Tuliowahi kupata pesa na kufilisika/kufulia, tujikumbushe hapa

Tuliowahi kupata pesa na kufilisika/kufulia, tujikumbushe hapa

Bahati mbaya sana kuna ambao wakisha lost hua hawaji kurudi kwn gemu

Kuna bro wangu mmoja enzi za JK alikamata mradi fulani serikalini aisee jamaa nadhani ndani ya 2 years alichezea kati ya 400 -600m au zaidi. Piga sana pombe na starehe za kila aina.

Amekuja kutemwa hana hata ki starlet wala kiwanja achilia mbali asset nyingine. Mbaya zaidi ile kitu ni kama ilimu affect kisaikolojia ikawa hata akipata kazi nyingine anaona hela ni ndogo anaacha. Mpaka leo jamaa bila bila yupo anakunywa pombe za kienyeji mpira karudisha kwa kipa[emoji20]
Dah![emoji22]
Kuna MDA unaweza hisi umerogwa
 
Hii ndo imenikuta baada ya kupata promotion ghafla,mambo fulani yakatokea ikabidi nifukuzwe hata nssf yangu kuipata imekuwa shida.Nipo najifariji na huu uzi japo naamini ni suala la muda nitapata kasehemu kakupata ridhiki.
Kufilisika hakutakiwi kakuchukulia negative Sana, kuchukulie Ni Changamoto ya kusonga mbele ili upate Nguvu ya kurud kwny game
 
Nlifilisika kabisa kipind cha korona biashara ilikuwa ngumu had nikauza frame kkoo, mke akaniacha , wana na baadhi ya ndugu walinicheka asa ivi nimerudi kwenye form hao hao wanaomba msaada nawazoom tu, uyo mwanamke anajifanya mwema asa ivi kunishaur sina kinyongo na mtu ila nimewajua vizur yupi wangu yupi si wangu.
Ukifilisika ndo utajua Nani mchaw wako
Binafs sinaga moyo wa huruma.

Nafunga vioo kabisa. Inabaki salamu TU.

Kila nikiombwa Ela, jibu Ni "Sina hela"
Watajiongeza wenyewe kua jamaa hataki shobo
 
Mwaka 2011 soko kuu mwanza nikiwa ninauza nafaka zikiwemo karanga, njugu, choroko,dengu,ufuta,ulezi,uwele,mtama,maharage na kunde.

Kamtaji kalivyokuwa nikawa naendea karanga tabora tani kadhaa nauza jumla. Nilipata pesa kwa njia hiyo. Basi kufkia December karanga zikawa chache Sokoni hivyo mwenye nazo alipiga pesa balaa.

January 2012 nikaingia poli kusaka karanga mpya ili niwahi bei sokoni. Basi nikapata kama gunia 30 (tani 3). Kufkisha Sokoni ziligombaniwa kama nyama. Nikaona pesa si hii apa. Nikazoa msingi wote around kama 22.8m. ili nikapige mkupuo mmoja nije nitulie.

Kuleta mzigo nafika Sokoni nakutana na fuso 6 zinashusha mzigo. Sasa kila mmoja ashajua ni dil acha bei ishuke. Nilijikuta karanga nimezinunua 2300 natakiwa niziuze 1600. Sasa nilipoharibu nikapiga mzigo stoo kwamba bei ikikaa sawa nitauza duh! Kumbe mzigo si haujakauka vizuri, nilikaa kama wiki nafungua stoo nakuta mzigo wote umevunda... Duh!
Pole Sana mkuu
 
Mimi binasfi cjawahi filisika lakin nakili wazi kabsa kma asingekuwa mke wangu kuniongoza vema kwenye mambo ya kheri mhhh bac mpaka sasa ningekuwa nishafilisika zamaaaaan!! Mwanamke wangu shujaa wangu hela natafuta mimi lakin matumiz napangiwa hela inayobaki tunafanyia jambo la maana kabsa ningekuwa mimi mwenyewe nicngeweza
Hongera Sana,
Sisi wake zetu kila Jambo wanatuskilzia tunasemaje,
Changamoto ikija Hana hata wazo la kukupa.
Unasimama kiume maisha yanaenda
 
