Nimefuatilia post za wadau hapa kuna kitu kimoja nimekiona ambacho kwa nafasi kubwa ndicho kilichosababisha washindwe kuidhibiti shilingi iliyopita mikononi mwao,nacho ni kupenda kuiona cash,kwamba bank account yangu inasoma 12mill au 20mill basi hata nikenda nikatoa mill1 nikanunua hiki mtabaki na balance yakutosha na shida ya pesa ukiishakuwa nayo na ukawa na uhuru nayo inakuwa rahisi sana kuitumia,pia kushindwa kuiheshimu na kusahau tulipotoka.
Obviously wengi tumetoka ktk familia maskini hata kutoa toa msaada maana sio kila aliefilisika hela alihonga hapana mwingine ndugu alimfuata bwana nipe kiasi fulani cha pesa nitarudisha baada ya muda fulani then anazingua kumshtaki unashindwa inabidi ukubali.binafsi nimeshika hela nikiwa mdogo sana{masuala ya elimu tusiulizane wakuu}ila hela yangu ikikaa tu ndani sikuiweka bank nikiwa aged 21 nikanunua kiwanja kwa Tsh3,150,000/= nikiwa 23 nikanunua kingine kwa thamani zaidi ya hiyo kidogo nikiwa aged 25 nikaanza ujenzi.
Kwanini nilifanya hivi,sikutaka kukaa na hela inizoee na hata nikifuatwa na ndugu kukopa nilikuwa najifanya masikini wa mwisho sometimes huko kwenye kununua assets nilikuwa nabaki na deni ila sio kiasi kikubwa na hii imenijenga sana kuithamini shilingi.na tunapozungumzia asset hatuzungumzii kumiliki gari,kwa imani yangu asset nzuri kwa sisi ambao tunadunduliza dunduliza ni kile kitu ambacho hakitakufanya utoe hela yako nyengine mfukoni kukihudumia labda kukiboresha tu kwa manufaa yako ya muda mrefu.