Tuliowahi kupata pesa na kufilisika/kufulia, tujikumbushe hapa

Tuliowahi kupata pesa na kufilisika/kufulia, tujikumbushe hapa

Namaliza chuo tu napta kazi. Inalipa mbaya nakodisha apartment. Nikifunga hesabu ya mwezi haina kwere nawatafuta washkaji tunasherehekea. Madem hawakauki kwangu full kujiachia ndani ya self contained. Luxury life. Sina saving. Siku nivofanyiwa auditing nakubaini madudu kazi ikaisha. Nilipagawa nikarudi kwa baba na mama. Nikapatwa na maradhi ya watu wazima mapresha wakati niko kijana mbichii. Washkaji walinitenga. Mpaka leo sijapata kazi ya mana nahangaika kwa wahindi kazi mlima mshahara kichuguu. Nawazaga Sana'a.

Hivi ni nini ambacho huwa kinafanya mtu akishuka kimaisha watu wamkimbie? Hata uliowasaidia watakuteta hadi ukome.... tena wanakusimanga na kukutangaza jinsi gani we ni fala na hata mambo mengine mengi utasingiziwa
 
Pole sana kaka,huwa tunajifunza tunapoanguka japo kwa maumivu makali sana,hela yako yoyote iweke sehemu ambayo ukiitaka lazima ikupe ugumu wa kuichukua ila ukiiweka sijui bank huku ukitembea na ATM Card mfukoni jua hiyo siyo yako.

Pia usimkopeshe mtu hata kama ndugu pesa yako iweke kwenye assets japo ukiwa na shida maisha utayaona magumu lakini at least utajifariji kwamba unacho kitu umekiweka mahali.maisha yanatisha sana aisee vijana ambao hamjapitia magumu mengi ktk maisha yenu mnaopita ktk uzi huu someni between the lines kinachoandikwa humu maana sio masihara cos kama bro hapa alipoteza 4mill 2yrs nyuma akala msoto huo akitokea mmoja wetu akaipoteza kama hiyo Tanzania ya leo hakuna namna itamfanya asifungwe kamba au asipelekwe Mirembe.

Shida zisikie kwa mwenzako na hazizoeleki tuwe serious na maisha.
 
Hivi ni nini ambacho huwa kinafanya mtu akishuka kimaisha watu wamkimbie? Hata uliowasaidia watakuteta hadi ukome.... tena wanakusimanga na kukutangaza jinsi gani we ni fala na hata mambo mengine mengi utasingiziwa
Jamii yetu inamchukulia mtu kwa kitu...i mean ukiwa nacho chakuweza kusaidia mawili matatu ktk jamii unayoishi basi wewe ni mzuri sana kwao,ila inapotokea kwa bahati mbaya kimekuondoka wanakukimbia wanakuona mzigo kumbe ingefaa wawe karibu na wewe zaidi ili hata angalao uweze kupata idea nyengine kupitia wao maana wanapokukimbia wanakuacha ukiwa frustrated...

Kwamba fulani alikuwa hivi leo yuko vile na mie niko hivi sasa wanapoanza kukupiga chenga na wewe unaingia hali ya uwoga hata ukiwa na idea yako kichwani ambayo ingeweza kukusaidia kupanda tena unashindwa kwenda kumshirikisha mtu sahihi unabaki unaumia moyoni na kwenda kwa watu ambao sio sahihi kwa lile ulilokuwa nalo mwisho una-fail tena ndiyo maana badhi ya watu wakipta mafanikio kwa mara ya pili utawaona ni kama wanyama lakini sivyo huwa wanaogopa ile hali ya mwanzo isiwakute tena.
 
Million 4 nazo ni pesa za kusimulia watu?
Mkuu,usidharau wanachomilik wenzio,siku ukikwama maishani ndiyo utajua milion 4 ni pesa za kusimulia Watu,usiwe mwepes kujivuna haujui kesho yako, kuna Watu wanamiliki mamilion ya pesa lakini ana shida na anaishi kwa stress kuliko huyo anayemilik hiyo milion 4, kuna Watu nimeishi nao walikuwa wana dharau kama wewe maana walikuwa na pesa hatari lakini hivi sasa ni aibu hata kusimulia, kwa hiyo jifunze kuheshimu cha Mtu hata kama ni kidogo kwako, kwake ni kikubwa tena mno
 
Kweli mkuu,binafsi hii thread nimeipenda na katika usomaji wa michango ya wadau nasoma bila kuacha kitu,inanipa somo kubwa katika maisha ya utafutaji japo najua ila nahitaji kujua zaidi wapi? tunapokosea
 
Hapana ninachaji simu. Naingiza wastan Wa buk 5 kwa siku. Nina familia inakula wastan Wa 3000 kwa siku piga hesabu ya 10 kwa wiki.
Tecno naziona kwa wateja
Umejipanga kuzuga mkuu ha ha haaa.

Mtu wa aina hiyo uliotaja hawezi hata kuchungulia humu na hata ukimlazimisha hatokuelewa yani
 
Nakumbuka mwaka jana nlikua na m180 but now balance inasoma m136 nataka nijenge fasta itaobak nifanye biashara yoyote zisije zikaisha
Mkuu wastani wako wa kukata kwa hiki kipindi sio m baya kua makini kwenye matumizi ya ziada.

Wengine tulikua hatujui hata burudani ni nini lakini kwa hii hali imebidi tuonekane huko afadhali watu waseme ulizitumbua kuliko hujazila na hunazo tena aghhhhhhr pesa ni mbaya sana zikikata kona asee
 
Kweli mkuu,binafsi hii thread nimeipenda na katika usomaji wa michango ya wadau nasoma bila kuacha kitu,inanipa somo kubwa katika maisha ya utafutaji japo najua ila nahitaji kujua zaidi wapi? tunapokosea
Mkuu pesa haina kinga iwe kuingia au kutoka.

Kuna watu acount zilinona huku atujui ata bei soda.

Unazipanga kaa matofali ikizidi hamsini sio inaliwa bali inaenda tafutiawa miatisa hamsini ili ijae.
Upepo unapo geuka hutaamini.

Ajabu wala bata wako poa tu
 
Wengi wa watu walipitia mafanikio makubwa sana na tunajuta...Anasa na starehe nzuri ni zile unakula na familia ukubwani maana hapo ndipo umuhimu wa pesa na uhitaji wa pesa unapoonekana...vijana hakikisheni mnaweka pesa zenu kwenye Asset na sio Liabilities....nunua viwanja kadri uwezavyo...wekeza kwenye mashamba hata kama ulimi sasa hivi... kula bata kwa akili sio kwa sifa ili watu wakuone.

Wanaokusifia sasa ukifilisika haohao wanakucheka na kukudharau.
 
Back
Top Bottom