Tuliowahi kupata pesa na kufilisika/kufulia, tujikumbushe hapa

Huu uzi unatia hata moyo, wakati wamechoma 10M, wengine 200M+ ila hawakukata tamaa.

Ila wengi ni pombe na wanawake vilihusika.

Mimi ni last week 4.5M, imekata kwenye bata sasa sina kitu usiku nikikumbuka jasho linanitoka tu..

Najipiga kifua, najiona mjinga kumbe kuna wenzangu waliumia zaidi.

Huu uzi unafundisha pia jinsi gani, ujana ulivyo mgumu kuuvuka bila msaidizi wa karibu aliyepitia, ila akikueleza unamuona huyu nae vp, aniache bwana kimoyo moyo.

Hahaha.
 
Ni kweli wanawake na pombe vinafilisi wanaume wengi.

Ni hatari sana
 
Duh 4.5M imekata kwenye bata wiki iliyopita, watu mna hela
 
Kwenye huu uzi ukisoma matukio mengi mengine ni ya kutunga ambao awajakamata hta milioni 1, wengne ni kweli wamezikamata na kuishia kuteseka, yote kwa yote ni bora uanzie msoto alafu Mungu akupe utakua umepata Elimu flani ya maisha, nilianzia mtaji wa laki5 mwaka2006 nilikua nachukua2 marudio ya mkonge (from Tow ) nadunduliza Kwenye viwanda vya magunia, leo hii Historia ni nyingine kbsa inahitaji vitabu na vitabu kuandika NAMSHUKURU MUNGU
 
Story yako Ni ya uongo pia.
 
Laana ya machozi
 
Mlio rudi kwenye gem tustuwane wakuu

Sioa lazima iwe kama ulivokua walau utoke kwenye msoto tu tupeane mbinu
Bahati mbaya sana kuna ambao wakisha lost hua hawaji kurudi kwn gemu

Kuna bro wangu mmoja enzi za JK alikamata mradi fulani serikalini aisee jamaa nadhani ndani ya 2 years alichezea kati ya 400 -600m au zaidi. Piga sana pombe na starehe za kila aina.

Amekuja kutemwa hana hata ki starlet wala kiwanja achilia mbali asset nyingine. Mbaya zaidi ile kitu ni kama ilimu affect kisaikolojia ikawa hata akipata kazi nyingine anaona hela ni ndogo anaacha. Mpaka leo jamaa bila bila yupo anakunywa pombe za kienyeji mpira karudisha kwa kipa😞
 
Yule dogo zile Hela sepenga alimkamua sana

Uzuri yule alishtuka mapema.

Ila nadhani mitikasi anayopiga na Dili anaxopata za matangazo ameshamake nyingi zaidi ya zile.
 
Tumuombee lakini anahitaji psy therapy
 
Kufilisika jamani hili neno naliogopa, hata kulitamka tu natokwa na machozi. Mwaka 2021 ulikuwa mbaya sana kwangu.
Hii ndo imenikuta baada ya kupata promotion ghafla,mambo fulani yakatokea ikabidi nifukuzwe hata nssf yangu kuipata imekuwa shida.Nipo najifariji na huu uzi japo naamini ni suala la muda nitapata kasehemu kakupata ridhiki.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…