Tuliowahi kupata pesa na kufilisika/kufulia, tujikumbushe hapa

Tuliowahi kupata pesa na kufilisika/kufulia, tujikumbushe hapa

Miaka 3 iliyopita nililima eka 40 za mpunga na 30 za mahindi nilipokuja kuuza mazao niliingiza faida ya mil 55 ukitoa na pesa ya mtaji.
Leo tar 1 nina laki moja tu..wanawake sio viumbe vya mchezo na kazi nimefukuzwa..niliowasaidia wamenitupa.
Nimejifunza mistake zote nilizofanya ila nikikumbuka naumia mno..kwa vile nina nguvu sina ulemavu naendelea kupambana.
Nimerudi home kwa wazazi maana hali ni tete ninaweza kuwa tahaira
Pole sana mkuu kama nikweli ila afadhali umezibujua ukifurahia kipindi hicho ila kuna zile zinakata tuuu na hujazifaidi kabisa inauma sana
 
Umenipa courage, sifikirii tena mpunga niliopoteza,kila cha moto nakiona
Mkuy pambana,hela iliyopotea hata ukiifikiria hairudi.Mi ningekuwa na roho nyepesi ningeshawehuka kitambo.tena bora wale waliofilisika kwa kuzitumbua atleast watasema walikula bata.mie hasara zote nimezipata kwenye biashara,lakini kukata tamaa kwangu ni mwiko.alimradi unapumua,hutakiwi kukata tamaa wala kusononeka.

Komaa, kaza mpaka kieleweke.
 
Kama nakufahamu hiv ,,si ulikuwa ukikuta malaya wa concord kwa anayekujua unamgawia elfu 10-20 ..ulikuwa unajiita jina flan hiv la dawa hedex kama sijakosea? Bora zilikuwa zako mana nilisikia ulifungwa kwa kuiba hela za ofis kumbe zilikuwa n zako na pikpik yako ilikuwa boxer nyeusi ,, mrefu ,mweusi mwembamba kiasi ,mkimya sana ! Tuanzie hapa nikukumbushe vingine
ohooo
 
Kuna jamaa yangu mmoja alikuwaga anafanya kazi sheli fulani kitengo cha stoo ye ndo anajua yameingia mafuta kias gani na yametoka kiasi gani jamaa alipoizoea kazi akaanza kupiga cha juu yeye na jamaaa zake wawili Sababu Ile sheli ilikuwa inahumia magari ya serikali na viwanda vikubwa akawa anakula njama na madereva wanapiga cha juu enzi za jakaya.

Maisha yakaendelea jamaa na wale wenzake maisha yakawa bomba wakajenga majumba mjini sehemu t ofauti ila nyumba walizokuwa wanakaa wakajenga sehemu moja majumba ya ukweli kwa mtu asiyefahamu kazi Yao ungedhani wanapiga kazi migodini au wafanyabiashara wakubwa au watu wenye nyadhifa kubwa serikalini wakafungua biashara mbali mbali kweli wakawa H abari ya mjini kutokana na jinsi walivyodesign zile nyumba zao na wakajenga sehemu moja .

Kilichowaroga wakanunua magari ya kifahari wakawa wanaibuka nayo kazi mmoja Lexus ,mmoja x3,mwingine prado tx wakawa wanaenda nayo kazini kwenye shell ya muhind hicho ndo kiliibua maswal mfanyakazi anayelipwa 120000 kwa mwez anawezaje kumiliki magari ya kifahari namna hiyo within two years ndo uchunguzi ukafanyika wa kimya kimya wakagundua njama zao ndo wakafukuzwa kazi walifunguliwa mashtaka ya wizi wakawa wameshinda mahakamani maana washitaki walikosa vielelezo vya ushahidi wa waliiba Wapi basi kesi ikaisha muhindi aliwaambia kitu kimoja akawabembeleza Mara kwa Mara kwamba wauze zile Mali wamrudishie ela yake hata nusu lasivyo watahangaika mpaka mwisho wa maisha Yao jamaa wakaona muhindi anatania.

Maisha yakaendelea miezi ikasonga walianzaga kufilisika biashara haziendi vitu vya kule nje majumba wakaanza kuuza hadi magari life likawa gumu wote wakabaki na Yale majumba.

