Tuliowahi kupata pesa na kufilisika/kufulia, tujikumbushe hapa

Tuliowahi kupata pesa na kufilisika/kufulia, tujikumbushe hapa

Miaka 3 iliyopita nililima eka 40 za mpunga na 30 za mahindi nilipokuja kuuza mazao niliingiza faida ya mil 55 ukitoa na pesa ya mtaji.

Leo tar 1 nina laki moja tu, wanawake sio viumbe vya mchezo na kazi nimefukuzwa niliowasaidia wamenitupa. Nimejifunza mistake zote nilizofanya ila nikikumbuka naumia mno..kwa vile nina nguvu sina ulemavu naendelea kupambana.

Nimerudi home kwa wazazi maana hali ni tete ninaweza kuwa tahaira
 
Miaka 3 iliyopita nililima eka 40 za mpunga na 30 za mahindi nilipokuja kuuza mazao niliingiza faida ya mil 55 ukitoa na pesa ya mtaji.
Leo tar 1 nina laki moja tu..wanawake sio viumbe vya mchezo na kazi nimefukuzwa..niliowasaidia wamenitupa.
Nimejifunza mistake zote nilizofanya ila nikikumbuka naumia mno..kwa vile nina nguvu sina ulemavu naendelea kupambana.
Nimerudi home kwa wazazi maana hali ni tete ninaweza kuwa tahaira
Pole mkuu
 
Wengi wa watu walipitia mafanikio makubwa sana na tunajuta...Anasa na starehe nzuri ni zile unakula na familia ukubwani maana hapo ndipo umuhimu wa pesa na uhitaji wa pesa unapoonekana...vijana hakikisheni mnaweka pesa zenu kwenye Asset na sio Liabilities....nunua viwanja kadri uwezavyo...wekeza kwenye mashamba hata kama ulimi sasa hivi... kula bata kwa akili sio kwa sifa ili watu wakuone...wanaokusifia sasa ukifilisika haohao wanakucheka na kukudharau.
Bora utajiri wa kuwekeza kuliko utajiri wa pesa,maana zikianza kupukutika utasema umerogwa
 
Kati ya watu usiotakiwa waamini na kuwasaidia, ni watu wanaokuwa karibu na wewe ukiwa na hela. Siku zikiisha watakusema na kukuona haufai.

Sidhani nitakuja saidia mtu maana wengi wao wanakugeuka na kukusema vibaya mambo yakienda ndivyo sivyo. Bora hiyo hela ukaipeleke kanisani kuliko kumpa ndugu mnafiki pale ukifuli

Hao unaocheka nao na kula nao raha ndio watakucheka baadae....
 
Miaka 3 iliyopita nililima eka 40 za mpunga na 30 za mahindi nilipokuja kuuza mazao niliingiza faida ya mil 55 ukitoa na pesa ya mtaji.
Leo tar 1 nina laki moja tu..wanawake sio viumbe vya mchezo na kazi nimefukuzwa..niliowasaidia wamenitupa.
Nimejifunza mistake zote nilizofanya ila nikikumbuka naumia mno..kwa vile nina nguvu sina ulemavu naendelea kupambana.
Nimerudi home kwa wazazi maana hali ni tete ninaweza kuwa tahaira
Pole sana mkuu,mimi mpaka leo sina rafiki hapa napofanyia kazi zangu maana nipo mbal na Nyumbani,urafiki na kazi yangu siutaki kabisa,kampani za kwenda kuzungusha bia baa siutaki,maana nashukuru nami si mtumiaji wa kilevi, nahitaji urafiki wa kimaslahi na siyo wa kinafiki, japo marafiki wa ukwel hawakosekani ila ni wawili tu na wapo mbali, nikiwa na shida tunasaidiana pamoja na huo umbali
 
Kati ya watu usiotakiwa waamini na kuwasaidia, ni watu wanaokuwa karibu na wewe ukiwa na hela....
Siku zikiisha watakusema na kukuona haufai.....
Sidhani nitakuja saidia mtu maana wengi wao wanakugeuka na kukusema vibaya mambo yakienda ndivyo sivyo....
Bora hiyo hela ukaipeleke kanisani kuliko kumpa ndugu mnafiki pale ukifuli

Hao unaocheka nao na kula nao raha ndio watakucheka baadae....
Sure mkuu.... balaaa sana unaowasaidia wanageuka maadui kabisa...
 
Nimesoma michango ya watu huku nikajifariji kidogo kuwa sikuwa nyang'au mwenyewe...nilikuwa na raman yangu ya utalii Arusha kila kwa siku nikipiga dili haramu sikosi chini ya $500 nikageuka papaa na wapambe kibao na demu matata kwenda moshi ni tax au Karatu tunachukua Noah private ...siku za game za UEFA kinywaji ni Heineken kwa yeyote atakayejipendekeza ...siku za kawaida ni Jack Daniels home kwa maza sifiki ....namnyamazisha na kumwekea pesa pesa bank ...kitu mwanamke alinifanya sitakaa nisahau baada ya kuishiwa..alichukua kila kitu cha ndani na polisi akanipeleka ...kutoka kwenye JD nikarudi kwenye viroba.

Uzuri nilikuwa nashamba kubwa nikauza nikajirudisha kwenye raman japo mapicha picha kibao ya maden kwenye bar nilizokuwa na sign bill ..pesa ukiwa nayo na mwanamke na marafiki wa mteremko ni shida kubwa....nshawah tumia 1 m bar kwa siku moja na dem anachekelea tu.
 
