Tuliowahi kupata pesa na kufilisika/kufulia, tujikumbushe hapa

Tuliowahi kupata pesa na kufilisika/kufulia, tujikumbushe hapa

aisee nakumbuka nipo mwaka wa pili chuo , maisha yakawa yamekaza sna kwa kwel nikaomba kamtaji nikafungua ki jisehem cha kuuzia spices sokon kama ka laki sita ivi yaan kila nikiwa na promis na demu nakula 50000 yaani kilikufa kibiashara hata hakikuchkua mda
 
aisee nakumbuka nipo mwaka wa pili chuo , maisha yakawa yamekaza sna kwa kwel nikaomba kamtaji nikafungua ki jisehem cha kuuzia spices sokon kama ka laki sita ivi yaan kila nikiwa na promis na demu nakula 50000 yaani kilikufa kibiashara hata hakikuchkua mda
Hahahaha hapo ndo ujue kichamganya mapenzi na kaZ
 
Namaliza chuo tu napta kazi. Inalipa mbaya nakodisha apartment. Nikifunga hesabu ya mwezi haina kwere nawatafuta washkaji tunasherehekea. Madem hawakauki kwangu full kujiachia ndani ya self contained. Luxury life. Sina saving. Siku nivofanyiwa auditing nakubaini madudu kazi ikaisha.

Nilipagawa nikarudi kwa baba na mama. Nikapatwa na maradhi ya watu wazima mapresha wakati niko kijana mbichii. Washkaji walinitenga. Mpaka leo sijapata kazi ya mana nahangaika kwa wahindi kazi mlima mshahara kichuguu. Nawazaga Sana'a.
 
Maumivu yanakuja wakati ambao unaona laki ni pesa nyingi sanaa kumbe, alaf wewe ulikua na milion 10 majuzi tu na leo umebakiwa na elf 30.
Hapo unajaribu kushusha hesabu ya matumizi lakini inagoma! Kuna kijasho flan chembambaaa huwa kinashuka usoni! Halafu kwa tabia mbaya ya "shida" ndipo inapojitokeza tena Ile ya muhimu sana!
 
Namaliza chuo tu napta kazi. Inalipa mbaya nakodisha apartment. Nikifunga hesabu ya mwezi haina kwere nawatafuta washkaji tunasherehekea. Madem hawakauki kwangu full kujiachia ndani ya self contained. Luxury life. Sina saving. Siku nivofanyiwa auditing nakubaini madudu kazi ikaisha. Nilipagawa nikarudi kwa baba na mama. Nikapatwa na maradhi ya watu wazima mapresha wakati niko kijana mbichii. Washkaji walinitenga. Mpaka leo sijapata kazi ya mana nahangaika kwa wahindi kazi mlima mshahara kichuguu. Nawazaga Sana'a.

Tena ukikaa vibaya hapo kwa wahindi watakuomba 0712 soon, maana wanapenda sana
 
Nimejifunza kitu hapa ili umiliki hella inatakiwa na karohoo mbaya kawepo halafu uwe mtu wa kulialia shida ili watu wasikufate kukukopa halafu kuepuka beer za round ni mbaya kuliko maelezo.

Yah mkuu, ndugu wengi wakishaona fulani ktk familia amepata mafanikio kidogo basi kama alikuwa na wazo lake faster analifufua hata kama hajawahi kujaribu hasara na faida zake so pesa zako wewe anaenda kuzifanyia majaribio akishindwa tu jua na wewe umeshindwa na kuwashtaki huwezi sasa hawa unawakataa kwamba hali yako ni mbaya,japo watakuchukia ila amini usiamini hata ukiwapa siku bahati mbaya mambo yako yakayumba wao ndio wa kwanza kukuponda.

Pombe nazo zinadanganya sana na ukisema usikae na wana watakuona huyu jamaa namna gani unaringa nini ila mie naona bora mtu kuacha tu.
 
Hichi ndo kilichosababisha mpaka leo ile 1,300,000 nikaipeleka kununua hisa mwezi wa saba.. Ungekuta ile hela imeshapotea mpaka sasa hivi.. Ni kitu pia nimejifunza.. Usikae na cash kabisa..

Ila na mimi nliwahi kupoteza kama 4,000,000 miaka 2 iliyopita.. Sitaki kukumbuka maana niliishiwa mpaka kula ilinishinda. Ilikuwa kuna wakati nashindia 1000 kwa siku. Asubuhi maandazi ya 500 mchana napitisha nakula mihogo ya 500 usiku imetoka.

Ndani ya miezi miwili nilichuja ilikuwa nikitembea barabarani gari kubwa ikipita napepesuka kabisa na kupulizwa na upepo tu. Acha kabisaaaa..

Huku kodi ya nyumba nadaiwa miezi mitatu sijalipa mwenyenyumba kila siku anakuja kunigongea asubuhi.. Acha kabisaa wandugu niliteseka mno na maisha karibu mwaka mzima.

Honestly ni kipindi ambacho kimebadilisha mwenendo wa maisha yangu. Nowadays najiona nimekuwa mtu mwenye roho mbaya sana na najiamini sana.. Mtu hata anililie shida wala sishituki maana shida nliyopitia si mchezo yani
 
Back
Top Bottom