Tuliowahi kupata pesa na kufilisika/kufulia, tujikumbushe hapa

Wosia wa masaa 7 πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Mwaka 2020 ni mwaka ulio nipiga mpaka leo sijatengamaa ile corona ile dah kwangu naonaga ni mwaka wa shetani kwangu.
Kuna ndugu yangu alikua anafanya kazi zanzibar, kwa siku alikua analipwa 35 na hayo matips hadi laki anaipata kikawaida kabisa kila akienda kazini, ilikua kwenye ma hotel haya ya kitalii.

Hii corona ilivyoingia zanzibar walikua very strictly kidogo, na wazungu wakaisha kabisa.

Mwamba alifilisika kiasi kwamba akarudi hapa dar akawa dereva bodaboda mpaka leo hajasimama tena. Kila ukiongea nae anailaumu sana hio corona.
 
Very trueπŸ™ŒπŸΎ
 
@Maxence melo
 
Nikiwa chuo nilipataga mkopo, lakini kukawa na hitilafu Fulani boom wakawa hawaniingizii. Nikaendea kufuatilia. Kufikia mwaka wa pili wa masomo wakaniingizia maboom yote at once ambayo sikuwa napewa. Mama yangu! Mwisho wangu wa kushika pesa ndefu ilikuwa ni laki moja, Sasa akaunti ikasoma milioni 2 kama na laki nane hivi. Ilikuwa mtu akilia shida kidogo tu nachomoa hata elfu50 Nampa.

Mwaka wa pili wa masomo haukuisha pesa zikapukutika zote. Nikawa kama kuku tu, lilikuwa fundisho kubwa sana na majuto sana. Nilipomaliza chuo nikawa na adabu sana na pesa.
 
Tinder, badoo na hi5 zinawangamiza vijana
 
Your best teacher is your last mistake...mimi niliajiriwa mgodi x take home ilikuwa 760k ilikuwa wazee wakinipiga vizinga kutoa 100k ni kawaida sana mara paap! kibarua kikazima kama mshumaa savings sikufanya aisee hao hao ndo wakwanza kusema "hata akiba alikuwa hajiwekei"..ila now nimekuwa mgumu sana kutoa pesa kizembe maisha ya kitaa yamenifunza aisee

NB: "THE WORST OF NOT HAVING MONEY IS HAVING IT AND LOSING IT"
 
Pole sana Mkuu eti baada ya 2 weeks huna ht Mia mbovu πŸ˜†πŸ˜†
 
Huyo hajafilisika alikua mzembe na mwizi tu.
Kazi ya hoteli kupata laki kwa siku sio tipu ni wizi tu humo.
Sasa angejiandaa vizuri mtaani hata bila kuilaumu corona ingefika siku kazi angefukuzwa.
 
Mkuu nimefukuzwa kazini kwa madai ya utoro maana nilipata issue moja,emergency nikaomba ruhusa nikanyimwa ikabidi nisepe hivo hivo,hasa kupata barua ya termination hawataki kunipa.
Hivyo na nssf yangu ngumu kupata

Mkuu kama una vielelezo vyote kawashtaki labour usiogope mkuu utapata haki yako.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…