Alianza mmoja akauza akakimbilia visiwani na familia yake mwingine naye akafata akamuuzia mnunuzi aliyenunua Ile ya awali ilikuwa kampuni ya wazungu akabaki jamaa yangu uyo akawa mgumu kuuza nyumba make angehangaika plan yake ilikuwa abaki na nyumba aje aiombee mkopo au akipata mtu mwenye ela nzuri ndo auze ajenge nyumba ya kawaida kama m30 hivi apo ashapigika watoto alikuwa amewapeleka medium school kawahamishia kwa gvt Kula anagongea kwa ndugu na jamaa .

Wakati anawaza hivyo ndo tetemeko la ardhi likapitia nyumba yake ikaharibika vibaya sana haikuwepo namna z aidi ya kubomoa akajenga upya ndo jamaa akawa ameishia apo alikimbia mji sijui yuko Wapi.

Wito:wizi sio mzuri hasa kiwaibia hawa wahindi
 
Mwanzoni mwa mwaka huu niliwekeza kwenye Bitcoin,nikanunua Bitcoin za jumla ya sh 1.3 milion.

Ile sijakaa vizuri,Hela hazitoki tena kwenye account. Siwezi kuwithdraw.
Sijakaa vizuri, Ile website niliyokuwa natrade nayo Ikafungwa ikawa haipo online.

Nimejiapiza siwezi kufanya biashara za mitandaoni za kipuuzi tena.
 
Kuna babu yangu wa ukoo mwezi wa Sita aliingizwa mjini na vijana wa kongo wakamuuzia dhahabu feki.

Ni daktar msitaafu alikuwa anamiliki dispensary na baa siku vijana walimuibikia kwamba wana dhahabu ya mil 50 ila yeye akiuza atapata mil 400 mzee akashawishika na akajihakikishia kwamba ni dhahabu kweli akaenda bank akachukua balance ya account yake akachukua pesa za baa na za hospital akaongezea akanunua dhahabu akauchuna mambo yote haya aliyafanya kwa siri akumshirikisha .

Siku za wafanyakazi kidai mishahara zikafika madawa na vifaa hospital na watu wa kodi wakaanza mambo Yao kila anakoomba mkopo amalizane na ayo madai holaaa ndo ukabidi amwambie mdogo wake aliyekuwa anamwamini maana watoto wake wengi kila mtu kakaa kijambazi ndo akamwambia m hapa nina dhahabu tafuta mteja tuuze tumalize hii ishu mteja kupatikana kumbe dhahabu feki asee mzee alipandisha presha ghafla akafariki usiku uo akafa kwa aibu ya Tamaa na kuingizwa mjini na usomi wake pia akaiacha family na madeni
 
Kuna jamaa yangu mmoja alikuwaga anafanya kazi sheli fulani kitengo cha stoo ye ndo anajua yameingia mafuta kias gani na yametoka kiasi gani jamaa alipoizoea kazi akaanza kupiga cha juu yeye na jamaaa zake wawili Sababu Ile sheli ilikuwa inahumia magari ya serikali na viwanda vikubwa akawa anakula njama na madereva wanapiga cha juu enzi za jakaya.

Maisha yakaendelea jamaa na wale wenzake maisha yakawa bomba wakajenga majumba mjini sehemu t ofauti ila nyumba walizokuwa wanakaa wakajenga sehemu moja majumba ya ukweli kwa mtu asiyefahamu kazi Yao ungedhani wanapiga kazi migodini au wafanyabiashara wakubwa au watu wenye nyadhifa kubwa serikalini wakafungua biashara mbali mbali kweli wakawa H abari ya mjini kutokana na jinsi walivyodesign zile nyumba zao na wakajenga sehemu moja .

Kilichowaroga wakanunua magari ya kifahari wakawa wanaibuka nayo kazi mmoja Lexus ,mmoja x3,mwingine prado tx wakawa wanaenda nayo kazini kwenye shell ya muhind hicho ndo kiliibua maswal mfanyakazi anayelipwa 120000 kwa mwez anawezaje kumiliki magari ya kifahari namna hiyo within two years ndo uchunguzi ukafanyika wa kimya kimya wakagundua njama zao ndo wakafukuzwa kazi walifunguliwa mashtaka ya wizi wakawa wameshinda mahakamani maana washitaki walikosa vielelezo vya ushahidi wa waliiba Wapi basi kesi ikaisha muhindi aliwaambia kitu kimoja akawabembeleza Mara kwa Mara kwamba wauze zile Mali wamrudishie ela yake hata nusu lasivyo watahangaika mpaka mwisho wa maisha Yao jamaa wakaona muhindi anatania.