Nimesoma michango ya watu huku nikajifariji kidogo kuwa sikuwa nyang'au mwenyewe...nilikuwa na raman yangu ya utalii Arusha kila kwa siku nikipiga dili haramu sikosi chini ya $500 nikageuka papaa na wapambe kibao na demu matata kwenda moshi ni tax au Karatu tunachukua Noah private ...siku za game za UEFA kinywaji ni Heineken kwa yeyote atakayejipendekeza ...siku za kawaida ni Jack Daniels home kwa maza sifiki ....namnyamazisha na kumwekea pesa pesa bank ...kitu mwanamke alinifanya sitakaa nisahau baada ya kuishiwa..alichukua kila kitu cha ndani na polisi akanipeleka ...kutoka kwenye JD nikarudi kwenye viroba..uzur nilikuwa nashamba kubwa nikauza nikajirudisha kwenye raman japo mapicha picha kibao ya maden kwenye bar nilizokuwa na sign bill ..pesa ukiwa nayo na mwanamke na marafiki wa mteremko ni shida kubwa....nshawah tumia 1 m bar kwa siku moja na dem anachekelea tu.
duuh pole mkuu
 
Yah mkuu,ndugu wengi wakishaona fulani ktk familia amepata mafanikio kidogo basi kama alikuwa na wazo lake faster analifufua hata kama hajawahi kujaribu hasara na faida zake so pesa zako wewe anaenda kuzifanyia majaribio
akishindwa tu jua na wewe umeshindwa na kuwashtaki huwezi sasa hawa unawakataa kwamba hali yako ni mbaya,japo watakuchukia ila amini usiamini hata ukiwapa siku bahati mbaya mambo yako yakayumba wao ndio wa kwanza kukuponda.pombe nazo zinadanganya sana na ukisema usikae na wana watakuona huyu jamaa namna gani unaringa nini ila mie naona bora mtu kuacha tu.
Hapo kwenye ndugu mkuu pagumu kweli kitanzania, sijui mtu unajitoa vipi maana ndugu wengine ni wale wakaribu kabisa.
 
Miaka 3 iliyopita nililima eka 40 za mpunga na 30 za mahindi nilipokuja kuuza mazao niliingiza faida ya mil 55 ukitoa na pesa ya mtaji.
Leo tar 1 nina laki moja tu..wanawake sio viumbe vya mchezo na kazi nimefukuzwa..niliowasaidia wamenitupa.
Nimejifunza mistake zote nilizofanya ila nikikumbuka naumia mno..kwa vile nina nguvu sina ulemavu naendelea kupambana.
Nimerudi home kwa wazazi maana hali ni tete ninaweza kuwa tahaira
Mkuu naamini ukirudi kwenye kilimo utafanikiwa tena, jipange upya, mara nyingine hizo ni blessings in disguise.
 
Hapo kwenye ndugu mkuu pagumu kweli kitanzania, sijui mtu unajitoa vipi maana ndugu wengine ni wale wakaribu kabisa.
Inabidi tu mkuu maana maisha ni yako,ukiwa mchanga kwenye kutafuta hela ogopa sana ndugu.ndugu wanaweza kukufilisi kisha hao hao wakakucheka ila kama umeshajijenga vya kutosha unaweza kutoa msaada ili kuondoa lawama ila mtaji wako wa mill15 au 20 uanze kusaidia watu nakwambia utageuka kituko.
 
mimi ndo ngedere kabisa nilifanya kazi kwenye kampuni ya gas ndan ya miaka mi3 nilipata kama milion 10 nikanunua pikipki yakutembelea nikawa kazi yangu kuwafata mademu na kwenda kula bata beach demu nikimpata mtandaon hata awe anakaa kibaha namfata na pikipiki kiukwel sikuamin kama ile hela ingekuja kuisha nilikuwa naiona nyingisana kumbuka mii nmetokea familia ya kimasikin iv nnavyoandika hapa nmerud naish hom kwa baba na mama sina hata mia mfukon
Kama nakufahamu hiv ,,si ulikuwa ukikuta malaya wa concord kwa anayekujua unamgawia elfu 10-20 ..ulikuwa unajiita jina flan hiv la dawa hedex kama sijakosea? Bora zilikuwa zako mana nilisikia ulifungwa kwa kuiba hela za ofis kumbe zilikuwa n zako na pikpik yako ilikuwa boxer nyeusi ,, mrefu ,mweusi mwembamba kiasi ,mkimya sana ! Tuanzie hapa nikukumbushe vingine
 
Ha ha ha,nilikua na kikazi kimoja kila siku hela ya maji ya kunywa 100,000 na kuendelea,
nakumbuka nimekula ulabu toka 2000-2010 non stop daily,

kweli pombe sio chai jameni,acheni nilime haya majaruba tu

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Hujawahi kufilisika mkuu.wewe uliingia hasara.ingekuwa umepoteza mtaji wa milioni 100 sawa.hizo za milioni 2,3 mpaka 10 tumeshapoteza wengi sana ni hela ya kawaida kuingia loss kwa sisi watafutaji.ikitokea unasikitika kidogo,unajitathmini wapi ulipokosea,unajipanga unarudi vitani.
Umenipa courage, sifikirii tena mpunga niliopoteza,kila cha moto nakiona
 
Namaliza chuo tu napta kazi. Inalipa mbaya nakodisha apartment. Nikifunga hesabu ya mwezi haina kwere nawatafuta washkaji tunasherehekea. Madem hawakauki kwangu full kujiachia ndani ya self contained. Luxury life. Sina saving. Siku nivofanyiwa auditing nakubaini madudu kazi ikaisha. Nilipagawa nikarudi kwa baba na mama. Nikapatwa na maradhi ya watu wazima mapresha wakati niko kijana mbichii. Washkaji walinitenga. Mpaka leo sijapata kazi ya mana nahangaika kwa wahindi kazi mlima mshahara kichuguu. Nawazaga Sana'a.
Pole sana
 
Back
Top Bottom