition. Ngoja siku ziishe. ATM utaipitia kwa mbaaali. Uingie ukafanye nini.?
Nimeyamiss haya maisha kwa kweli.
yaaani mlemleeee!!! halafu unajifanya uko bize na miamalaaa, unapishana na wadosi kwenye ATM, ukikuta ATM haina salio unaanza kulalama kwamba wanazingua wanakuchelewesheni kwenye biashara!! kumbe unawahi baa[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]

zikiisha hautatamani hata kupasogelea!! unaona hadi vibinti vinaingia wewe salio linasoma tshs 1600.50/= ( maana yake haitoki) [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] halafu huna hata vocha.
 
Kila pesa ipitiayo mikononi mwako ina jini. Shetani hapendi watu wawe na maisha mazuri bali mabaya ili awatawale. Pesa yoyote halali yaweza kuwa mtaji wako haijalishi ni kiwango gani.

Biashara nyingi za kuonekana unapoifanya nyingi hufilisi watu wengi bali zinazoonekana za ovyo au za siri hutajirisha wengi. Mfano usindikaji wa mazao, kilimo, ununuzi wa hisa, ujenzi wa nyumba za biashara and others related to these.

Wengine wana mikosi ukidiriki kumwambia unachotaka kufanya basi katu hufanikiwi hivyo siri ya mipango yako ndiyo siri ya mafanikio.
 
Back
Top Bottom