Mimi binasfi cjawahi filisika lakin nakili wazi kabsa kma asingekuwa mke wangu kuniongoza vema kwenye mambo ya kheri mhhh bac mpaka sasa ningekuwa nishafilisika zamaaaaan!! Mwanamke wangu shujaa wangu hela natafuta mimi lakin matumiz napangiwa hela inayobaki tunafanyia jambo la maana kabsa ningekuwa mimi mwenyewe nicngeweza
Huyo ndio wife material
 
Mimi story yangu Ni ndefu zaidi, hila nilikuwa na mtaji wa Kama milioni 120, utawala wa Magu mtaji wote ulikata na kesi juu,

Tulipewa economic case na money laundering, tulikaa keko na segerea miezi mitatu + ,

Yaani biashara za halali lakini zilituweka jela na makesi juu, tuliweka wakili akawa tapeli, tukajapata wakili mwingine alitupambania mwisho wa siku kesi iliisha na miguu juu wote mam'ae,

Sasaivi kidogo ramani zinaanza kusoma baada ya kuingia huyu mama
 
Miezi saba mkuu
Pambana mzee upate mafao yako muda mwingine unapoenda ofisi zao unawakazia katika namna nzuri mwisho wa siku mambo yako yanatiki.

Kama unahisi Kuna mtu anaweza kukupa msaada kwenye hiyo kampuni usisite kumface kama ni meneja au staff yoyote yule ila kama Bado ngumu unaenda hata Kwa mkuu wa wilaya.
 
Pambana mzee upate mafao yako muda mwingine unapoenda ofisi zao unawakazia katika namna nzuri mwisho wa siku mambo yako yanatiki.

Kama unahisi Kuna mtu anaweza kukupa msaada kwenye hiyo kampuni usisite kumface kama ni meneja au staff yoyote yule ila kama Bado ngumu unaenda hata Kwa mkuu wa wilaya.
Asante mkuu
 
Mimi ndio ngedere kabisa nilifanya kazi kwenye kampuni ya gas ndani ya miaka mi3 nilipata kama milion 10 nikanunua pikipiki ya kutembelea nikawa kazi yangu kuwafata mademu na kwenda kula bata beach demu nikimpata mtandaon hata awe anakaa Kibaha namfata na pikipiki kiukwel sikuamini kama ile hela ingekuja kuisha nilikuwa naiona nyingi sana kumbuka mii nmetokea familia ya kimasikin hivi nnavyoandika hapa nmerudi naishi home kwa baba na mama sina hata mia mfukoni
Daah
 
Duh,sikuwah kupewa hela,sikuwah kuomba mtaji ila nilipiga kbarua nikapata 8000 (elfu nane) nikaanza biashara ya kamba za simu,nikauza kila siku napata faida 4000 -5000 nikameki mpk ikafika laki na nusu,nikaanza kununua na housing za simu,biashara ikanenepa mpk kufika laki tano,nikafungua kibanda cha mbao,nikaendelea kdgo kdgo nikapata compiter nikaanza kuweka mziki,nikakomaa kama mwaka hiv,kipimd kile kuweka mziki mmoja jero bas kwa siku napata 20k ikipungua snaa 15k,nikaanza kuweka simu moja moja huko nje ya mji,nikauza kama sina akil nzur,nikafukisha mtaji wa milion 4,kiukwel nikaingia kwenye frem,we bwana wee wacha nikomae muuza simu maaruf,nikakomaa nikawa na nyumba na kagar vitz,CHA kunisogeza mjini,nikakomaa hvyo hvyo kuja kutamalaki nina zaid ya milion 20,nikaanza kukopesha watu kwa riba,unakuja na gari na kadi nakupa hela,aisee nikapiga mihela kila siku na maisha yakawa safiii.