Maisha yakaendelea miezi ikasonga walianzaga kufilisika biashara haziendi vitu vya kule nje majumba wakaanza kuuza hadi magari life likawa gumu wote wakabaki na Yale majumba.

Alianza mmoja akauza akakimbilia visiwani na familia yake mwingine naye akafata akamuuzia mnunuzi aliyenunua Ile ya awali ilikuwa kampuni ya wazungu akabaki jamaa yangu uyo akawa mgumu kuuza nyumba make angehangaika plan yake ilikuwa abaki na nyumba aje aiombee mkopo au akipata mtu mwenye ela nzuri ndo auze ajenge nyumba ya kawaida kama m30 hivi apo ashapigika watoto alikuwa amewapeleka medium school kawahamishia kwa gvt Kula anagongea kwa ndugu na jamaa .

Wakati anawaza hivyo ndo tetemeko la ardhi likapitia nyumba yake ikaharibika vibaya sana haikuwepo namna z aidi ya kubomoa akajenga upya ndo jamaa akawa ameishia apo alikimbia mji sijui yuko Wapi.

Wito:wizi sio mzuri hasa kiwaibia hawa wahindi
Mkuu si kuibia wahindi tu, kwa ujumla mali ya wizi haidumu, ni kama nguo ya kuazima itabaki kuwa sio yako hata ikikupendeza namna gani.
 
Duh,sikuwah kupewa hela,sikuwah kuomba mtaji ila nilipiga kbarua nikapata 8000 (elfu nane) nikaanza biashara ya kamba za simu,nikauza kila siku napata faida 4000 -5000 nikameki mpk ikafika laki na nusu,nikaanza kununua na housing za simu,biashara ikanenepa mpk kufika laki tano,nikafungua kibanda cha mbao,nikaendelea kdgo kdgo nikapata compiter nikaanza kuweka mziki, nikakomaa kama mwaka hiv,kipimd kile kuweka mziki mmoja jero bas kwa siku napata 20k ikipungua snaa 15k,nikaanza kuweka simu moja moja huko nje ya mji,nikauza kama sina akil nzur,nikafukisha mtaji wa milion 4,kiukwel nikaingia kwenye frem,we bwana wee wacha nikomae muuza simu maaruf,nikakomaa nikawa na nyumba na kagar vitz,CHA kunisogeza mjini,nikakomaa hvyo hvyo kuja kutamalaki nina zaid ya milion 20,nikaanza kukopesha watu kwa riba,unakuja na gari na kadi nakupa hela,aisee nikapiga mihela kila siku na maisha yakawa safiii.

Balaaa lilipoanzia...
Nikapata mchongo wa madin kule tanga sehem za kigongoi na kigwase,sina uzoef,siyajui madin wala sijui soko,hapa ndo penye tatizo kwa weng,naletewa madin hata kuyakagua sijui halaf naemtegemea kumbe nae hajui tunanunua mabov tu,najua tunaenda kupata hela town kumbe naenda kuumizwa,sikukata tamaa,nikafanya tena na tena lakin wap,mwsho nikakuta nimepoteza karib milion 17 bila faida,nikaona isiwe tabu,nikaanza kuchimbisha watu mm mfadhili,nikapiga piga hela ikakata,nikaangalia nyuma na kuangalia nilipo anguka nikajua ni uzoefu na utaalam wa madin sina,nikaendelea kukomaa nikauza gar,kupeleka hela mgodin holaaa,duka nimefunga,mtaji umekata,na sina mbele wala nyuma...

Mm mwanaume nilianza sifir nikapata hela sasa nikaenda kwa wakwe zangu nikawaomba nimwache mke pale miez sita kuna mahali nahitajika,kosa waliloffanya ni kukubali,bas baada ya kumwamishia mke pale na mtoto nikaondoka nikaipiga nyumba bei,nikauza kila kitu bila mke kujua,nikapata kama 22m maana niliiuza sbu ya uharaka nyumba yenye thaman zaid ya 40ml. Nikasepa zang mgodini,asee yaliyonikuta nikachanganyikiwa zaid,nikaitumbukiza hela na haikurud hata mia zaid ya maden,nikabakiwa mikono mitupu,nyumba,duka,gar,mke sina kwa kipind hcho japo mke najua nikirud ntampata. Nikamtapele jamaa mmoja laki na nusu nikakimbilia mbinga songea kulima mahind vibarua maana naona aibu ya kurud,nikapiga msimu wa kwanza nalala kwa mshakaji wng kimya kimya dunia haijui nilipo,nikaomba nami heka moja nilime mazao yangu,nikakomaa haswa asee duuuh achen asee maisha haya,bas nikapata gunia tisa nikazilipua fasta gunia moja 20k nikasepa zangu tabora,maana nina ifaham kwa kias,nikapata dili la asali,watu wana asali pa kuiuza kwa dar hawapajui nikaona fursa hii,nikawaambia mm ninamteja dar twenden,tukaja mpka dar[emoji3] [emoji3]

nilipo fufukia
Nikawapeleka kwa mshakji wakauza asali ya milio 9 kama sikosei,wakakosea wakanipa laki tano,nikawaambia kaleten nyingine najua pa kuuza bei kubwa zaid,wakaenda huko wakakusanyaaaa za nyuki wa kubwa na wadogo,kuleta mzigo nam nilikua nimepata jamaa muhindi anainunua,bas kushusha tu mzigo hela hizo,genji yangu na ujanja nikapata 2ml. Nikasema nipange chumba kulala kwa washkaji nimechoka,nikapanga chumba tabata liwit uswahilin,kila wakileta mzigo dar mm ndo mjanja wao napata laki tano mok milion,muda wote mke hajui nilipo wala namba zang hana na niliamua makusud kukaa hvyo,baada ya miaka mitatu ya asali nikajikuta nina zaid ya milion 4,nikaanza tena kurudia biashara yang ya zaman japo nilikua na mtaji lakin soko lilikua shida,nikaona niwe mbunifu zaid,nikakomaa na biashara ya kutembeza mpka nikafungua tena frem,bas bhna mungu akivyo wa ajab,naletewa simu za ishu kutoka nairob nauza jumla jumla siku mbili sina kitu,biashara ikarud kwenye mstari,nikanunua sehem kule pugu shule ya sekondar nikaanza kuinua kdgo kdgo,mpk nilipohakikisha nimepauwa ndo nikarud kumsalimia mke na mtoto,zaid ya miaka mitatu nilivyokua mkimbiz ndan ya nchi yngu. Kiukwel leo naweza kwenda popote,muda wwte,naweza kula cchte,naweza nunua ving ambavyo watu wanataman kua navyo,wala sitok jasho,nilale,niamke hela napata tu,japo uchum umebadilika lakin siwez kushindwa kuyamudu maisha kwa hali yyte kwa sasa,na mwaka jana nilitaka kujenga shule ya awali mpk sekondar sema kuna ukiritimba flan nikakutana nao nikaghairi. So anaefilisika usimcheke hata siku moja maana anauwezo wa kurud barabarani na akafanikiwa zaid.
 
hahahaaa!! zungushaaaa, wape bia haoooo!!! wanywe mpaka waombe poa!! kampuni kubwa hiiiiiiii!!!, bill inakuja 70,000/= mfukoni una 50,000/= unachukua pikipiki fasta huku wadau unawaacha wanakula mvinyo, unaenda kuvuta 200,000/= ili imalize kila kitu[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] mnahama viwanja huku group linakufuata nyuma kila MTU na bebi wake unawanywesha wewe!!!
Saguda Umenichekesha sana hiki ulichokisema kimenikuta Mwezi wa 10 hapo Kahama nilifikisha Duara nilikuwa nakula si chini ya Laki nne na kuendelea kila siku...ninavyoongea hapa nimelala mchana huu naangalia Tv mambo yamegeuka...
 
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] pole comrade, haya ndo maisha buannna!!! VP lakini huko kahama mambo yakoje?
 
Back
Top Bottom