Balaaa lilipoanzia...

nikapata mchongo wa madin kule tanga sehem za kigongoi na kigwase,sina uzoef,siyajui madin wala sijui soko,hapa ndo penye tatizo kwa weng,naletewa madin hata kuyakagua sijui halaf naemtegemea kumbe nae hajui tunanunua mabov tu,najua tunaenda kupata hela town kumbe naenda kuumizwa,sikukata tamaa,nikafanya tena na tena lakin wap,mwsho nikakuta nimepoteza karib milion 17 bila faida,nikaona isiwe tabu,nikaanza kuchimbisha watu mm mfadhili,nikapiga piga hela ikakata,nikaangalia nyuma na kuangalia nilipo anguka nikajua ni uzoefu na utaalam wa madin sina,nikaendelea kukomaa nikauza gar,kupeleka hela mgodin holaaa,duka nimefunga,mtaji umekata,na sina mbele wala nyuma...
Mm mwanaume nilianza sifir nikapata hela sasa nikaenda kwa wakwe zangu nikawaomba nimwache mke pale miez sita kuna mahali nahitajika,kosa waliloffanya ni kukubali,bas baada ya kumwamishia mke pale na mtoto nikaondoka nikaipiga nyumba bei,nikauza kila kitu bila mke kujua,nikapata kama 22m maana niliiuza sbu ya uharaka nyumba yenye thaman zaid ya 40ml. Nikasepa zang mgodini,asee yaliyonikuta nikachanganyikiwa zaid,nikaitumbukiza hela na haikurud hata mia zaid ya maden,nikabakiwa mikono mitupu,nyumba,duka,gar,mke sina kwa kipind hcho japo mke najua nikirud ntampata. Nikamtapele jamaa mmoja laki na nusu nikakimbilia mbinga songea kulima mahind vibarua maana naona aibu ya kurud,nikapiga msimu wa kwanza nalala kwa mshakaji wng kimya kimya dunia haijui nilipo,nikaomba nami heka moja nilime mazao yangu,nikakomaa haswa asee duuuh achen asee maisha haya,bas nikapata gunia tisa nikazilipua fasta gunia moja 20k nikasepa zangu tabora,maana nina ifaham kwa kias,nikapata dili la asali,watu wana asali pa kuiuza kwa dar hawapajui nikaona fursa hii,nikawaambia mm ninamteja dar twenden,tukaja mpka dar[emoji3] [emoji3]

nilipo fufukia
,nikawapeleka kwa mshakji wakauza asali ya milio 9 kama sikosei,wakakosea wakanipa laki tano,nikawaambia kaleten nyingine najua pa kuuza bei kubwa zaid,wakaenda huko wakakusanyaaaa za nyuki wa kubwa na wadogo,kuleta mzigo nam nilikua nimepata jamaa muhindi anainunua,bas kushusha tu mzigo hela hizo,genji yangu na ujanja nikapata 2ml. Nikasema nipange chumba kulala kwa washkaji nimechoka,nikapanga chumba tabata liwit uswahilin,kila wakileta mzigo dar mm ndo mjanja wao napata laki tano mok milion,muda wote mke hajui nilipo wala namba zang hana na niliamua makusud kukaa hvyo,baada ya miaka mitatu ya asali nikajikuta nina zaid ya milion 4,nikaanza tena kurudia biashara yang ya zaman japo nilikua na mtaji lakin soko lilikua shida,nikaona niwe mbunifu zaid,nikakomaa na biashara ya kutembeza mpka nikafungua tena frem,bas bhna mungu akivyo wa ajab,naletewa simu za ishu kutoka nairob nauza jumla jumla siku mbili sina kitu,biashara ikarud kwenye mstari,nikanunua sehem kule pugu shule ya sekondar nikaanza kuinua kdgo kdgo,mpk nilipohakikisha nimepauwa ndo nikarud kumsalimia mke na mtoto,zaid ya miaka mitatu nilivyokua mkimbiz ndan ya nchi yngu. Kiukwel leo naweza kwenda popote,muda wwte,naweza kula cchte,naweza nunua ving ambavyo watu wanataman kua navyo,wala sitok jasho,nilale,niamke hela napata tu,japo uchum umebadilika lakin siwez kushindwa kuyamudu maisha kwa hali yyte kwa sasa,na mwaka jana nilitaka kujenga shule ya awali mpk sekondar sema kuna ukiritimba flan nikakutana nao nikaghairi. So anaefilisika usimcheke hata siku moja maana anauwezo wa kurud barabarani na akafanikiwa zaid.
[emoji2936]
 
Tafuta kitabu kinachoitwa ''The anatomy of failure'' cha Praise George. Utajifunza mengi sana mle. Soma piakingine cha The Law of Success by Napoleon.
Utagundua why people fail.
Nimekitafuta law of success
 
Back
Top Bottom